Waliwatoa dhabihu vijana na binti zao kwa sanamu

Waliwatoa dhabihu vijana na binti zao kwa sanamu

karibia wakristo wote hutafuta kilicho kikuu, na hutaka Watoto wao wawe wakuu ulimwenguni. Lakini hiki sicho Mungu anachotaka kwa ajili yetu!

22/8/20213 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Waliwatoa dhabihu vijana na binti zao kwa sanamu

“Naam, walaitoa wana wao na binti zao kuwa dhabihu kwa mashetani.” Zaburi 106:37. Hii imeandikwa kama onyo kwetu, ili tusifanye kama hivyo.

Sanamu inaitwa “Ukuu wa ulimwengu”

Kuna sanamu inaitwa: ukuu wa ulimwengu. Huyu ni muungu ambaye amekuwa akiabudiwa karibu na kila mtu, kwa watu wa dunia n ahata wa madhehebu, tajjiri na maskini. Karibia kila mkristo hutafuta yaliyo makuu katika ulimwengu, hata kwa ghalama za Imani ya ukristo wao. Na pale wanapokuwa wamejitoa kwa ajili ya sanamu hii, wazazi wao hawawapati kamwe.

Ibrahimu alimtoa mwanae kutokana na mapenzi ya Mungu, lakini leo watu wanawatoa Watoto wao kutokana na mapenzi yao wenyewe, kutokana na vile watu wanachoangalia na kupendezwa nacho. Wana wa Israeli waliwatoa dhabihu vijana na binti zao kwa sanamu (Zaburi 106:37), na ni jambo ambalo limekuwa likifanyika kwa enzi zote. Watu wanatamani kufanya kila jambo ili Watoto wao wawe wakuu ulimwenguni. Lakini Yesu alisema: “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu.”

Ukuu wa kumjua Yesu Kristo

Kuwa wakuu hutakiwa kuujaza ubongo wao kwa ujuzi wa ulimwengu, na kwa hali hii kila kitu kimetolewa  dhabihu kwa madhabahu ya sanamu. Paulo anasema “Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo. Naam, Zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo.” Wafilipi 3:7-8.

Hata katika makusanyiko mengi ya kidini, mmoja anaweza kuwa mchungaji baada ya kusoma kwa muda mrefu. Lakini kama tunamjua Mungu, tunazungumza maneno ya Mungu bila kuhitaji elimu ya kidunia. Hekima ya ulimwengu huu, kwa upande mwingine, huchelewa katika kujifunza kumjua Mungu kwa Imani.ujuzi wao wenyewe hushikamana nao, na mara kwa mara hulinganisha ujuzi wa ulimwengu (ambao ni udanganyifu mtupu) na hekima ya kimungu, ambayo itajidhihirisha kwa wakati wake kutawala watawala na wenye nguvu.

Acha tuwatoe dhabihu vijana na binti zetu kwa Bwana, kwani huu ndio uungu wa kweli. Acha tuwafundishe ambacho Mungu hukichukulia kama kikuu ili waweze kumtukuza yeye. Tuwatoe kwa ajili yake ambae ndiye kiongozi wa watawala na wenye nguvu, hivyo tutawapata milele.

Omba upate jicho ili uweze kuona

Mwombe Mungu akupe jicho la ndani ili uweze kuona, kwani kama ukiangalia kwenye karatasi yoyote ya dini (Haijalishi hasa ni ipi), utagundua kwamba wanapendezwa na ukuu wa ulimwengu, hata kama hawasemi kuwa ni sawa. Viongozi wa mikusanyiko ya kidini mara nyingi wana vutiwa na ukuu wa ulimwengu na watu wanataka iwe hivyo. Kwao Mungu aunganishwe na ulimwengu. Bila kujalisha namna gani watu wenye hofu ya Mungu walivyo na hali ya chini na maskini, hata kama ujuzi wa kimungu ni mkuu, bado wanaonekana kuwa chini ya wengine.

Lakini macho ya Mungu yanatosha kutumika kama “makuhani” mbele za Mungu. Ezekiaeli 44. Yamejazwa na hofu na upendo wa Mungu, huwapenda watu wake watakatifu. Hawajitoa dhabihu kwa mashetani, lakini wamekuwa wakitoa dhabihu kwa Mungu aliye hai kupitia Yesu Kristo Bwana wetu, na wataishi milele. Lakini wale ambao huabudu sanamu watapotea milele.

“Watoto wadogo, jilindeni  nafsi zenu na sanamu.” 1Yohana 5:21

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya Johan O Smith ambayo awali ilionekana kwenye kichwa cha Habari “De ofret sine sønner og døtre til maktene” (“Waliwatoa dhabihu vijana na binti zao kwa mashetani”) kwenye chapisho la mara kwa mara la BCC “Skjulte Skatter" (Hazina zilizofichika) agosti 1933. Imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika katika tovuti hii.