Hakuna anayepaswa kutenda dhambi

Hakuna anayepaswa kutenda dhambi

Jaribu ni mtihani wa imani yangu.Maisha haya ni ya kufurahisha sana.

14/4/20123 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Hakuna anayepaswa kutenda dhambi

5 dak

Jaribu ni mtihani wa imani yangu.Maisha haya ni ya kufurahisha sana.

 

Imeandikwa na UkristoHai.

 

“Ndugu zangu , hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi timilifu, mpate kuwa wakamilifu bila kupungukiwa na neno” Yakobo 1:2-4

 

Jaribu sio dhambi .Ni mtihani wa imani yangu — mtihani wa kuona ikiwa ninaishi mbele ya watu au mbele za Mungu — mtihani ikiwa namuogopa Mungu au la. “Tukisema kwamba hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, wala kweli haumo mwetu” 1 Yohana 1:8. Kuwa na dhambi inamaanisha tuna tamaa za dhambi. Lakini ninapokuwa mwaminifu ninapojaribiwa, ninaweza kumwangamiza shetani ambaye ana nguvu za mauti. Hivyo, ninaweza kufurahi ninapoingia kwenye jaribu.

Ninapojaribiwa

“Heri astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidi wampendao. Mtu ajaribiwapo, asiseme, ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa. Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi, na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti .” Yakobo 1: 12-15

Hupaswi kukubaliana na majaribu kwenye mitihani yako, lazima uue vitu ambavyo unajaribiwa. Ukimtuhumu ndugu yako, ina athari kwa roho yako. Basi huwezi kuwa hai kwa Mungu. Unapokuwa hai kwa Mungu, unampenda ndugu yako huwezi kumtuhumu!

 

Kila mtu anayekubali mawaidha katika Biblia yu hai kwa Mungu. Haijalishi anavyoudhi mtu, hawezi kulazimisha dhambi kama hasira, kukosa subira, kukereka, n.k., kwa mtu mwingine.Kwa maneno mengine, sio kosa la mtu mwingine kamwe. Dhambi katika mwili wako mwenyewe, katika asili yako ya dhambi, imeamshwa na mambo yanayotokea. Ikiwa utaanza kulaumu watu wengine katika mawazo yako, umeanguka katika dhambi na hukuwa mwaminifu katika jaribu.

Sipaswi kutenda dhambi!

Ingawa nina dhambi, sipaswi kuanguka dhambini. Jaribu ni mtihani wa imani yangu. Haya ni maisha ya kufurahisha sana. Ingawa nina dhambi katika mwili wangu, katika asili yangu ya dhambi, sipaswi kutenda dhambi!

“Basi kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo  alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu ya mauti, yaani ibilisi.” Waebrania 2:14.Kifo ni sikitiko kubwa kwa watu wengi kwa sababu inakomesha mipango yao yote ya kibinadamu. Tunaweza pata uzima wa milele kwa kutokubali majaribu.Yesu alikuja kuwakomboa wale wote ambao walikuwa watumwa wa dhambi maisha yao yote kwa sababu waliogopa kifo

Yesu - Kuhani wetu Mkuu

“Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. Hivyo ilimpaswa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.” Waebrania 2:16-18. Alipaswa kufanana na nduguze! Je, hiyo si rahisi? Tunapoteseka katika mwili, tunapoteseka kwa kutokubali kutenda dhambi, basi sisi pia huacha kutenda dhambi. Roho wa Yesu haikuharibiwa kamwe na dhambi iliyo katika mwili wake. Ni Kuhani Mkuu kushangaza kama nini!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii inategemea makala ya Kare J. Smith iliyochapishwa hapo awali kwenye https://activechristianity.org/ na imebadilishwa na kupewa ruhusa ya matumizi kwenye tovuti hii.