Yesu: Mwenye nguvu ya kusaidia!

Yesu: Mwenye nguvu ya kusaidia!

Biblia Inazungumzia Kushinda Dhambi. Watu wengi huja kwa Yesu kwa ajili ya msamaha wa dhambi zao - lakini vipi kuhusu kushinda dhambi hizi?

17/2/20244 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Yesu: Mwenye nguvu ya kusaidia!

Yesu, mkuu na mwalimu mwema, daima yuko tayari kutusaidia. Watu wengi wanajua kwamba Yeye daima yuko tayari kutusamehe dhambi zetu, na kwamba tunaweza kuja kwake tunapokuwa wagonjwa au tuna shida zingine. Lakini msaada halisi ambao mkuu na mwalimu mwema anataka kutupa, ni msaada wa kushinda dhambi inayoishi ndani yetu - Huu ndio wokovu halisi aliokuja nao, lakini karibu hakuna mtu anayekuja Kwake kwa hili.

"Ni nani huyu atokaye Edomu, mwenye mavazi ya kutiwa damu kutoka Bosra? Huyu aliye na nguo za Fahari, anayekwenda katika ukuu wa uweza wake?"  Isaya 63:1.

Mwanafunzi  anataka kuwa kama bwana wake

Kulikuwa na wengi waliomfuata Yesu kwa sababu ya ishara na maajabu aliyofanya, lakini ni wachache tu ambao walikuwa wanafunzi wake waaminifu ambao walitaka kujifunza kuwa kama Bwana wao. Walikuwa tayari kuokolewa.

Yesu alizungumza na wanafunzi Wake kuhusu haki, na kama sisi kwa moyo wetu wote tunataka kukaa mbali na kila aina ya udhalimu—wadogo na wakubwa—tutapata uzoefu kwamba ana uwezo wa kutuokoa, kwamba Yeye ni mwenye nguvu kutusaidia.

"Heri walio maskini wa  roho; maana ufalme wa mbinguni ni wao." Mathayo 5:3. Kama sisi ni maskini wa roho, kama sisi tuna  njaa na kiu ya haki, na huzuni juu yetu wenyewe tunaweza kusaidiwa kuwa zaidi na zaidi kama Bwana wetu.

Je, unahuzunika kwa dhambi yako?

Watu wengi hawajisikii dhambi zao. Hawatajuta wanapotenda uovu kidogo au kutumia maneno yasiyo ya kweli. Ingawa imeandikwa kwamba kama wanafanya mambo kama hayo, dini yao haifai.. (Yakobo 1:26). Wanasema watasamehewa lakini hawatafuti msaada Kushinda Dhambi[GS1] [IH2] .

Ikiwa tunaona kwamba dhambi fulani bado ina nguvu juu yetu—kwa mfano hasira, uchungu, wasiwasi, kuvunjika moyo—basi inapaswa kuwa muhimu sana kwetu, suala la uzima na mauti, kushinda dhambi hizi. Tunapaswa pia kuhuzunika juu ya hilo kwamba sisi si kama Bwana wetu.

"Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa." Waebrania 2:18.

Si dhambi kujaribiwa; lakini tunapojaribiwa tunapaswa kumlilia Yesu ambaye ni mwenye uweza wa kutusaidia. Yeye mwenyewe alijaribiwa, lakini daima alitafuta msaada kutoka kwa Baba yake wa mbinguni na kamwe hakutenda dhambi katika majaribu, kama tunavyoweza kusoma katika Waebrania 4:15: "Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye aliyejaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi."

Kama angeingia katika majaribu hata mara moja, shetani angekuwa na sehemu ndani yake, na kifo kingekuwa na nguvu juu Yake, kama vile inavyofanya juu ya watu wengine wote.

Wokovu kwa wale wanaomtii  

Kulikuwa na kilio cha msaada katika moyo wa Yesu tunaposoma katika Waebrania 5: 7-9: "Yeye siku hizo za mwili wake, alimtolea yule awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua Pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu; na ingawa ni mwana, alijifunza kutii kwa mateso hayo yaliyompata; naye akipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokovu wa milele kwa watu wote wanaumtii.."

Vita hivi vya moyo wote, aliomba kwa kilio kikubwa na machozi, ilikuwa vita ya kutuokoa sote kutoka katika kifo cha milele na kuzimu. Ni ukuu na utukufu kiasi gani Bwana wetu wa mbinguni basi alikuwepo kwa ajili yetu! Yeye daima alikuwa ameshinda! Kifo hakiwezi kumzuia! Alishinda kwa kuwa mtiifu na mwaminifu alipojaribiwa, na sasa anaweza kuwaokoa wale wote wanaomtii. Lakini hawezi kutusaidia au kutuokoa ikiwa sisi ni waasi au wakaidi.

Bwana huyu mkuu na mwema anastahili upendo na utii wetu. Tusimwache Yeye amesimama peke yake na wokovu wote na msaada anaotaka kutupa.

Kuwa msaidizi

Pia tutakuwa wasaidizi wa kweli kwa kiwango ambacho tumekuwa tayari kusaidiwa. Kuna mahitaji makubwa kwa watu kama hao kila mahali. Hawana haja ya kufanya hivyo, lakini wanasaidia na kutoa! Wapo tayari kusaidiwa ili waweze tena kutoa msaada kwa wengine! Wao ni watu wenye manufaa zaidi duniani.


 [GS1]Unganisha na kifungu cha 36l - Inamaanisha nini kupata ushindi juu ya dhambi?

 [IH2]Unganisha kwenye makala:

https://activechristianity.africa/what-does-it-mean-to-get-victory-over-sin

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii inategemea makala ya Aksel J. Smith ambayo ilionekana kwanza chini ya kichwa "Mwalimu wa kusaidia" katika BCC ya "Skjulte Skatter" (Hidden Treasures) mnamo Desemba 1968. Imetafsiriwa kutoka kwa Norway na imebadilishwa na ruhusa ya matumizi kwenye tovuti hii.

© Hakimiliki Stiftelsen skjulte skjulte skatters forlag