Nilivyojifunza kuwa mtu halisi

Nilivyojifunza kuwa mtu halisi

Linda alipata uhuru wa kweli alipogundua kwamba kulikuwa na mmoja tu aliyepaswa kumpendeza.

7/2/20184 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Nilivyojifunza kuwa mtu halisi

Tangu zama za utoto, nilikuwa nikijifunza kwamba ilikuwa ni muhimu kuwafurahisha na kuwapendeza watu. Ilikuwa muhimu kuwa mwenye akili, kupata elimu nzuri, kuwa maarufu, kuvaa kwa mtindo, n.k. kama mtoto na mwenye umri wa chini ya miaka ishirini, mara nyingi nilijilinganisha na wengine, lakini kamwe sikujiona nikiwa vizuri kuliko mmoja kati yao. Rafiki zangu siku zote walionekana werevu, wenye mwonekano mzuri, na wazuri katika michezo.

Nilipoteza hali ya kujiamini na nikawa mkimya sana. Kwa kuwa nilikua mkimya, nilianza kupoteza mahusiano na wengine na mwishowe nilipoteza rafiki zangu. Sikuweza kusema nilichotaka kusema kwa sababu nilkuwa nikiogopa kwamba wengine wasingependa. Nilihisi kama nilikuwa nje. Nakumbuka nilikua mpweke na mwenye huzuni ndani yangu. Mimi halisi nilikuwa nimefungiwa kwenye sanduku, na nilitamani kuwa huru.

Sikutaka kusihi kama mtu mwenye mpweke na mwenye huzuni katika maisha yangu yaliyobakia na nilianza kutafuta kitu ambacho kingenifanya mwenye furaha na kuniletea amani. Sikuelewa hasa sababu ya tatizo langu kwamba niliishi maisha bila Mungu na kwama ilikuwa ni kupitia kwa Mungu pekee ndipo ningepata uhuru.

Kinachohitajika ni kile tu ambacho Mungu huwaza.

Nilipokuwa na miaka 20, nilikutana na mtu fulani aliyenambia, kwa mara ya kwanza maishani mwangu, kwamba ningemwomba Yesu moyoni mwangu na angekuwa rafiki yangu. Yesu alikuwa Bwana na mwokozi wangu; nilimkabidhi moyo wangu wote na maisha yangu mikononi mwake. SIkujihisi mpweke tena. Niliacha kujaribu kuyaongoza maisha yangu mwenyewe, kwa kuwa nilikuwa nimejifunza kwa maumivu kutoka kwenye maisha yangu ya nyuma yaliyopelekea kwenye kukata tamaa, huzuni, na hali ya kukosa furaha. Sasa nilimuhitaji Yesu ayaongoze maisha yangu na kunipeleka kwenye maamuzi. Nilihisi furaha na amani lakini bado nilikuwa nikiogopa juu ya mawazo ya watu juu yangu.

Mara nyingi, nilijikuta nikielezea nilichokuwa nikisema ama kufanya kuhakikisha wengine wanakubaliana na mimi. Kidogo kidogo roho mtakatifu wa Mungu alinionesha kupitia neno lake kwamba kuna mmoja to niliyepaswa kumfurahisha, na huyo ni Yesu. Alinipenda na alinifia ili niwe huru kutokana na mawazo ya watu juu yangu.

Nilifanya uamzi thabiti wa kuacha kujaribu kuwafuraisha watu, bali kumtukuza Yesu pekee. Neno la Mungu lililonisaidia wakati ule lilikuwa, “wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini viumbe vyote ni utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yote.” Webrania 4:13. Niligundua kwamba macho ya Mungu yananitazama, hivyo sipaswi tena kuogopa juu ya mawazo ya watu juu yangu. Kinachofaa ni kile ambacho Mungu huwaza.

Wakati mwingine watu wenye nguvu hunifanya nitake kujiondoa ndani yangu tena. Ndipo kifungu, “Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali nguvu ya upendo na ya moyo wa kiasi,” kilinisaidia dhidi ya hisia hizi za woga. (2Timotheo 1:7.) Kwa muda fulani, nilikuwa huru Zaidi na Zaidi kutoka kwenye mawazo ya watu. Badala ya “kufungwa” na wengine, kwa furaha nikawa “nimefungwa” kwa Yesu wangu Zaidi na Zaidi, na kwa kile ambacho Mungu ananiwazia. Nilijilinganisha mwenyewe na neno la Mungu linavyosema na kumruhusu anifundishe namna ya kuishi ili nimtukuze.

Kuwa huru

Nilianza kuwaza kwa namna tofauti kabisa. Nilielewa kwamba maisha si mimi pekee. Badala ya kufanya kile nilichotaka na kupenda, nilianza kuwasaidia na kuwajali wengine, wakati huohuo nikawa huru kutoka kwenye mawazo ya watu juu yangu zaidi na zaidi. Bwana mwema ulinifungulia fursa nyingi kwangu kuweza kufanya hivi.

Sasa ninapokuwa pamoja na marafiki na familia naweza kusema ninachotaka kusema. Sasa huwa nawasikiliza marafiki na familia kwa lengo la kuwa msaada kwao. Maisha yangu ni ya kitajiri na yenye kujaa. Unapokuwa huru kweli kutoka kwenye kujiwazia mwenyewe na juu ya namna wengine wanavyokutazama, unaweza kuwasaidia wengine kutafuta njia ya Mungu na kushuhudia uhuru ule ule.

Yesu amenipa akili timamu na naweza kujihisi mimi kama mimi na karama na utu ambao nimepewa. Woga haunitawali tena. Mungu ni msaidizi wangu na huwa namwomba msaada wakati wa shida. Mzigo mzito nilioubeba kwa miaka mingi umeondoka. Pumziko langu na amani imekua tele. Nimekuwa huru na mwepesi kila siku. Yesu ni mwokozi mkuu kwa kweli.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya Linda awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/  imepewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.