Je, Yesu ni upendo wako wa kwanza?

Je, Yesu ni upendo wako wa kwanza?

Ni vyema kujitathimini wenyewe kuona kama Yesu bado ni upendo wa kwanza katika maisha yetu.

9/8/20184 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Je, Yesu ni upendo wako wa kwanza?

6 dak

“Umeacha upendo wako wa kwanza”

Yesu, kupitia kwa mtume Yohana, alimwandikia barua kiongozi wa kanisa la Efeso. Alimwambia: “Nayajua matendo yako, na taabu yako, na subira yako, na ya kuwa huwezi kuchukuliana na watu wabaya, tena umewajaribu wale wajiitao mitume, nao sio, ukawaona kuwa waongo; tena ulikuwa na subira na kuvumilia kwa ajili ya jina langu, wala hukuchoka. Lakini nina neno juu yako, ya kwamba umeuacha upendo wako wa kwanza.” Ufunuo wa Yohana 2:2-4.

Licha ya kufanya kazi nyingi nzuri, hazikutosha, kwa sababu aliuacha upendo wake aliokuwa nao mwanzoni. “Upendo wake wa kwanza” kama ilivyoandikwa katika tafsiri za biblia zingine – kwamba kumpenda Yesu kulizaliwa moyoni mwake mwanzoni alipoamini.

upendo wa kwanza ni nini?

Upendo wa kwanza inamanisha upendo ambao huja kabla ya wengine wote: Upendo mkuu.

Upendo mkuu kuliko upendo wetu kwa:

·         Sisi wenyewe

·         Familia zetu

·         Marafiki zetu

Hata kama tunawapenda na kuwasaidia na kutumia muda wetu kuwahudumia wengine, upendo wetu kwa Yesu huwepo kabla ya wowote kati ya huo, hivyo tunaweza penda familia zetu kwa uungu, siyo kwa upendo wa kibinadamu. Ndiyo maana Yesu alisema “yeyote akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.” Luka 14:26.

Kumpenda Yesu ni kuzishika amri zake. (Yohana 14:15) hivyo kama kitu chochote, tamaa zetu, au uhusiano wetu na watu wengine ukijaribu kuvunja amri yoyote – kama tuna upendo wa kwanza, tutamtanguliza Yesu na tutafanya mapenzi yake. Ndiyo maana Yesu alitumia neno kali kama kuchukia. Ni chuki dhidi ya kitu chochote ambacho kinaweza kusababisha tutende dhambi.

Tukiwa na upendo huu wa kwanza, hivyo tutafanya kila kitu kwa ajili ya Yesu. Hatufanyi mema na kuchagua vitu sahihi si kwa sababu tunahitajika tufanye, au tunafanya kupata heshima. Tunafanya kwa lengo moja pekee na hiyo sababu ni Yesu. Soma pia: Je, kweli Yesu ni mtawala wa moyo wako?

Upendo wa kwanza: Kufanya mambo kwa sababu sahihi.

Tunaweza kuwa na shauku na bidii kufanya kazi nzuri, hususani tunapofanya vitu ambavyo wengine wanaweza kuona, kwa sababu mbaya. Tunatakiwa tuendelee kujihukumu wenyewe na kuondoa tamaa za kupata heshima, tamaa yoyote ya kutaka kuwa na zuri mbele za watu. Ndipo tutabaki katika upendo wa kwanza.  (1Wakorintho 16:14)

Tunaweza fanya mambo kirahisi kwa kufuata marafiki na familia wanavyofikiria ama wanavyosema. Tuna hofu kwamba watawazaje kama tukifanya hiki ama kile, ama hoja zetu na maoni yetu ya kibinadamu yanatuweka mbali na amri za Kristo. Kubakia katika upendo wa kwanza inamanisha kwamba matendo yetu yamejikita katika neno la Mungu, na si kwa lolote lile.

Upendo wa kwanza wa kristo hutufanya tuhitaji kuwa kama yeye, hivyo tunajifunza kutenda kama ambavyo angependa. (Warumi 8:29). Ndipo tunapata upendo, furaha, uvumilivu, fadhili, wema, uaminifu, upole, kujidhibi. (Wagalatia 5:22-23) Ndipo matendo yetu ni baraka na mfano, na tunaweza kuwa na upendo wa Kimungu kwa watu. Tunapofikiria kuhusu Yesu kwanza, ndipo tunapokuwa na uhusiano mzuri kwa sababu kila tunachofanya kiko huru toka dhambini na ubinafsi. Tunahitajika kufikiria kwanza uhusiano wetu na baba na mwana, ndipo uhusiano wetu duniani ufuatie. Soma pia: ulifahamu kuwa maisha ya Yesu yanaweza kuwa maisha yako?

Barua kutoka kwa yesu

Yesu angesema nini angekuandikia barua? Je, Angeweza kuusifu upendo wako kwake ama ungeweza,au kama kiongozi wa kanisa la efeso ungehitaji kuambiwa “…….. Basi kumbuka ni wapi ulikoanguka, ukatubu, ukafanye matendo ya kwanza”?  Kuwa na huu upendo wa kwanza na kuwa na shauku kufanya mambo yote kwa ajili yake tunapompa kwanza moyo wetu ni jambo kuu. Lakini kubaki kwenye pendo hili katika hali zote za maisha, katika mapito yetu yote ya maisha, bila kukata tamaa na bila kutafuta manufaa yetu wenyewe, yenye huongoza katika uzima wa milele.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita katika makala ya Kathryn Albig awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ na imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika katika tovuti hii.