Yesu anataka kuwa Mchungaji wako Mwema

Yesu anataka kuwa Mchungaji wako Mwema

Je, unamruhusu Yesu kuwa Mchungaji wako au bado unajaribu kutawala maisha yako mwenyewe?

23/1/20174 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Yesu anataka kuwa Mchungaji wako Mwema

Yesu, Mchungaji Mwema

Yesu anasema katika Yohana 10:11, “Mimi ndimi mchungaji mwema.” Anataka kuwa mchungaji mwema kwa kila mtu, ndiyo maana alikufa kwa ajili ya dhambi za ulimwengu wote na si kwa ajili ya watu wachache tu. Lakini ukweli ni kwamba watu wengi hawataki kuwa na Yesu kama mchungaji wao, badala yake wanataka kuwa na udhibiti wa maisha yao wenyewe. 

Basi, Yesu ni mchungaji wa nani na kondoo wake ni akina nani?  ni wale watu wote waliokubali kuacha kila kitu ili kuwa wanafunzi wake. Tunaweza kusoma hili katika Luka 14:26-27, 33: “Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe na ndugu zake waume na wake; naam hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. Mtu yeyote asiyechukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu....... Basi kadhalika kila mmoja wenu asiyeacha  vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

Kila mtu ambaye yuko tayari kufanya hivi, anakuwa mfuasi au mwanafunzi wa Yesu. "Mwanafunzi hawi mkuu kuliko mwalimu wake, lakini kila mtu ambaye amehitimu hulingana na mwalimu wake.." Luka 6:40. Je, ni kweli kwamba ninaweza kuwa kama Yeye? Ndiyo, hivyo ndivyo mstari unavyosema.

Hili pia linathibitishwa katika Warumi 8:28-29: “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.” Fikiria kuwa na mchungaji, kiongozi, na mwalimu ambaye anaweza kutufundisha kutumia kila kitu maishani mwetu ili kifanye kazi kwa ukuaji wetu wa kiroho!

Yesu ni Mchungaji aliyebobea

Kazi ya mchungaji ni kuwalinda, kuwatunza, na kuwalisha kondoo, na Yesu ni mtaalamu wa kufanya hivyo. “Yesu anaelewa kila udhaifu wetu, Bali yeye  alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote bila kufanya dhambi!” Waebrania 4:15. Yesu, aliyeishi na kutembea katika dunia hii anajua hasa ni nini kibaya kwetu, na pia ni nini kinachofaa kwetu. Inasema hivi katika Zaburi 23:2 : “ katika malisho ya majani mabichi hunilaza; kando ya maji tulivu huniongoza.”

Yesu anatuongoza kwenye chakula cha kweli. “ ‘’ Yesu akawaambia, Chakula changu, ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka. nikamalize kazi yake.” Yohana 4:34. Pia tunapata chakula hicho cha kweli cha kiroho kwa kufanya mapenzi ya Mungu. Tunakuwa na nguvu zaidi katika roho zetu tunapotii na kufanya kile ambacho Yesu anazungumza na mioyo yetu. (Waebrania 5:9; Yakobo 1:25.)

Yeye pia hukutana na kiu yetu. “Hata Siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama akapaza sauti yake akisema, mtu akiona kiu na aje kwangu anywe. Aniaminiye mimi kama vile maandiko yalivyonena,mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. kama vile Maandiko yasemavyo.” Yohana 7:37-38.

Tunasoma katika Mathayo sura ya 4 kwamba Yesu alipojaribiwa na Shetani kule jangwani, sikuzote alitumia Neno la Mungu kumnyamazisha. Anatufundisha kufanya vivyo hivyo ili tujionee yale yaliyoandikwa katika Warumi 16:20 : “Na Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi.”

Katika njia ya kwenda Emau wanafunzi walipomsikiliza Yesu, mioyo yao iliwaka ndani mwao, na ni vivyo hivyo leo tunaposikia sauti ya Bwana na Mwokozi wetu aliyebarikiwa kupitia Neno Lake.

Jifunze kwa Yesu, Mchungaji wako

Wana-kondoo wanapokuwa wachanga, Mchungaji huwalinda na kuwatunza. Lakini wanapoanza kukua na kukomaa, ndipo anawafundisha kujilinda na kila aina ya uovu. Siku hizi, wengi wa wale wanaojiita Wakristo kwa kweli wanataka Yesu awafanyie kila kitu. Wana furaha sana kumwamini ilimradi tu wasichukue msalaba wao wenyewe na kumfuata.

Lakini Biblia inasema nini? “maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa. Nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia ; tupate kuishi kwa kiasi, na haki,na utauwa katika ulimwengu huu wa sasa..” Tito 2:11-12. Ndiyo, neema iliyo katika Kristo Yesu inatufundisha kupinga kila aina ya uovu, na sio tu kuupinga, bali kuushinda.

Yesu anamwalika kila mtu ambaye kweli anataka maisha haya ya kushinda dhambi yote aje kwake. Tunasoma hivi katika Mathayo 11:28-30: “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu. Mimi ni mpole na mnyenyekevu. Nanyi mtapata raha kwenu. Nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.”

Makala haya yanatokana na makala ya Bruce Thoma yaliyochapishwa awali kwenye https://activechristianity.org/ na yamebadilishwa kwa ruhusa ya matumizi kwenye tovuti hii.

Shiriki