Mungu ana kitu fulani anataka kufanya maishani mwangu. Anataka kabisa kunibadilisha niwe kama yeye. “Maana wale aliwajua tangu asili, wafananishwe na mfano wa mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.” Warumi 8:29. Na anaweza kufanya Zaidi ya hayo. Ila ikiwa yote ninayoyaona ni kwa jinsi nilivyo kama mwanadamu, jinsi gani vitu vilivyokuwa zamani, asili yangu mwenyewe ya dhambi,familia “dhambi” iliyorithiwa, ikiwa ni kama ninakubali hii ni jinsi gani nilivyo, na kufikiri siwezi kufanya chochote, hivyo ninamuwekea mipaka Mungu. Hivyo hawezi kunibadilisha.
Kubali ukweli na uwe na imani
Ni kweli kwamba nimekwisha kubali ukweli kuhusu jinsi nilivyo. Ninaona jinsi ilivyo sasa, ndio. Lakini inahitajika kuwa na Imani. Ninatakiwa kuona jinsi gani itakuwa ikiwa nitajitoa kwa Mungu. Sio mimi ninayekwenda kufanya mwenyewe, ila Mungu anakwenda kufanya vitu ndani yangu. Lakini ninapaswa kuwa kuwa tayari kutoa 100%. Ninatakiwa kubadili mtazamo wangu kutoka kukubali jinsi nilivyo kuwa mtazamo kuwa na imani. “Basi Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana” Waebrania 11:1
Imeandikwa katika Jeremia 29:11 “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho” ikiwa ninaamini kwamba haya ni mawazo ya Mungu kwangu, hivyo ninapaswa kuwa na fikra hizohizo kwangu. Ndio, ni kweli kwamba huenda nina “dhambi” fulani filani ambazo zimenishikilia kwa ukaribu. Lakini tu ni kwa sababu iko hivyo sasa, haimanishi kwamba itabaki hivyo. Mungu atanisaidia na kunipa zana na nguvu kushinda mambo hayo endapo siruhusu hoja za kibinadamu na fikra zangu za kibinadamu kunirudisha nyuma. Nikiwa na imaini ndani yake na tumaini la baadaye.
“Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu; bali kwa damu ya thamani ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.” 2Petro 1:18-19.
Yeye hufanya kazi na mimi binafsi na kwa njia binafsi. Hivyo siwezi kiutazama pembeni nakuona namna anavyofanya kazi na wengine na kuyalinganisha maisha yang una wao. Wanapaswa kuwa watiifu kufanya kile Mungu anachotaka wafanye na kuwa vile Mungu anataka wawe, na nipaswa kufanya hivyo pia.
Mungu anaweza kufanya kitu kipya ndani yangu
Pengine inaweza kuonekana kama ni muujiza kunibadili kutoka jinsi nilivyo. Ninajijua mwenyewe na ninajua ya kuwa kuna mambo yananyoonekana kama hayawezekani kubadilika. Lakini je, hatumtumii Mungu wa miujiza? Mungu ambaye ni muumbaji wa vitu vyote anaweza kufanya kitu kipya kabisa ndaini yangu. Ninapaswa tu kuwa na nia na kuamini.
Yesu alikuja na alituonesha njia. Ninapaswa kujikana mwenyewe, ninapaswa kusema hapana ninapojaribiwa kutenda dhambi, dhambi inayokuja kutoka kwenye asili yangu ya dhambi. Ninapaswa kuacha mapenzi yangu. Ninapaswa kujinyenyekeza. Ninapaswa kushikilia neno la Mungu.
Na ninapojihisi kwamba siwezi kufanya hivyo, ninapaswa kuamini maneno haya: “Na akaniambia, Neema yangu yakutosha ; maana uwezo wangu hutimilika katika udhaifu…. Ili uwezo wa kristo ukae juu yangu. Kwa hiyo napendezwa na udhaifu, na ufidhuli, na misiba, na adha, na shida, kwa ajili ya Kristo. Maana niwapo dhaifu ndipo nilipo na nguvu.” 2Wakorintho 12:9-10
Na ndipo mabadiliko huanza kutokea maishani mwangu. Ninakuwa huru. Ninagundua kwamba sipaswi kubaki kama nilivyo wa asili. Katika hali ambayo kipindi fulani ningekuwa nimetengenezwa katika hali fulani, sipaswi kuguswa kwa namna hiyo tena. Badala yake naweza kuguswa na tunda la roho. Naweza kuwa mtu ambaye Mungu anataka niwe. Ninakuwa mwenye furaha kama mawazo yangu yataacha kuwa ya kujifikiria mwenyewe, na kuanza kuwaza mawazo ya Mungu.