Kuweza kutazamia siku ambayo nitakutana na Mwokozi wangu na kupokea thawabu ya maisha ya uaminifu, ni mojawapo ya faida kuu za kuwa Mkristo.
Nilipokuwa hata simjui Mungu, Alikuwa akinivuta kwake kwa upole. Sasa namchagua kila siku.
Yesu hayupo hapa duniani kwa kibinafsi, kwa hivyo ninawezaje kuwa mwanafunzi Wake? Ninawezaje kumfuata na kuishi karibu naye?
Nilitakiwa kupigana vita ili kuishinda hali yangu ya uduni, hisia kwamba sikuwa na thamani na sikuwa muhimu kuliko wengine, na kuwa na Imani katika upendo wa Mungu kwangu binafsi.