“Mtapokea nguvu roho mtakatifu atakapowajia”

“Mtapokea nguvu roho mtakatifu atakapowajia”

Pengine hiki ni moja kati ya vifungu vya biblia vinavyojulikana katika muunganiko na pentekoste, lakini lengo la nguvu hii ni nini?

17/7/20212 dk

Na Ukristo wa Utendaji

“Mtapokea nguvu roho mtakatifu atakapowajia”

“Mtapokea nguvu”- katika maisha yako binafsi.

Ujumbe wa pentekoste ni faraja kuu kwa wanaoamini hili: “Sikiliza! Mtapokea nguvu roho mtakatifu atakapowajia!” Na hakuwa mtu yeyote aliyenena maneno haya, alikuwa Yesu kristo mwenyewe, muda mfupi kabla ya kwenda juu mbinguni.

Watu wapo tofauti sana. Wengine ni wazuri sana, ambapo wengine ni wasumbujfu na wenye majivuno. Baadhi ni wenye msaada na wenye urafiki ambapo wengine ni vigumu hata kuwa pamoja nao. Lakini kuna jambo moja ambalo liko sawa kwetu sote ikiwa tunataka kuishi kutokana na mafundisho ya Biblia.

Tukiwa waaminifu, kuna hitimisho moja: Usipokuwa mwema kwa kila mmoja, na hakika siyo kwa wakati wote siwezi kusema kwamba upendo huniongoza kila mara katika fikra zangu na maneno”.

“Mtapokea nguvu”- kuishi pamoja kama wakristo katika ushirika

Ungeweza kufikiria kwamba jambo gumu Zaidi ni kumpenda adui yako. Na hivyo ni vigumu. Lakini Yesu alisema, “Hakuna mwenye upendo mwingi kama kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.” Yohana 15:13. Tukiishi pamoja katika ushirika wa kikristo mwaka baada ya mwaka tunajuana mmoja na mwingine vizuri. Lengo ni kwamba tunapendana kama kama dada na kaka (Ndiyo kila mmoja!) kwa mfano kwa kutokua na wivu wala uchungu, ama kufikilia uovu. Kutokuwa na lawama kamwe, bali kujali kutia moyo na kuwasamehe wengine. Tukiwa waaminifu tunapaswa kukubalia: “Binafsi siwezi kuwapenda kaka na dada zangu wote kila wakati, na binafsi siwezi kuwapenda wengine kama Yesu alivyonipenda.” Ndipo ujumbe huu wa Pentekoste ni Faraja kuu:

Lakini mtapokea nguvu, akisha kuwajilia juu yenu roho mtakatifu!” Matendo 1:8

Ndiyo, Pentekoste kweli ni kipindi cha sherehe pamoja na ahadi tukufu na ujumbe!

Soma zaidi kuhusu roho anachoweza kutufanyia: Mambo ya kushangaza ambayo roho mtakatifu anaweza kukufanyia!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita katika Makala ya Jan – Hein Staal awali ilichapishwa katika https://activechristianity.org/ imepewa ruhusa kutumika katika tovuti hii.