Nawezaje kusaidia?

Nawezaje kusaidia?

Navyoweza kupata njia ya kufahamu wakati sahihi, maneno sahihi, na matendo sahihi hivyo ninaweza kuwasaidia na kuwabariki wengine.

18/2/20205 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Nawezaje kusaidia?

“Naye alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaomtii. Kisha ametajwa na Mungu kuwa kuhani mkuu kwa mfano wa Melkizedeki” Waebrania 5:9-10

Melkizedeki – ni mtu kwenye Biblia ambaye watu wanamfahamu kidogo sana. Alionekana ghafla na kumpatia chakula na divai Ibrahimu na baraka baada ya Ibrahimu kupigania kumweka huru mpwa wake Lutu katika jiji la Sodoma. Alikua “mfalme wa Salemu”, lakini hakuna aliyemfahamu mama yake wala baba yake. Alionekana kwa muda mfupi na akatoweka haraka, akatokomea kusikojulikana. (Mwanzo 14:18-20)

Japo kuna machache yanayojulikana kumhusu, historia yake ilinivutia. Alikuja kwa Abraham kwa wakati sahihi, aliongea maneno ambayo Abraham aliyahitaji, halafu akaondoka.

Nawezaje kuwa Melkizedeki?

Imenipa shauku ya kuwa wa baraka kama Melkizedeki ninapojishughulisha na wengine. Panaweza kuwa na mahitaji mengi ndani ya wale wanaonizunguka. Pengine mwingine anahitaji aina fulani ya neno, chakula kizuri, ama sikio Sikivu. Pengine mwingine ni mgonjwa, mpweke ama anahangaika kwa namna fulani. Endapo nitajifikiria mwenyewe, mahitaji na matakwa yangu mwenyewe, ni rahisi kukosa fursa ya kuwa mwenye baraka kwa wengine. Lakini kama kweli nataka kuwabariki wengine, na kuwa na shauku ya kumtumikia Mungu kwa kila ninachofanya, hivyo ninaweza kusikiliza sauti ya roho na kuamini kwamba anaweza kuniongoza kwenye mambo ambayo yanaweza kuwa msaada kwa wengine.

Lakini je, Najuaje nini cha kutoa? Nitajuaje nini cha kumweleza mtu ambaye anaweza kuwa na shida? Jibu ni kwamba kwanza ni kuwa na moyo safi – kufanya yale ambayo tayari nafahamu kuwa ni sahihi. Mungu alipomtaka Musa na Aroni kuongoza wana wa Israeli, alisema “Basi sasa, enenda, nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na kukufundisha utakalolinena” Kutoka 4:12. Tukiishi kwa kufuata yale tunayoona yapo sahihi, tunakua na ahadi hii pia. Mungu anapotaka tufanye jambo, hutupa pia kile tunachohitaji ili kuweza kuifanya jambo hilo. Tunatakiwa tuenende kwa Imani, tuzungumze ama tufanye kile ambacho Mungu anatuambia moyoni mwetu, na kumwachia matokeo Mungu.

Acha matokeo mikononi mwa Mungu.

Natambua mwenyewe, wakati mwingine kuacha mambo mikononi mwa Mungu ni vigumu sana. Tunapenda kuona matokeo ya kazi zetu. Je, nilisema kitu sahihi? Je, mtu huyu anashukuru kwa kile nilichotoa? Je, wengine wanajua kama mimi ni “Baraka” kiasi hiki?

Fikira zote hizi zinaweza kuja haraka sana. Lakini kama natafuta wengine wanishukuru, ama kunitukuza ama hata kuona kama nilichosema ama kutenda kilikua sahihi, hivyo nakua natafuta maslahi yangu mwenyewe. Hivyo sivyo ambavyo Mungu anataka anaponitumia kubariki mtu Fulani, na sivyo alivyofanya Melkizedeki alivyofanya. Aliondoka kimyakimya na kuacha kila kitu mikononi mwa Mungu.

Haijulikani kama alijua hata matokeo ya matendo yake. Ukweli ni kwamba, sadaka yake ya chakula na divai vilimpa Abraham nguvu na ujasiri baada ya vita. Lakini cha muhimi zaidi, maneno yake yenye kutia moyo yalimsababisha Abraham kusema HAPANA kwa mfalme wa Sodoma alipotaka kumpa Abraham utajiri wa kidunia. Hii ni muhimu sana, kwa sababu ilimaanisha kwamba Abraham hakuweka uaminifu wake kwenye vitu vya kidunia ama watu, bali kwa Mungu pekee. Kitendo hiki kilikuwa muhimu ndio maana Melkizedeki alijulikana pia kama “Mfalme wa haki” (Waebrania 7:1)

Kumekuwa na nyakati katika Maisha yangu ambapo nilihitaji kumsaidia mtu Fulani, lakini pia nilitambua kwamba sikua na nguvu za kutosha zilizobakia, na nilipaswa kuamua. Je, naendelea kujaribu kusaidia, nikijua kwamba nafanya hivyo kwa nguvu zangu mwenyewe? Ama niende na kumwacha mtu huyo mikononi mwa Mungu, nikijua kwamba ana mpango juu ya wale ninao wajali na hivyo ataendelea na kazi yake? Kwanza ndani ya moyo wa huyo jamaa, na pili labda kwa kupitia wengine ambao wanaweza kusikia sauti yake pia.

Mungu hutoa ukuaji

Hadithi ya Melkizedeki imekua msaada mkubwa kwangu katika nyakati zile. Mfano wake umenipa Imani dhabiti moyoni mwangu kwamba ninaposikiliza sauti ya roho, naweza kuamini ambacho hufanya kazi moyoni mwangu. Naweza kuamini kabisa kwamba Mungu huendelea kufanya kazi hata nisnapokuwa nimeondoka kimyakimya, na naweza kuyaacha matokeo mikononi mwake.

Nimekumbushwa fungu katika 1Wakorintho 3:7: “Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye” Haijalishi nionapo matokeo ya kazi zangu na sala sasa na hata milele, haijalishi. Kwa kuwa Mungu ndiye anapaswa kupokea sifa kwa ajili yake.

Naweza kuwa safi wakati wote ili niweze kusikia sauti ya Mungu moyoni mwangu, naweza kuwa mnyenyekevu hivyo nifanye kazi alizonipangia, na naweza kuwa mwenye haki hivyo ninaweza kuwa kama “upepo huvuma upendako, na sauti yake waisikia, lakini hujui unakotoka wala unakokwenda; kadhalika na hali yake kila mtu aliyezaliwa kwa roho.” Yohana 3:8. Hilo ndilo lengo maishani mwangu na najua kwamba nitakuwa na kila kitu ninachohitaji – kwangu mwenyewe na kwa wengine.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya Heather Crawford awali ilichapishwa katika https://activechristianity.org/ imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika katika tovuti hii.