Je, ulifahamu kwamba Maisha ya Yesu yanaweza kuwa Maisha yako?

Je, ulifahamu kwamba Maisha ya Yesu yanaweza kuwa Maisha yako?

Kuwa mtiifu katika maneno ya Mungu ambayo Yesu alisema kutatupeleka katika maisha kwenye wingi wake katika uzima wa milele. Imeandikwa na Ukristo hai.

30/7/20183 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Je, ulifahamu kwamba Maisha ya Yesu yanaweza kuwa Maisha yako?

5 dak

Kuwa mtiifu katika maneno ya Mungu ambayo Yesu alisema kutatupeleka katika maisha kwenye wingi wake katika uzima wa milele. Imeandikwa na Ukristo hai.

Yesu ni uzima

“Yesu akamwambia, mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa baba, ila kwa njia yangu.” Yohana 14:6

“Hapo mwanzo kulikuwapo neno. Naye neno alikuwapo kwa Mungu, naye neno alikuwa Mungu…. ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao uzima ulikuwa nuru ya watu…. Naye neno alifanyika mwili, akakaa kwetu…” Yohana 1:1, 4, 14.

“Roho ndiyo itoayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.” Yohana 6:63

“Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.” Yohana 6:68

Zishike amri zake

Kama tunataka uzima uliokuwa ndani ya Yesu uwe uzima wetu, tunahitajika kuyatii maneno ya uzima. Tunahitajika kuzishika amri zake. “Mkinipenda, mtazishika amri zangu.” Yohana 14:15. Yesu alichotaka ni kwamba maisha aliyoishi yanahitajika yawe maisha yetu pia. Tunahitajika kukata tamaa zetu za dhambi kila siku na kumfuata. (Luka 9:23) hicho ndicho kitatupeleka katika uzima wa milele.

“Maana wale alioowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.” Warumi 8:29. Hii inamaanisha kwamba wanahitajika wawepo watu wengi wanaozishika amri zake na kwa njia hiyo wawe kama yeye. Ni chaguo ambalo tunafanya. Kuchagua kutenda mema huleta uzima na baraka! (Kumbukumbu la torati 30:15,19) Lakini kufanya hivi tunapaswa kujua neno la Mungu. “…Ufanye bidi katika kusoma…. uyatafakari hayo; ukae katika hayo, ili kuendea kwako kuwe dhamiri kwa watu wote…” 1Timotheo 4:13,15.

Uzima wa Yesu ndani yetu

“Basi nasema, enendeni kwa roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili…Tukiishi kwa roho, na tuenende kwa roho.” Wagalatia 5:16, 25. Hapa tunaweza kuiona njia ya uzima. Tunapozishika amri zake, hatuwezi kuvutwa na tamaa za miili yetu yenye dhambi, na, kwa njia hiyo tutazishinda. Tunapaswa  “Kupiga vita vile vizuri vya Imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, na ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.” 1 Timotheo 6:12. Kupiga vita hivi vizuri Mungu ametupatia roho mtakatifu kutuonesha dhambi ambazo tunapaswa kuzishinda na kutupa nguvu ya kuzishinda. Hivyo naisha ya Yesu yataonekana ndani yetu. (2Walorintho 4:10). Tunakuwa mabalozi katika Maisha yake; tunaishi maisha ambayo yanampa sifa, na tutatakasika na kuwa kama yeye! (1Yohana 3:1-3)

Tumsifu Yesu aliyekuja chini duniani kutuonesha njia ya kuishi, hivyo tukaweza kupata uzima katika nyanja zote, uzima wa milele. (Yohana 10:10) Kuishi hivi hutupa uzima ambao ni zaidi ya chochote ambacho tungeweza kushuhudia hapa duniani. Tayari tumeanza kuonja na kushuhudia uzima wa milele wakati tukiwa bado hapa – matunda ya roho yenye baraka.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii awali ilichapishwa katika  https://activechristianity.org/ imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika katika tovuti hii.