Mfano wa Yusufu

Mfano wa Yusufu

Tunaweza kujifunza mengi kutokana na hadithi ya Yusufu.

11/10/20164 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Mfano wa Yusufu

7 dak

Tunasoma kuhusu Yusufu katika Biblia - alikuwa kijana wa pekee sana. Jibu la maombi ya mama yake. Mwana mpendwa wa baba yake. Mwotaji wa ndoto za kinabii. Alipoteza kila kitu ndugu zake walipomuuza kama mtumwa huko Misri, lakini akaishia kuwa wa pili kwa amri kwa mtawala wa Misri. Ni nini kilikuwa cha kipekee kwa kijana huyu?

Tunaweza kusoma hadithi katika Mwanzo. Hadithi jinsi Yusufu, mwana mpendwa zaidi wa baba yake, Yakobo, aliuzwa kuwa mtumwa na ndugu zake wenye wivu. Jinsi alivyonunuliwa huko Misri na Potifa, ofisa wa Farao (mtawala wa Misri). Potifa akampenda na kumfanya kuwa msimamizi wa nyumba yake na vyote alivyokuwa navyo.

Kisha mke wa Potifa akajaribu kumshawishi  afanye nae dhambi ya ngono. Yusufu alijikuta katika hali gani! Hakuna jambo jema lingetokana na jambo hili, bila kujalisha nini alifanya. Lakini alikuwa na mtazamo safi na mzuri wa akili. Kwake yeye hakuwaza kumkubali. “Nawezaje kufanya jambo baya namna hii? Ni dhambi dhidi ya Mungu,” alisema. Mwanzo 39:7-9. Haikujalisha matokeo ya kusema Hapana kwake yangeweza kuwa yapi. Hakuna kitu ambacho kingeweza kumfanya atende dhambi dhidi ya Mungu wake.

Uovu mkubwa wa dhambi

Je, una mtazamo gani unapojaribiwa? Je, labda unafikiria kuikubali dhambi? Je, unafikiri juu ya faida na hasara za kujitolea na una wasiwasi kuhusu matokeo? Au una hofu ya kimungu kama Yusufu aliyokuwa nayo? Je, ungekataa kumtenda Mungu wako dhambi, bila kujali matokeo ni yapi?

Tunapaswa kutambua jinsi dhambi ilivyo mbaya. Ikiwa kweli ulielewa jinsi Mungu anavyohisi kuhusu dhambi - ni kiasi gani Anachukia - basi huwezi hata kufikiria kutenda dhambi. Mungu ni mtakatifu kabisa, na anataka kila kitu katika uumbaji wake kiwe kitakatifu pia. Dhambi huharibu kila kitu. Kabla ya dhambi kuja ulimwenguni, kulikuwa na amani kati ya Mungu na watu. Lakini dhambi huwatenganisha watu na Mungu (Isaya 59:2). Mungu anawapenda watu aliowaumba na anataka kuwabariki, lakini hawezi kufanya hivyo dhambi inapoingia kati.

Ndiyo, Yeye ni Mungu mwenye upendo, na kuna msamaha wa dhambi, lakini fikiria jinsi furaha zaidi unavyoweza kumletea unapokuwa na mtazamo ule ule thabiti wa akili ambao Yusufu alikuwa nao: “Nifanyeje jambo baya namna hii?”

Kuchagua kutenda dhambi wakati unajua vyema si jambo dogo! Lazima uwe mtiifu kwa sauti hiyo ya ndani inayokuambia usifanye jambo fulani. Sauti hiyo inazungumza na moyo wako na inakuambia wakati jambo fulani lipo nje ya mapenzi ya Mungu. Linaweza kuwa jambo "kubwa", kama uzinzi kama Yusufu alivyojaribiwa, au jambo linaloonekana dogo na lisilo na madhara - kwa mfano, uwongo mdogo. Kwa Mungu, dhambi ni dhambi, na anachukia yote, kwa sababu ina maana kwamba umechagua kufanya mapenzi yako mwenyewe na kuishi kwa ajili yako mwenyewe na si kwa ajili yake.

Matokeo ya kuchagua kutotenda dhambi

Lakini wale wanaomcha Mungu na kuchagua kutotenda dhambi wataona kwamba ni thamani kabisa. Si rahisi kukataa kutenda dhambi. Inagharimu kitu. Lakini matokeo ni nini? "Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana." 2 Wakorintho 4:17.

Ingawa alitupwa gerezani, Yusufu alipata mamlaka zaidi na zaidi huko pia. Mungu alimpa kipawa cha kufasiri ndoto, na kwa sababu hiyo akawa msaada mkubwa kwa Farao. Akawa wa pili katika uongozi wa Misri yote! Na juu ya yote hayo, pia alimrudisha baba yake na familia. Hili halikutokea kwa bahati. Mungu huwatunza watu kama Yusufu - wale wanaomcha na hawakubali dhambi. Unaposema Hapana kwa kile ambacho unajua ni kibaya, na badala yake unachagua kumpendeza Mungu vizuri, basi Mungu pia atakubariki, kama alivyofanya kwa Yusufu (Wagalatia 6:9).

Yusufu alimcha Mungu na akachagua kutotenda dhambi

Maamuzi unayofanya yanaonyesha mtazamo wako wa akili ni upi. Amua leo kwamba hutafanya uovu na kumtenda Mungu wako dhambi! Unaweza kumwomba Mungu ili akufundishe kuchukia dhambi kama yeye anavyofanya. Kisha fanya ulichoamua. Mungu huwasaidia wale ambao mioyo yao ni amini kwake. Tunaweza kusoma hilo katika 2 Mambo ya Nyakati 16:9: “Kwa maana machi ya Bwana hukimbia – kimbia duniani kote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao waliokamilika moyo kueleka kwake”. Utajikuta unapata amani na furaha unapochagua kutenda mema (Warumi 2:6-7).

Yusufu alimcha Mungu na akachagua kuchukia dhambi. Hii ilimaanisha kwamba maisha yake yalibarikiwa na Mungu. Inaweza kuwa sawa kwako! Ni jambo ambalo unapaswa kuamua mwenyewe. Amua kufa kuliko kutenda dhambi, na itakufaa. Mungu atahakikisha hilo!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala haya yanatokana na makala ya Ann Steiner yaliyochapishwa awali kwenye https://activechristianity.org/ na yamebadilishwa kwa ruhusa ya matumizi kwenye tovuti hii.