Ama - au
Pengine unaishi kutokana na asili ya mwili wako, ambayo katika tafsiri tofauti za Bibilia hujulikana kama mtu mwenye dhambi au mwili, au huishi kutokana na roho. “Kwa wale waufatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifatao roho huyafikiri mambo ya roho. Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani.” Warumi 8:5-6. Unaweza kuishi kutokana na asili yako ya dhambi (Warumi 7:5), au uwe katika roho (Warumi 8:9). ni juu yako. Je unaishi kutokana na tamaa za mwili wako wa asili au unaishi katika roho mtakatifu?
“Basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili,” Romans 8:12. ukiishi katika roho, mwili wako wa asili na tamaa zake za dhambi unakua dhaifu; “unasulubiwa” (Wagalatia 2:20). Lakini ukiishi kwa kufuata mwili wako wa asili na tamaa za dhambi, unaivunja dhamira yako na huwezi kumsikia azungumzae kutoka mbinguni. Unasikiliza nini? Tamaa na hamu katika mwili wako wa asili? au katika dhamira yako na kwake ambaye huzungumza toka mbinguni?
Hakuna awezaye kuwatumikia mabwana wawili.
Ni mmoja ama mwingine. “Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Huwezi kumtumikia Mungu na mali.” Mathayo 6:24. Bwana wako ni yupi? Kristo ama shetani? Ni yupi unampenda zaidi? Ni yupi unayemfuata? Majibu yako katika maswali haya muhimu yataamua jinsi gani maisha yako ya milele yatakavyokua. Kuwa mkweli kwako mwenyewe.
Ikiwa mpaka sasa umekua ukiishi kutokana na mwili wako wenye asili ya dhambi, na umekuwa ukitenda kutokana na mapenzi na mawazo ya mwili wako wenye asili ya dhambi, hivyo basi tubu. Sitisha mahitaji yote ya mwili wako wenye asili ya dhambi. Fungua moyo wako na masikio yako kwa ajili ya wito wa Mungu na sauti yake. Kila mmoja lazima amtumikie Bwana – pengine dhambi na udhalimu ambavyo matokeo yake ni mauti, au haki ambayo matokeo yake ni maisha na amani. Hakuna njia ya katikati. Pengine sheria ya mauti au sheria ya neema na haki. (Warumi 5:17). Pengine ujiweke wazi katika haki au ujiweke wazi katika kutokuamini.
Utamtumikia nani?
“Lakini sasa mkiisha kuwekwa huru, na kuwa mbali na dhambi, na kufanywa watumwa wa Mungu, mnayo faida yenu, ndiyo kutakaswa, na mwisho wake ni uzima wa milele.” Warumi 6:22.
Kila mmoja wetu anatakiwa kuamua mwenyewe ni nani atakayemtumikia. Hii hutegemea na nini tunachohitaji. Wote tuna nguvu ya kuchagua. Hakuna awezae sema kwamba hawezi mtumikia Bwana ikiwa anataka kufanya hivyo. Mungu hujibu haraka sana wakati mtu anapochagua kumtumikia. Atamsaidia mtu huyo kuweka kila sehemu ya maisha yake katika mpangilio. Kama asingefanya hivyo hakuna mtu ambaye angeweza kumtumikia. Hata hivyo imeandikwa “Na yeye atakaye na ayatwae maji ya uzima bure” Ufunuo wa yohana 22:17.