Siri rahisi ambayo humaliza msongo wa mawazo

Siri rahisi ambayo humaliza msongo wa mawazo

Wakati mwingine inaweza kuonekana kama kuna msukumo unakuja kutoka kwenye mwelekeo wote.

22/8/20213 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Siri rahisi ambayo humaliza msongo wa mawazo

Kuwa kijana leo kunaweza kuja na misukumo mingi. Kuna matarajio, msongo wa mawazo, na mahitaji ambayo huja kutoka katika mwelekeo wote.

Hali ya baadaye haina uhakika.  Mara nyingi huwa tunajipa msukumo mwingi dhidi yetu wenyewe kwa sababu ya matarajio ya kweli ama ya kufikirika kutoka katika jamii.

Matarajio dhidi ya uhalisia

Mwenyewe sikuwahi kuwa na furaha kwa kuwa wa “wastani”. Nilitaka kuwa bora kwa kila jambo, na nilipata ugumu kukubaliana na ukweli kwamba kulikuwa na mambo ambayo sikuwa vizuri kwake. Hii ilileta hali ya kukata tamaa, uchungu, na wivu pale nilipojilinganisha na wengine.

Mwishoni, nilitambua kwamba matarajio yangu makubwa yalikuwa yakinifanya mtumwa! Nilikua sina furaha kwa kile nilicokuwa nimepewa; hakikuwahi kuwa cha kutosha niliishia kuwa mwenye uchovu na msongo wa  mawazo.

“Sisi ni kazi bora ya Mungu”

Niligundua kwamba nilipokuwa nikijaribu kuwapendeza marafiki zangu, familia yangu na  mimi mwenyewe, nilikua nakosa kitu pekee ambacho ni cha muhimu. Na hivyo kuna mmoja tu natakiwa kumpendeza. Mmoja aliyeniumba – mwalimu na bwana wangu.

“Maana tu kazi ya mikono yake, tuliumbwa katika kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo”. Waefeso 2:10.

Mungu aliniumba kutokana na malengo yake kamili. Hiki ni kitu alifikiria na alipanga kwa umakini.

Alinichagua kabla ya ulimwengu kuumbwa, na alinipa utu wa kipekee, talanta na uwezo ambao alijua ingekuwa vyema.

Ninapokuwa huru kutoka kwenye magumu yangu mwenyewe, uduni, ubora, n.k – ndipo najifunza kutumia karama na uwezo wa ambao Mungu amenipa nimtumikie kwa namna alivyopanga kwa ajili yangu. Ndipo macho yangu yanafunguliwa kutumia fursa nilizopewa na kuishi mbele ya uso wa Mungu. Naweza kuishi kwa njia inayompendeza, na ninakuwa huru dhidi ya kujaribu kuwa “mkamilifu” kwa sababu zote za uongo.

 

Kutumia alichonipa Mungu

Ninapokuwa mwaminifu Zaidi kwa kile Mungu alichonipa, hivyo hakuna sababu ya kutokuwa na furaha au mwenye msongo wa mawazo kuhusiana na hali yangu ya baadaye  kwa kuwa najua ya kuwa Mungu ana malengo kamili kwa ajili yangu. Atanitunza! Naweza nisiwe “mkuu wa ulimwengu”ama kuwa kamili kwa kila kitu, lakini ninapofanya kila kazi kwa moyo wangu wote kama nafanya kwa ajili ya Bwana na si kwa ajili ya wanadamu ( Wakiolosai 3:23) ndipo itakapobarikiwa. Ndipo nitajifunza kufanya vyema na vyema.

Kwa hiyo sasa, ingawa asili yangu bado inataka kila kitu kiwe kamili, siishi tena kama vile ninaishi katika msukumo mkubwa. Siwezi kujiruhusu kutumia karama ambazo Mungu amenipa kuwaonesha watu weengine kwamba mimi ni bora kuliko wao kwa sababu nitajikuta nje ya mapenzi yake. Lakini naweza kufanya  alichonipa Mungu kwa urahisi na kwa uaminifu na kuwa katika pumziko ndani yangu!

Ninaweza kuwa kama udongo mkononi mwa mfinyanzi – Mungu anaweza kunitumia na ninaweza kunifanya mtu anayetaka niwe.

Ninapoishi hivi, hakuna “msukumo”naweza kutazama hali yangu ya baadaye kwa tumaini na ujasiri.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya Eunice Ng awali ilichapishwa katika https://activechristianity.org/ imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika katika tovuti hii.