Kuwalaumu wengine ni kama hali ya asili ya upumuaji kwa watu wengi. Watafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba kila linalotokea, bado watu watawafikiria vyema.
Nimekaa kwenye dawati langu, nikifikiria kuhusu jambo fulani nililolisikia kwenye mkutano wa Kikristo wa krismasi wa hivi karibuni. Walizungumza kuhusu 1 Wakorintho 11:31 ambapo inasema, “Lakini kama tungejipambanua nafsi zetu , tusingehukumiwa.”
Katika hali yoyote, ni hali ya kawaida kuwahukumu ama kuwalaumu wengine. Hii ilianza mwanzoni na mwitikio wa Adamu Mungu alipomuuliza kile alichofanya. Hakumlaumu Hawa pekee kwa kumpatia tunda, alimlaumu Mungu moja kwa moja (“huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami….” Mwanzo 3:12).
Jina langu “zuri”
Nikitazama nyuma, naona aibu ninapofikiria muda wote niliokuwa nikifanya jambo lile lile, kujitetea kutoka kwenye lawama na kuzielekeza kwa wengine. Ni kama vile unakosa utawala dhidi yake. Maneno huonekana kama huja yenyewe: “Halikuwa kosa langu! Ni yeye aliyefanya hivyo…” kusema ukweli, nilikua kinyume na wazo hilo toka mwanzo…” n.k.
Kwa nini niko hivyo? Sijawahi kujaribiwa kusema kwamba sikuwa sehemu ya jambo lililogeuka na kuwa mafanikio. Kwa nini nasema kwamba sikuwa sehemu ya jambo ambalo halikwenda vyema? Kuna jibu moja. Kama mtu, nimezaliwa na asili ya dhambi ambayo ina majivuno ambayo haiwezi kukubali kwamba nilifanya jambo baya machoni pa watu wengine. Hivyo wakati wowote kama jina langu zuri lipo kwenye hatari, ninajaribiwa kudanganya, kuwashambulia na kuwalaumu wengine.
Kujihukumu mwenyewe na kukubali ukweli
Suluhisho ni lipi? Kujihukumu mwenyewe? Hiyo haionekani kama kitu chanya. Lakini ikiwa mimi ni mkarimu kwa mtu ambaye kamwe hawezi kukubali kwamba nimefanya jambo baya au nimefanya jambo jema, inaweza kuwa vigumu sana kwa wengine kuwa karibu yangu. Sitaki kuwa hivyo! Ikiwa nataka kubadilika kwa wema, ninapaswa kufanya jambo dhidi yake – haitatokea yenyewe.
Hivyi, ikiwa nitajihukumu mwenyewe na kuyakubali makosa yangu, Nini kitafuata? Ikiwa sitakubali nitakapojaribiwa kuwalaumu wengine, nitaanza kuona makosa na dhambi ndani yangu Zaidi. Machafuko yote ninayohisi katika hali zangu mara zote huja kutoka kwenye tamaa zangu za dhambi, kwa mfano, tamaa yangu ya kuwa kama, ya kufikiriwa sana, Fahari yangu. Haitokani na matendo ya wengine. Sipaswi kumlaumu mtu mwingine – kuna mengi katika asili yangu ambayo ninaweza kufanya kazi nayo!
Hii itanifanya niwe mkarimu Zaidi kwa watu wanaonizunguka, na juu ya hapo, Mungu anaona. Ninajua kwamba “atamlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake wale ambao kwa saburi katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutokuharibika watapewa uzima wa milele.” Warumi 2:6-7.