Biblia ina maana gani hasa inaposema “kuamini”?

Biblia ina maana gani hasa inaposema “kuamini”?

Kuamini ni zaidi ya kukubali tu kwamba Biblia ni ya kweli.

30/1/20243 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Biblia ina maana gani hasa inaposema “kuamini”?

4 dak

Kuamini ni zaidi ya kujua tu kwamba Biblia ni ya kweli na kukubali kwamba imeongozwa na roho ya Mungu. Kuamini ni sawa na kuwa na imani kwamba Mungu yupo, yu hai, anatenda, na anapendezwa nawe sana leo. “Lakini pasipo Imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamin kwamba yeye yuko…” Waebrania 11:6. Hapa imeandikwa kwamba Mungu yupo, si kwamba Mungu alikuwepo!

Kuamini sio batili

Unapoiamini Biblia kiukweli, utaanza kufanya jambo fulani! Imani si hisia batili. Ukisoma Waebrania, sura ya 11, utaona jinsi mashujaa wa imani katika Agano la Kale walivyoshinda magumu mengi makubwa kupitia imani yao. Walimtumikia Mungu aliye hai ambaye aliwasaidia kwa namna ya ajabu.

Imani katika Mungu inanisukuma kufanya jambo fulani, kama ilivyoandikwa katika sehemu ya mwisho ya Waebrania 11:6 : “… Huwapa thawabu wale wamtafutao kwa bidii.” Mashujaa wa imani walimtafuta Mungu kwa bidii na walikuwa na bidii sana katika imani yao: "Kwa Imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika Habari ya mambo yasiyoonekana bado kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunde Safina, apate kuokoa nyumba yake." Waebrania 11:7. Leo, sisi pia tunapaswa kumtafuta Mungu kwa bidii kwa kusoma, kutii Neno lake na kuamini kwamba atatupa thawabu.

Je, Mungu huwalipaje wale wanaomtafuta kwa bidii? Kuna mifano mingi katika Biblia. Kwa mfano, soma 2 Petro 1:4 na utaona kwamba Mungu “… Ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa wshirika wa tabia ya uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.”

Ahadi ya thamani

Kushiriki asili ya kimungu ya Yesu ndiyo thawabu kuu iliyopo na si jambo ambalo ni gumu kuelewa. Asili ya kimungu ni tu tunda la Roho: upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, na kiasi ambalo limeelezwa katika Wagalatia 5:22-23. Njia nyingine ya kuelezea asili ya kimungu ni "maisha ya Yesu", ambayo wengine wanaweza kuyaona ndani yetu. ( 2 Wakorintho 4:11 )

Kwa mara nyingine tena, tunapaswa kumtafuta kwa bidii na kuwa watiifu ikiwa tunataka kushiriki katika tunda la Roho. Ni lazima "tuepuke uharibifu wa ulimwengu unaosababishwa na tamaa za kibinadamu". 2 Petro 1:4. Ni lazima “Siku zote twachukua katika mwili kuuawa kwake Yesu…” 2 Wakorintho 4:10. Kuepuka uharibifu wa ulimwengu huu, ambao unajumuisha dhambi ndani yetu, na kujazwa na tunda la Roho - ndivyo Agano Jipya lote linavyohusu.

Kwa Kupitia imani yao hai, mashujaa wa Agano la Kale walipata uzoefu wa uwezo mkuu wa Mungu kuwaangamiza adui zao. Katika Agano Jipya, Mungu amefanya jambo la utukufu zaidi: Ndani ya mwili wa Yesu, Aliharibu dhambi ambayo inapatikana katika asili ya mwanadamu. (Warumi 8:3.) Mungu hakumlazimisha Yesu kujitoa Mwenyewe; lakini Yesu mwenyewe alimwamini na kumtii Mungu katika hali zake zote za maisha.

Yesu ameshinda, na amefanya iwezekane kwa wewe na mimi kushinda pia. ( Ufunuo 3:21 ) Anaweza kutuokoa kabisa!

Yesu akamwambia, Ukiweza! yote yanawezekana kwake aaminiye.” Marko 9:23.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala haya yanatokana na makala ya Doug Lowery yaliyochapishwa awali kwenye https://activechristianity.org/ na yamebadilishwa kwa ruhusa ya matumizi kwenye tovuti hii.