Je, inagharamu nini kuwa mwanafunzi wa Yesu?

Je, inagharamu nini kuwa mwanafunzi wa Yesu?

Kuna watu wengi wanaokuja kwa Yesu. Lakini si wengi wao wanakuwa wanafunzi.

18/10/20164 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Je, inagharamu nini kuwa mwanafunzi wa Yesu?

6 dak

Lengo la mwanafunzi

Je, ina gharimu nini kuwa mwanafunzi?

Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.” Luka 14:26.

Inawezekana kuja kwake bila kuwa mwanafunzi wake. Inawezekana kusamehewa dhambi zako bila kuachana na dhambi, na ndivyo ilivyo kwa Wakristo wengi. Lakini Yesu hakuwahi kutenda dhambi.

Kwa upande mwingine, ni rahisi kuona jinsi watu wa kidini wanavyotenda dhambi kwani wengi wao husema uwongo, hawalipi madeni yao, wana kiburi, wanasengenya jirani zao, wanashuku nk. Hakuna hata mmoja wa Wakristo hawa anayeweza kusema kama Paulo, “Mnifuate mimi kama mimi ninavyomfuata Kristo’’ 1 Wakorintho 11:1.

Lengo la wanafunzi ni kumfuata Bwana wao na kuwa kama Yeye. Wanafunzi husikiliza kwa makini kile Roho anachowaambia kufanya na kuchukia ushauri wote wenye nia njema lakini wa kibinadamu kutoka kwa baba, mama, kaka, dada, mke, na watoto. Wanachukia hata maisha yao wenyewe, mapenzi yao wenyewe ya dhambi na asili, na kwa hiyo wanajihukumu wenyewe mara kwa mara - wanaona mambo ya dhambi wanayojaribiwa, na kutoyakubali. Kwa njia hii, wanashinda dhambi na Shetani. Wana furaha ya kujiweka safi na uovu daima.

"Na yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata, hawezi kuwa mwanafunzi wangu." Luka 14:27.

Ipo katika asili yetu ya kibinadamu kwamba hatutaki kuteseka - tungependelea dhambi kuliko kuteseka. Kwa mfano, ikiwa mtu amefanya kitu kibaya, jambo rahisi zaidi ni kusema uongo "mdogo". Lakini sisi tunaotaka kumfuata Yesu tunaamini kwamba tunapaswa kusema ukweli daima, kwa sababu uongo ni dhambi. Ikiwa tutachagua kutii kile tunachoamini na kusema Hapana kwa jaribu la kusema uongo, basi "tutachukua msalaba wetu" na kuwa wanafunzi wa Yesu. Hivi ndivyo tunavyofanya na dhambi zote, na bila mtazamo huu mkali hatuwezi kushinda dhambi na kuwa wanafunzi wa Yesu.

Soma pia: Yesu ni nani kwako? na Je, Yesu ndiye upendo wako wa kwanza?



Amua kama unataka kulipa gharama ya kuwa mwanafunzi

Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, wakisema, mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.’” Luka 14:28-30.

Hiki ndicho kinachotokea kwa maelfu ya Wakristo. Wanataka kuwa wakristo, lakini hawataki kuacha dhambi. Huenda mtu fulani ameanza kwa kusema kwamba amemkubali Kristo moyoni mwake na anapenda kwenda kwenye mikutano ya uamsho wa Kikristo, lakini inapofikia maisha yake ya kila siku, watu wa mahali pake pa kazi wanaona kwamba bado anadanganya, anasengenya, anaiba n.k. wanaambiana, “Anapaswa kuwa Mkristo,” na wanamdhihaki na hawana heshima kwake.

Mtu huyo hakufikiria juu ya gharama ambayo kwa kweli ingegharimu kuwa mwanafunzi na, bila shaka, hakuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo.

Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini? Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, na mtu yuke akali mbali.’’ Luka 14:31-32.

Ukristo ni kama vita. Unapaswa kukaa chini na kuamua ikiwa "watu elfu kumi" wanaweza kumshinda mfalme anayekuja dhidi yako na "watu elfu ishirini". Ukiona huna uwezo wa kushinda, basi unawatuma baadhi ya watu kwa adui kuomba amani. Lakini aina hiyo ya amani ni amani ya kutisha. Yesu hakuja kuwapa aina hii ya amani wanafunzi wake; badala yake, Aliamua kulipa gharama. Kisha akapigana na kushinda dhambi, Shetani, na pepo wachafu na nguvu zote.

Vivyo hivyo, sisi pia tunapaswa kuamua ikiwa tuko tayari kulipa gharama ya kuwa mwanafunzi wa Yesu. Na tusipoacha vyote tulivyo navyo, hatuwezi kuwa wanafunzi wake. Katika Waebrania 10:34 (NLT) imeandikwa, “… Mkijua kwamba nafsini mwenu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo.”

Tunaweza "kuja" kwa Yesu ili kuondoa mzigo wa dhambi, na kwa kweli hujisikia vizuri wakati mzigo huu unaondolewa. Lakini ili kuwa mwanafunzi, mengi zaidi yanahitajiwa. Kisha tunapaswa kuacha yote tuliyo nayo. Hiyo haimaanishi kwamba tunapaswa kutoa kila kitu tulicho nacho, lakini inamaanisha kwamba tuwe tayari kufanya lolote ambalo Roho anatuomba tufanye kwa vitu tulivyo navyo.

Wakati tumefikiria juu ya gharama na kuamua kwamba inawezekana kufanya chochote ambacho Yesu anatuomba, basi sisi ni wanafunzi wa Yesu Kristo kweli.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala haya yanatokana na makala ya Johan Oscar Smith ambayo yalionekana kwa mara ya kwanza chini ya kichwa “Wanafunzi” katika jarida la BCC la “Skjulte Skatter” (Hazina Zilizofichwa) mnamo Februari 1942. Imetafsiriwa kutoka kwa Kinorwe na imechukuliwa kwa ruhusa ya tumia kwenye tovuti hii.© Hakimiliki ya Stiftelsen Skjulte Skatters Forlag