Muwe wema ninyi kwa ninyi

Muwe wema ninyi kwa ninyi

Sote tuna sababu njema kuwa wema sisi kwa sisi na kuonesha huruma na uelewa.

4/12/20172 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Muwe wema ninyi kwa ninyi

2 dak

Muwe wema ninyi kwa ninyi!

“Tena kueni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.” Waefeso 4:32.

“Kwa pendo la ndugu, mpendane ninyi kwa niniyi..” Warumi 12:10.

Kwa ujumla, watu wana mioyo migumu kwa kiasi kikubwa ama kidogo. Hii hutoka katika dhambi. Na tunahitaji kuokolewa kabisa kutoka dhambini, na kubadilika kabisa kabla kuwa wenye moyo mwema kwa wengine.

Moyo mwema ni nadra sana. Kuwa na moyo mwema tunapaswa kuwaelewa wengine na kuwa na huruma.

Ukweli ni kwamba tuna asili sawa ya dhambi na tabia ndani yetu kama watu wengine, na tumeshuhudia kwamba ni vigumu kuzishinda tabia hizi za dhambi. Hii ndiyo sababu kwa nini  tunapaswa kuwa na huruma dhidi ya wengine wanapoanguka.

Ni vibaya kabisa kusema, “Siwezi kabisa kuelewa kwamba amefanya hiki ama kile!” badala yake, tunapaswa kusema: “Hii inahuzunisha sana, lakini naelewa kabisa, na nina sababu ya kuonesha huzuni na uelewa.” Ndiyo, hebu fikiria kama ingekuwa wewe ama mimi!

Sote tuna sababu njema ya kuwa msimamo katika kutafuta kuokolewa kutoka kwenye magumu yote. Ndipo inakuwa kawaida kwetu kuwa moyo wenye huruma sisi kwa sisi kwenye maisha ya kila siku. Inaweza kuwa hivyo

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya Elias Aslaksen ambayo awali ilionekana kwa kichwa cha Habari “Tenderheartedness” Kwenye jarida la BCC "Skjulte Skatter" (Hazina zilizofichika) Februari 1966. Imetafsiliwa kutoka kwenye Kinorwe na imepewa ruhusa kutumika katika tovuti hii.