Namna ya kupata kanisa la kweli

Namna ya kupata kanisa la kweli

Nawezaje kupata kanisa sahihi kati ya mengi?

22/6/20175 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Namna ya kupata kanisa la kweli

Biblia inazungumza kuhusu “Kanisa” kwa sababu, kama wakristo, tunahitaji kuwa Pamoja na waumini wengine wenye Imani sawa. Hii hujenga Imani yetu, na neno la Mungu linatuambia kuwa Pamoja mara kwa mara kadri tunavoona siku za kurudi Kristo zinakaribia. (Yuda 1:20; Waebrania 10:25.)

Lakini swali ni: Je! Tunapataje kanisa la kweli kati ya mengi? Kuna maelfu ya makanisa ya kuchagua.

Kanisa la kweli la kikristo

Chaguo ni gumu kwa kweli kwa kuwa kila kanisa linasema kwamba wamejengwa katika “mfano wa Biblia”au katika “msingi wa kitume”. Wote wanaweza kuonekana wema na mara nyingi kunakuwa watu wema wengi katika makanisa haya. Muda mwingi kunakuwa na shughuli mbalimbali, kitu ambacho ni kizuri, lakini swali ni, “Je! Ni kweli wanafanya Yesu alichofundisha?”

Mimi mwenyewe nilikuwa katika kanisa ambalo lengo lao kubwa lilikuwa ni kubisha Milango na kueneza injili. Hili si kosa, lakini ilikuwa ni jambo pekee ambalo lilikuwa muhimu katika kundi hili. Ni sawa kweli katika kanisa jingine nililokuwemo. Walikuwa wakiwalisha maskini, na hapakuwa na kosa kwa hili, lakini hiki ndo kitu pekee walichoweza kutoa.

Yesu alitupa kazi ya kuwafanya wanafunzi mataifa yote (Mathayo 28:19) na Yesu na mitume wanatuambia kuwajali wahitaji, lakini shughuli hizi lazima zitoke katika kuishi Maisha ya kipekee ya haki, na hivyo ndivyo injili inavyohusu.

Paulo alimwandikia kijana Timotheo, “Jitunze nafsi yako na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia.” Timotheo 4:16. Mitume waliandika mengi kuhusu kuja katika Maisha ya utauwa nan jia ya kufikia Maisha haya. Paulo anauita mchakato huu “Kufa kwa ajili ya Yesu” kunakopelekea uzima. ( 2 Wakorintho 4:10), na Patro anazungumza kuhusu “Kuteseka katika mwili na kuacha dhambi” (Petro 4:1), wakati Yohana anasema, “Nawaandikia haya, ili kwamba msitende dhambi.” (1 Yohana 2:1) Na Yuda anatuonya tusitumie Neema kama kisingizio cha kutenda dhambi. (Yuda 1:4).

Kanisa la kweli la kikristo ni kanisa ambalo jambo la muhimu Zaidi ni kubadilika kwa ndani, bila kujali jina la kanisa. Badiliko hili si tu kuhusu kujaribu kuonekana mwema ili niwapendeze wengine Zaidi, bali ni badiliko ndani yangu ambalo linanifanya kuwa mtu mpya katika Kristo. Ninakuwa kama Kristo. (2 Wakorintho 5:17; Wagalatia 6:15; Warumi 8:29. Hakuna kitu kingine ambacho ni chema vya kutosha.

Tunapotafuta kanisa linalofaa tunapaswa kujiuliza: Je, ni nini ninachokitaka mimi mwenyewe kama mkristo na katika Maisha yangu ya Kikristo? Je, niko tayari kuacha Imani yangu ya kibinafsi ikiwa haipatani na neno la Mungu? Au Je, nitatosheka na kupata dhamiri nzuri, kusikia maneno ya kupendeza katika kanisa lisilo na Maisha katika mafundisho, au lile linalohibiri msamaha bila kuhubiri Maisha na utii wa neno la Mungu? (2 Timotheo 4:2-4)

Katika kanisa kama hili tunaweza kupata hisia nyingi nzuri, lakini hatuji katika Maisha mapya katika Kristo. Tunaweza tu kuwa watu wazuri lakini na asili yetu ya kibinadamu yenye dhambi ikiwa bado I hai. Tunapaswa kufanya Paulo alichowaambia Wakorintho kufanya: “Jijaribuni wenyewe kwamba mmekuwa katika Imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa mmekataliwa.” 2 Wakorintho 13:5.

Tunapaswa kuwa waaminifu kwetu wenyewe na kuhakikisha kwamba tunataka kile tu ambacho Yesu anataka kwa ajili yetu na si kitu kingine chochote, na kwamba tuko tayari kuacha kila kitu ili kupata Maisha katika Kristo (Mathayo 13:46) tunapaswa kuwa wakweli na waaminifu na tusiwe na maslahi au matumaini mengine ya upande mwingine. Kisha Yesu anaweza na atatuongoza katika sehemu ambayo ni bora kwetu. Tunaweza kuwa na uhakika na hili.

Tafuta Maisha ya Kristo

Zaidi ya yote, tunapotafuta kanisa linalofaa, tunapaswa kuwa na shauku ya kupata uzima wa Kristo, badala ya kutafuta tu kanisa ambalo linatupa hisia nzuri.

Mwinjilist mmoja mkuu alisafiri ulimwenguni kote na kusema alikuwa ameulizwa maswali ya kila aina: Je, unaamini katika utatu? Nini nafasi yako kuhusu nafasi ya mwanamke? Unabatiza vipi? Na maswali mengine yanayofanan. Haya yote yanaweza kuwa mwaswali mazuri sana, alisema, lakini katika safari zake nyingi, hakuna mtu aliyewahi kuuliza swali moja rahisi, muhimu. “Ni aina gani ya Maisha unayoongoza?”, Je, unakasirika? Uhusiano kati yako na mke wako ukoje? Je, umejaa furaha katika majaribu yako yote? Je, ni matokeo gani ya injili unayohubiri katika Maisha yako mwenyewe? 1 Timotheo 4:16?

Yohana aliandika kwamba uzima ndani ya Yesu ulikuwa nuru ya wanadamu (Yohana 1:4). Tunapoona Maisha – Maisha ya Kikristo - katika kanis, basi tunajua tumefika nyumbani. Maisha haya , nuru hii ndiyo huleta umoja.

Biblia haizungumzi kuhusu makanisa mengi tofauti na yanayoshindana, bali kuhusu “kanisa” (Waefeso 3:10 na mistari mingine) na tunabatizwa katika “Mwili mmoja” (Waefeso 4:4). Kwamba kulikuwa na migawanyiko katika kanisa la Korintho ilikuwa ishara kwamba tayari walikuwa wameshindwa, kama Paulo asemavyo, “Basi imekuwa pungufu kwenu kabisa kwamba mnashitakiana ninyi kwa ninyi. Maana si afadhali kudhulumiwa? Maana si afadhali kunyang’anywa mali zenu? 1 Wakorintho 6:7.

Ikiwa kuna umoja wa kweli war oho, umepata kanisa la kweli. Nawatakia kila la kheri wale wote wanaotafuta kwa dhati, kwani ukitafuta, utapata, kama ilivyoandikwa katika Mathayo 7:7!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya David Stahl awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.