Je, kristo ni mtawala wa moyo wako?

Je, kristo ni mtawala wa moyo wako?

Unadhani ni aina gani ya maisha mtu ataishi kama yesu ni Bwana na mwalimu wa kweli wakati wote?

14/12/20164 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Je, kristo ni mtawala wa moyo wako?

6 dak

Fikiria itakuaje kama Yesu kristo, Mwana wa Mungu atakaa na kutawala ndani ya moyo wako. Unadhani aina gani ya maisha mtu ataishi kama yesu ndiye Bwana na kiongozi wake wakati wote?

Wangapi wanaweza kusema ni kweli kristo ni Bwana katika mioyo yao? Bwana inaamisha mtu anayetawala ambaye ni bosi. Ni katika mioyo ya wangapi ambayo hutawala? Yesu mwenyewe anasema “Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo?” Uzima hutoka moyoni. Kristo ni uzima, mwanga wa wanadamu. Tu wakristo wa kweli ikiwa Yesu ndiye mtawala pekee ndani ya mioyo yetu. Huo ni ukristo. Kuna vitu vingi sana vinavyoitwa ukristo, lakini watu wachache tu ndiyo wakristo wa kweli. Kwa wengi wanaojiita wakristo, siyo sahihi kusema kwamba kristo anakaa katika enzi za mioyo yao.

Acha kutenda dhambi!

Mtu hapaswi kuomba msamaha kama kristo alikua Bwana pekee moyoni mwake. Fikiria hili kwa makini! Kama ndiye mtawala pekee ndani ya mioyo yetu usiku na mchana, tunaomba msamaha kwa lipi?  Kama kila kitu kilienda kama Yesu alivyotuonesha na tulifanya mapenzi yake siku nzima tuombe msamaha kwa lipi tena? Watu humwita “Bwana, Bwana” Lakini hawafanyi mapenzi yake. Huenenda na njia zao bila kumheshimu. Humtafuta kristo, si kwa sababu wanataka kumfanya mtawala wa mioyo yao.

Watu wengi wanahitaji kutatuliwa shida zao – wanahitaji msamaha wa dhambi zao – lakini kina nani wanamhitaji kama Bwana, ambaye atayaongoza na kuendesha maisha yako yote? Ni uongo kumwita Bwana kama hautaki kuwa naye kama Bwana wako. Basi acha kumwita Bwana. Lakini kama unataka akuongoze, acha kutenda dhambi. Je utapoteza nini kama ukichagua kuwa naye kama Bwana wako? Tutapoteza kila kitu ambacho ni kiovu!  Tunaweza poteza kila kitu ambacho hakina thamani! Tutafaidika na nini? Tutapata hekima na upendo wa Mungu na Kristo. Na tukimpenda Mungu tutaheshimu maneno yake. 1Yohana 2:5

Tunatenda dhambi kama hatuheshimu neno lake, sheria, lakini tunaweza samehewa ikiwa tutajutia na kutubu. Hoja zetu za asili na ujanja hutusababisha kutenda dhambi. Lakini kuwa na Kristo kama Bwana wetu ni mbingu duniani.  Fikiria ni salama kiasi gani ikiwa yeye ambaye ni hekima, atuongoze katika kila tunachofanya na ikiwa Kristo, anayetupenda kwa pendo timilifu huketi katika enzi ya moyo wangu.

Nguvu ya kuwa na Kristo kama Bwana na mwalimu

Mambo yote ni mema upendo unapotawala! 1Wakorintho 13:7. Hivyo Yesu Kristo, mwana wa Mungu, hukaa na kutawala kwa uhuru katika enzi za mioyo yetu kama nguvu ya ndani. Wengi wanae kama “mgeni” na pale baba na mwana wanapotembelea mioyo yao mara moja baada ya muda mrefu huonja utamu wake kwa kiasi kidogo.  Hii ni kuhusu wengi wanaojiita wakristo. Hivi ndivyo ilivyo kiuhalisia!

Lakini yesu anapokua Bwana na mwalimu moyoni mwetu, huishi humo. Hukaa humo milele na si mara moja moja. Upendo umekuja moyoni mwetu na kamwe hauwezi kuondoka.  Hutuongoza sisi katika kila jambo! Unaweza kuuonja ikiwa upendo huwepo mara moja baada ya muda, lakini kama upendo ni bwana, kiongozi wa milele moyoni mwako, utakuwepo siku zote. Hivyo utakua mtu ambaye anaishi katika upendo. Kama sheria, upendo huwatembelea tu watu wakati fulani; hivyo huwa unaongezeka na kupungua kwa wale wamtafutao Mungu na kuwa naye kama mgeni mioyoni mwao. Mara moja baada ya muda huuona uzuri wa Mungu, lakini aondokapo hubaki na mashaka kwani hakuna wa kuwaongoza.

Tukimpenda Kristo kama nguvu ya ndani mioyoni mwetu tunapata kila kitu kilichoandikwa katika kitabu cha 1Wakorintho 13. Kristo hutawala katika njia ambayo mara zote tunakua wenye kuridhika. Lakini watu wengi wanaojiita wakristo hupenda kuenenda na njia zao, hivyo shetani ndiye hutawala mioyo yao. Lakini huwa vizuri sana na hali ya kimbingu ndani yetu na kutuzunguka Kristo anapokua Bwana na mwalimu wetu.

Amini katika neno la Mungu! Kristo anapaswa kuwa na nguvu yote mioyoni mwetu. Hakuna kibaya kitakachotokea Kristo akiwa mtawala, kwa sababu anataka upendo na wema. Yeye aliye mtawala imara atafanya kila kitu kuwa imara.

Kristo ni mtawala madhubuti, lakini hufikiria mema juu yangu! Mfanye awe mtawala wako! Upendo haufikirii juu yake wenyewe; hufikiria yaliyo mema kwa wengine. Kwa hiyo, nawashauri mchagueni Kristo awe Bwana na mtawala mioyoni mwenu!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita katika makala ya Elias Aslaksen awali ilichapishwa katika https://activechristianity.org/ Na imepatiwa ruhusa kutumika katika tovuti hii.