Hatari ya kusengenya

Hatari ya kusengenya

Maneno yana nguvu. Yanaweza kujenga na kubomoa

6/3/20175 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Hatari ya kusengenya

9 dak

Watu hupenda kujua na kushiriki uvumi na siri. Mara nyingi hawafikirii kama ni ukweli au uongo. Huongeza maelezo na uongo hapa na pale ili waweze kupata mwitikio sawa. Huwa wanakuwa wasimuliaji wabaya sana. Wanataka kujua kuhusu ugomvi na kutoa maoni yao.

“Tena anagalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, kokote anakoazimia kwenda nahodha. Vivyo hivyo ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivunia majivuno makuu. Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana.” Yakobo 3:4-5

Masengenyo: Ujumbe ambao husambaa kama saratani

Watu wengi huona wizi, hasira na wivu kama dhambi, lakini mara nyingi hawafikirii kwamba usengenyaji pia ni dhambi.

“Jiepushe na maneno yasiyo na maana, ambayo si ya dini; kwa kuwa wataendelea Zaidi katika maovu, na neno lao litaenea kama donda-ndugu.” 2Wakorintho 2:16-17. Masengenyo yanaweza kuja kwetu kama kitu cha asili. Mazungumzo rahisi yanaweza kuwa fursa ya kulalamika ama kuzungumza kwa njia hasi kuhusu mtu fulani. Labda tuna kitu dhidi ya mtu fulani na tunataka wengine kushiriki mawazo haya kwa siri, kuongezea mawazo yetu wenyewe ili kuwafanya wengine wakubali, ooh ndiyo yuko kama hivyo,” au “ni hali ya kutisha alivyoondokana nayo.” Kwa kusengenya tunawatia moyo wengine wasengenye pia.

Matokeo ya masengenyo ni ya kutisha: Mgawanyiko, mapigano, tuhuma. Shetani hupenda mgawamyiko. Hupenda fursa ya kuvunja ushirika na umoja. Inatisha namna masengenyo yanavyoweza kubomoa. “Na mchongezi huwafarakanisha rafiki.” Mithali 16-28.

Madhara ya masengeyo hubakia kwa muda mrefu. Kwa kipindi fulani, swala dogo linaweza kuwa kubwa ambalo linaunda ukuta kati ya marafiki.

Kukua katika upendo kati ya mmoja na mwingine

“Tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.” Waefeso 4:32

Kuwa huru kutoka kwanye masengenyo, kwanza tunapaswa kukua katika upendo. Je, maneno yetu yanajenga vifungo vya upendo, ama yanabomoa?

Imeandikwa kwenye kitabu cha Mathayo 12:34: “Maana kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.” Kama midomo yetu ni myepesi kunena maovu dhidi ya wengine, hii inatuambiaje kuhusu mioyo yetu? Ni upendo kiasi gani tulio nao kama tuko wepesi kuongea mabaya dhidi ya wengine nyuma yao?

Tunapowapenda wengine, ni rahisi siyo rahisi kuwasengenya. Malalamiko yote juu yao hupotea. Upendo umeandikwa kwenye 1Wakorintho 13:4-5: “Upendo huvumilia, hufadhili; hupendo hauhusudu; upendo hauatabakari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; hauafurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; hutumaini yote; hustahimili yote.” Kama hii ni aina ya upendo tulio nao kwa watu wanatuzunguka, tungeona wazo fikra ya kuongea mabaya kuhusu wao kama hali ya kutisha.

Tunahitaji kumwomba Mungu atusaidie ili tuweze kukua katika upendo na kuonesha wema na ukarimu juu ya wengine. Kama tunadhani mtu fulani anafanya jambo vibaya, tunaewza kumwombea mtu huyu na Mungu atatuonesha tunavyoweza kusaidia. Labda tunaweza kumfuata mtu katika roho wa upedendo na kuwauliza kuhusu ukweli wa mada, kuliko kuwasengenya. Ni kitu ambacho hakiwezekani kuwa na fikra ovu dhidi ya mtu tunaemwombea, au kumsengenya. Tunapaswa kujikita katika kwenye mambo chanya na kuwa macho kuwaombea wengine. Kwa kushiriki pendo hili, tunaweza kusaidia kuleta amani na utulivu.

Umewahi kusikia uvumi ama Habari kuhusu mtu mwingine? Acha ifie kwako! “Moto hufa kwa kukosa kuni; na bila mchongezi fitina hukoma.”Mithali 26:20. Hata kuruhusu uvumi utembee katika fikra zetu ni hatua ya kwanza ya kupita kuelekea kwenye mgawanyiko na fitina. Uongo husambaa kama moto wa nyikani.

Uamuzi thabiti wa kumalizana  na usengenyaji

Tunapaswa kufanya nini endapo wenzetu wanapoanza kusengenya? Pengine tupo kwenye mazungumzo ambapo watu wanaanza kuzungumza kuhusu mtu mwingine. “He, mlisikia kuhusu alichofanya?”

Kama huwezi kufanya jambo dhidi yake, tupo kama watuhumiwa kama mmoja aliyanzisha. Hatuwezi kuwa sehemu ya masengenyo ili kuwa “maarafiki”. Je, tuna nia ya kupambana dhidi ya hali hii? Tunataka kumalizana na masengenyo?

Watu watajitetea wao wenyewe kwa kusema kwamba wanachosema ni ukweli. Hii siyo sababu! “Kwa hiyo wewe mtu uwaye yote uhukumuye, huna udhuru, kwa maana katika hayo umhukumuyo mwingine wajihukumu mwenyewe kuwa na hatia; kwa maana wewe uhukumuye unafanya yaleyale.” Warumi 2:1. Hata kama kila neno lilikuwa kweli, tunahitaji kukumbuka kwamba kusengenya, kumsema mtu vibaya nyuma yake, ni dhambi! Tukisikiliza masengenyo, pia tuna tuhuma.

Barikianeni na kujenga ninyi kwa ninyi

“Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye uhitaji, ili liwape meema wanaosikia.” Wefeso 4:29

Midomo yetu inaweza kutumika kufanya mengi mazuri katika kubariki na kuwainua wengine, au maovu mengi na kubomoa katika kusema mabaya kuhusu wengine. “Katika kinywa kilekile hutoka baraka na laana.” Yakobo 3:10. Tunapoanza kupambana dhidi ya masengenyo katika maisha yetu wenyewe, tunaweza kuwa mfano kwa wengine. Na watu watahisi kwamba masengenyo ni kitu kibaya. Tunapaswa tujitazamia kila wakati ili tujenge umoja kwa maneno yetu, badala ya kubomoa. “tukiwapenda wengine, tutaishi kwenye mwanga hivyo hakuna jambo ndani yetu litakalosababisha mtu fulani atende dhambi.” 1Yohana 2:10.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya Frank Myrland awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ na imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumia katika tovuti hii.