Ninaamini Mungu aliniita kwa jina langu

Ninaamini Mungu aliniita kwa jina langu

Nilitakiwa kupigana vita ili kuishinda hali yangu ya uduni, hisia kwamba sikuwa na thamani na sikuwa muhimu kuliko wengine, na kuwa na Imani katika upendo wa Mungu kwangu binafsi.

4/4/20185 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Ninaamini Mungu aliniita kwa jina langu

“Kila mmoja hunichukia mimi, hakuna anayenipenda….”

Tuliimba wimbo huu wa Watoto. Tulidhani ilikuwa utani. Nilipofikia umri wa miaka kumi, niligundua kwamba ilikuwa rahisi kufikiri kwa namna hii. Mambo yalipoenda tofauti na nilivyofikiria ama kupanga, au sikualikwa katika tukio Fulani, ilikuwa rahisi kiufikiria kwamba hakuna mtu anaenipenda na kila kitu kilikua dhidi yangu.

Hali ya uduni iliyofikichika, inasubiri kujionesha yenyewe

Kama mtu mzima, niligundua kwamba ilikuwa rahisi kuwaza kwamba Mungu alikuwa ananipinga mambo yalivyoonekana kwenda hovyo katika maisha yangu.Mashaka haya juu ya upendo wa Mungu yamenisu katika maisha yangu. Nimetumia vifungu tofautitofauti kupigana na hili na hii imenisaidia kushinda katika hali fulani. Lakini hali hii ya uduni imekua ikikaa nyuma yangu mara kwa mara. Ujanja ni kwamba shetani huja kama Malaika wa nuru. (2Wakorintho 11:14) Hufanya ionekane ni “unyenyekevu” kuwaza kwamba sipendwi ama siko mwema vya kutosha, au kwamba sijaalikw kwenye mambo tofautitofauti kwa sababu sistahili.

Miaka michache iliyopita, kwa kipindi kifupi, nilipoteza baadhi ya wapendwa wang una nilipoteza matumizi ya  mkono wangu wa kuume jambo ambalo pia lilipelekea maumivu ya mwili ya mara kwa mara. Nilionesha uso wenye furaha kwa wengine lakini ndani yangu nilikua naumizwa. Nilitambua baada ya muda kwamba nilikua nimeacha kuamini kwamba Mungu alinipenda na kunijali haswa. Ingewezekanaje mtu aliyenipenda aruhusu haya yatokee? Mungu yupo kweli? Nilikuwa nimefanya nini kibaya kiasi kwamba nikastairi mateso ya namna hii? Nilihisi kwamba nilikuwa nikivutwa taratibu kwenye giza nene na kukata tamaa na sikujua namna ya kutoka nje. Nilikua napoteza hata hamu ya  kuishi – ilikua ngumu na maumivu na nlijihisi niko peke yangu.

 Vifungu vimeandikwa maalum kwa ajili yangu.

Katikati ya hali hii, Rafiki alitumia muda wake kuniuliza nilivyokua naendelea. Alinitia moyo na kuniombea na kunipa vifungu hivi katika Isaya 43:1-5. Alinifanya niahidi kuvisoma vifungu hivi kila siu na kuweka jina langu pale. Niliahidi. Na hiki ndicho nilichosoma:

“Lakini sasa Bwana aliyekuhuluku ee (Charis), yeye aliyekuumba ee (Charis), asema hivi, usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu (Charis). Upittapo katika maji mengi, nitakuwa Pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, huatateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza. Maana mimi ni Bwana, Mungu wako; mtakatifu wa Israeli, na mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako. Kwa kuwa ulikuwa wa thamani machoni pangu, na mwenye kuheshimiwa, nami nimekupenda; kwa sababu hiyo nitatoa watu kwa ajili yako; na kabila za watu kwa ajili ya Maisha yako.Usiogope; maana mimi ni Pamoja nawe; nitaleta wazawa wako toka mashariki, nitakukusanya toka magharibi.”

Nilisoma vifungu hivi kila siku. Mwanzoni kadri nilipokuwa nikivisoma, nilikua nastajabu kwamba vilikuwa vimeandikwa kwa ajili ya nani kwa sababu ni kwaeli kwamba havikuwa kwa ajili yangu. Lakini kwa utii niliendelea kuvisoma. Taratibu kwa rehema ya Mungu, Imani ilianza kuku ana nilitambua kwamba vilikuwa vimeandikwa maalumu kwa ajili yangu. Mungu alinipenda, alinichukua; ni kweli alifanya hivyo! Ndiyo, ppangekuwa na wakati ambao ningepita kwenye maji na moto, lakini angekuwepo hapo Pamoja nami, kunipa nguvu.

Uhuru!

Ndipo nilipogundua: hii ilikuwa nafasi yangu ya kuingia katika mzizi wa hali hii ya kutoamini na hisia za kutokua na thamani ambazo zimekua zikinipa shida katika Maisha yangu yote, na kuziua moja kwa moja. Hali hii yote ilikuwa rehema ya Mungu ili niweze kuwa huru kutoka kwenye huzuni  iliyokuja  nilipokuwa nikiishi kwa mashaka. Nilikuwa nikihisi kama Ayubu, kwamba kila mtu yuko dhidi yangu, ndipo kifungu kuhusu Ayubu katika litabu cha Yakobo 5:11 kilinijia: “Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia Habari ya Subira yake Ayubu, mmeuopna mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.”

Hii ilikuja kama ufunuo kwangu: Je ninaona matokeo ambayo Mungu alitaka kuyaleta? Je ninaona hali hizi ambazo zilinipeleka katika mwisho wangu mwenyewe na nguvu yangu mwenyeewe, ambapo kiukweli jibu lilikuwa ni maombi yagu? Maombi yangu kwamba nilitaka kuwa huru kutoka kwenye mashaka na kumtumikia Mungu kwa moyo wangu wote? Hali hizi ambazo ningekuwa nimefanya jambo lo lote ili kuondokana nazo zilikua ni kitu ambacho kiliniweka huru kutoka kwenye mashaka. Haya yalikuwa matokeo yaliyopangwa na Bwana. Mambo yote haya yalitumwa kutoka kwa Mungu kwa sababu alinipenda na alitaka niwe huru na mwenye furaha.

Lakini Mungu asungefanya hili litokee kimiujiza; Nilipaswa kuukubali ukweli na kuyashinda mambo haya yaliyonifanya nikose furaha tangu utotoni. Nilipaswa kupigana: kupigana dhidi ya mashaka na kutoamini na kupgiana kuamini katika Warumi 8:28. “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufaanya kazi Pamoja na wale wampendae katika kuwapatia mema, yaani wale walioitwa kwa kusudi lake.” Neno la Mungu lilikuwa silaha yanguna kilikuwa kitu pekee ambacho kilifanikiwa dhidi ya mashaka haya. Hoja zangu mwenyewe na fikra zangu hazikuwa na kazi tena.

Sasa nina amani ndani yangu, kwa sababu hatimae nimeshawishika kwamba Mungu ananipenda; kwamba nina thamani kwake na kwamba anadhibiti na kupanga kila kitu kidogo katika Maisha yangu kwa ajili ya wema kwangu. Sina woga kwa Maisha yangu ya baadae, kwa sababu najua kwamba Mungu ana udhibiti dhidi yake na na atakua na mimi kwa kila kilichopo mbele yangu. Najua bado sijamalizana hali yangu ya uduni, lakini imepoteza nguvu na udhibiti dhidi yangu, kwa hiyo ni suala  la muda tu. Nina shukuru kwa ajili ya neno la Mungu na nguvu lililo nalo dhidi ya giza, na nashukuru kwa kujali na maombi ya wana wa Mungu .

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya Charis Petkau awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ na imechulkuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii