Mambo matano ya kushukuru

Mambo matano ya kushukuru

Kwa nini mara kwa mara unaweza kuwa mwenye shukrani na mwenye furaha, bila kujali hali yako ama unavyojihisi.

20/3/20175 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Mambo matano ya kushukuru

Siku zote maisha si rahisi. Siku zingine mambo yote huenda ovyo na unahisi kwamba haiwezi kuwa mbaya Zaidi. Nyakati nyingine mambo huenda vyema na maisha unayahisi kuwa mazuri. Lakini wewe unaeishi kwa ajili ya Mungu, unaweza kuwa na shukrani kila wakati – bila kujali unavyohisi.

“Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika kristo.” 1 Wathesalonike 5:18

Mawazo yenye shukrani yana athari kubwa maalumu kwetu sisi. Ukosoaji, kulalamika na mawazo ya giza hukimbia unapochagua kuwa mwenye shukrani hata katika hali mbaya Zaidi. Je! Hii si silaha yenye kutumika ambayo unapaswa kuwa nayo maishani mwako?

Kila mara una jambo la kushukuru, bila kujalisha mahali ulipo wala unavyohisi. Soma Zaidi kufahamu hasa hiki ni nini!

1.      Umeapokea uzima!

Kwamba u mzima si tu kwa sababu ya nafasi. Mungu amekupangia uzaliwe na uishi duniani kwa muda mfupi, na anataka uishi maisha ya furaha. Wale wanaoishi maisha yao kwa kufuata mapenzi ya Mungu, wataona kwamba hivi ndivyo ilivyo kabisa!

Si tu kwamba anakupa uzima, lakini pia hukupatia ushauri mzuri wa namna ya kuishi. Hupaswi kutilia shaka hili. Unachopaswa kufanya ni kufungua biblia kutafuta sheria za Mungu, na zote ni za kweli kwa 100%. “ Anayebariki wengine hubarikiwa sana .” Mithali 11:25. “Kwa maana, atakayependa maisha, na kuona siku njema, auzuie ulimi wake usinene mabaya, na midomo yake isiseme hila.” 1Petro 3:10.

Fikiria kwamba Mungu anakupenda sana kwamba alikupa uzima, eneo zuri la kuishi (Dunia) na sheria zake kamili kuishi ndani yake. Hili ni jambo la kushukuru sana!

2.      Kamwe hauko peke yako

Watu wengi wapo katika hatua moja katika maisha yao huhisi kwamba hakuna mtu anaewaelewa, hakuna mtu anayewafahamu, hakuna mtu anayejali. Lakini unapaswa kujua kwamba kila wakati una rafiki, mtu ambaye hukusaidia na una baba ambaye yu pamoja nawe. Bila kujali unapoishi, unapoenda na unachofanya, Mungu yupo hapo. Yupo kwa ajili yako. Daudi anaandika juu ya hili;

“Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu; umelifahamu wazo langu tokea mbali. Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu, umeelewa na njia zangu zote.” Zaburi 139:2-3.

Mungu hukutazama, hukusaidia. Anakupenda hivyo hawezi kukuacha uwe mpweke. Ni salama kuwa karibu nae. Hili ni jambo la kushukuru.

3.      Unaweza kujawa na furaha wakati wa majaribu

Hakuna mtu anaishi bila kupitia mateso. Hali ngumu majaribu yanapokuja, unaweza kujaribiwa kutilia shaka kwamba Mungu anajua lililo jema kwako, kwa kuwa ameacha mambo haya yatokee. Lakini Mungu anajua kilicho bora kwako, kwa sababu anataka kukufundisha kwa kupitia majaribu haya, ili mwishoni uweze kushiriki katika asili ya utauwa. (Yakobo 1:12; 2Petro 1:4.) 

Mungu anajua hali gani unapaswa kuwa nayo kujiandaa kwa ajili ya mbingu. Kama unaamini hili, unaweza kujawa na furaha hata unapokuwa katika ugumu ya kibinadamu. Wanachohofia wengine, makwazo na kuwa na uchungu, inaweza kuwa kitu chanya kwako.

Katika majaribu unaona maumivu yako, hasira, tuhuma, wivu, mapenzi yako mwenyewe n.k., na kwa kutokujitoa kwa dhambi hizi, taratibu utamalizana na dhambi hizi katika asili yako. Ndipo utapata tunda la roho maishani mwako! Hivyo kuna sababu kubwa kujawa na furaha wakati wa majaribu – kwa kuwa hukuleta karibu na mbingu.

“Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa Imani yenu huleta subira. Subira na iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.” Yakobo 1:2-4.

Fikiria kwamba una sababu ya kuwa na furaha juu ya mambo ambayo wengine huyaona kama mzigo! Mungu anajua unachohitaji na hukusaidia kwa njia yote! Hili ni jambo la kushukuru.

4.      Mungu anakupenda sana

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Yohana 3:16.

Kifungu hiki ni kwa ajili yako: “Mungu alikupenda hata akamtoa mwanawe wa pekee, ili wewe umwaminiye usife bali uwe na uzima wa milele.” Mungu aliwaza juu yako alipomtuma Yesu, mwanawe mpendwa duniani kuwa mwanadamu ili uokolewe. Kupitia Yesu unaweza kupata msamaha wa dhambi zote ulizotenda na kuanza upya. Unapata nafasi ya kuishi kama Yesu mwenyewe, huru kutoka katika dhambi zote! (Warumi 6:22) Mungu anatafuta kuwa na ndugu kama yeye – wale wanaomfuata na kutafuta mapenzi ya Mungu katika mambo yote.

Mungu anatupenda sana kiasi kwamba alimtoa mwanawe sadaka, Yesu, aliyefanya iwezekane kwamba tusitende dhambi tena. Hilo ni jambo la kushukuru.

5.      Una baadae yenye tumaini

Unaweza kuitazamia baadae! Unapokuwa umemkabidhi Mungu maisha yako yote na mapenzi yako yote una baadae yenye tumaini, katika maisha na katika uzima wa milele.

Siku moja utakutana na Yesu tena. Na utakutana na wengine walioishi maisha ya kiuanafunzi kama ambavyo unayoishi, na mtajawa na furaha pamoja nao! Baada ya hapo unaweza kuwa katika dunia mpya ambapo roho wa Mungu mwenyewe atatawala na hapatakuwa na dhambi tena. Kila jambo katika dunia mpya hutokea kwa Imani, tumaini na upendo. (Ufunuo wa Yohana 21:1-3; 1Wakorintho 13:13.)

Ikiwa umeishi kwa ajili ya Mungu hapa duniani, unaweza kuitazamia siku ambayo utakuwa na Yesu. Fikiria kuhusu kuchaguliwa kwa ajili ya jambo kama hili! Ni tumaini kiasi gani! Hili ni jambo la kushukuru sana!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya Janne Epland awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ na imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.