Kwa nini ni muhimu kuwa mwadilifu katika maswala ya pesa?

Kwa nini ni muhimu kuwa mwadilifu katika maswala ya pesa?

Biblia inasema nini kuhusu pesa?

10/3/20175 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Kwa nini ni muhimu kuwa mwadilifu katika maswala ya pesa?

Pesa ina nguvu kubwa sana ulimwenguni, tupende au tusipende. Kuipata. Kununua. Kuuza. huwezi kuiepuka. Pesa ni kitu chenye nguvu. Wakati unayo au wakati hauna inaweza kujaza mawazo yako yote. Kwa hivyo mtumishi wa Mungu, mkristo wa kweli, anawezaje kuwa mwadilifu kuhusiana na maswala ya pesa?

 Biblia inaweka wazi kabisa kwamba hatupaswi kupenda pesa au vitu ambavyo pesa inaweza kununua. "Upendo wa pesa unasababisha kila aina ya uovu. Watu wengine wameacha imani, kwa sababu walitaka kupata pesa zaidi, lakini wamejisababishia huzuni sana." 1 Timotheo 6:10. Tunaweza kuona wazi kabisa katika ulimwengu unaotuzunguka. Tamaa ya kupata utajiri huleta mateso na uovu mwingi. Walakini sote tunapaswa kushughulika na pesa maishani mwetu, hatuwezi kuizuia. Kwa wengine ni mapambano ya kweli kupata pesa ya kutosha kujikimu; kwa wengine ni kutumia kile walicho nacho kwa busara na haki, au jaribio la kutaka zaidi na zaidi wakati wote.

Meneja mwenye haki

   Yesu anaelezea mfano kuhusu kuwa msimamizi mwadilifu. Meneja ni mtu anayeangalia kitu ambacho kimefanywa kuwa jukumu lake. Katika kuhitimisha mfano huo Yesu anasema: "Aliye mwaminifu lilio dogosana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo huwa dhalimu katika lililo kubwa pia. Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli? Na kama hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?” Luke 16:10-12. Yesu ameiiweka wazi kwamba, Mungu anahitaji kuwa waaaminifu katika vitu vya hapa duniani kwa sababu jambo hili ni la muhimu.

Ni wazi kwamba ni muhimu kabisa kuwa waadilifu katika maswala ya pesa kuishi maisha ya Kikristo kwa moyo wote. Ikiwa hatuwezani na hili, basi ni jinsi gani Mungu anaweza kutupa utajiri wa kweli?

 

Ikiwa una pesa kidogo sana, au ikiwa una pesa nyingi, Mungu anadai uwe mwadilifu na kile ulicho nacho. Karibu miaka elfu tatu iliyopita Sulemani aliandika maneno haya: "Tazama, hili tu nimeliona; Mungu amemfanya mwanadamu mnyoofu, lakini wamebuni mavumbuzi mengi ." Mhubiri 7:29. Katika jamii ya kisasa hii bado ni sawa. Mara nyingi miradi ambayo watu huja nayo ni juu ya njia za kujinufaisha, na hawafikiri juu ya athari hii  kwa wengine walio karibu nao. Na wakati mipango hii inahusu mambo ya pesa, mara nyingi ni 'tamaa', ambayo hufafanuliwa kama "hamu kubwa ya kumiliki kitu". Ni wangapi walio na unyenyekevu wa kuona hii ndani yao? Ni kwa asili yetu kutafuta zaidi na zaidi, kwa sababu ya kiburi chetu na imani kwamba tunastahili zaidi ya kile tulicho nacho.

 

 

Tamaa

Neno la Mungu linasema wazi kabisa juu ya tamaa. Ni moja ya amri kumi za asili ambazo Mungu aliwapa watu wake katika agano la zamani. Na hiyo haijabadilika kwa ulimwengu wa  sasa. “Mwenendo wenu usiwe wenye tamaa; Ridhika na vitu  ulivyo navyo." Waebrania 13: 5 Tuna mfano mzuri kutoka kwa Mtume Paulo, ambaye anatoa ushuhuda wake juu ya mambo haya: "Sikuambii hili kwa sababu ninahitaji chochote. Nimejifunza kuridhika na vitu nilivyonavyo na kila kitu kinachotokea. Ninajua kuishi katika hali ya umaskini  na ninajua kuishi katika hali ya utajiri. Nimejifunza siri ya kuwa na furaha wakati wowote katika kila jambo linalotokea, wakati nina chakula cha kutosha na ninapokuwa na njaa, wakati nina zaidi ya mahitaji yangu na wakati sina mengi. Ninaweza kufanya vitu vyote kupitia Kristo, kwani ananipa nguvu.” Wafilipi 4: 10-13. Kama Wakristo wanaomcha Mungu, lengo letu linapaswa kuwa na ushuhuda huo katika maisha yetu, kwamba tunaridhika na kile tulicho nacho, tukiamini kwamba Mungu atawaangalia wale wote wanaomtumaini.

 

Ikiwa tunajifunza, kama vile Paulo alivyofanya, kuridhika na hali yetu ya kifedha maishani, itakuwa msaada mkubwa kwetu na kwa wale wanaotuzunguka. Hii inamaanisha kuwa sisi ni wasimamizi wa kile Mungu ametupa, kwa uadilifu na sio kwa faida yetu wenyewe ya ubinafsi.

 

"Afadhali  mali kidogo pamoja na haki, kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu." Mithali 16: 8

 

Kufanya kazi kwa bidii kupata pesa sio vibaya, na hakuna fadhila yoyote katika kuwa masikini kuliko kuwa tajiri, lakini ikiwa ni upendo wa pesa ndio unatusukuma kupata zaidi na zaidi na kutafuta zaidi, kuleta machafuko na dhambi ambayo hututenganisha kutoka katika mapenzi ya Mungu, basi kwa kweli tunapaswa kujihukumu wenyewe na kuondoa udhalimu wote.

 

Tafuteni kwanza ufalme wa Mungu

 

Pia sio haki au uungu "kutumia pesa tu bila kufikiria" ili "kuwa na muda zaidi wa vitu vya kiroho." Imeandikwa kwamba "kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani" 1 Wakorintho 14:33 . Kuwa mwaminifu na mwadilifu katika maswala ya pesa inamaanisha kuwa mimi huchukua wakati na juhudi ya kuweka na mambo sawa.

 

Ikiwa tunajifunza kuichukua kama Yesu anavyosema katika Mathayo 6:33, kila kitu kinakua wazi na rahisi. “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake...”-tukifanya hivyo na kuamini hivyo “...hayo yote mtazidishwa,”- hii itatuweka huru kutokana  na wasiwasi juu ya mahitaji yetu ya kidunia.

 

"Na kazi ya haki itakua amani; na mazao ya haki yatakua utulivu na matumaini daima." Isaya 32:17.

 

Kama ilivyo kwa haki yote, kuwa mwadilifu katika maswala ya pesa kuna ahadi kubwa zilizoambatanishwa nayo. “Umependa haki,umechukia maasi; kwa hiyo, Mungu wako amekutia mafuta, mafuta ya shangwe kupita wenzio. " Waebrania 1: 9. Ikiwa sisi ni waaminifu sana na wenye haki na pesa zetu, basi pia tunapata "mafuta ya shangwe". Fikiria amani na raha tunakayoipata wakati tuko huru kutoka kwa mafadhaiko na juhudi za kuchosha ambazo udhalimu na kupenda pesa husababisha! Tunapotenda haki, tunajifunza zaidi na zaidi na inakuwa sehemu ya maumbile yetu.Tunajifunza kuipenda na athari iliyobarikiwa, na amani katika maisha yetu.

Jamii
Chapisho hili linapatikana katika

Nakala hii ilichapishwa hapo awali kwenye https://activechristianity.org/ na imebadilishwa na ruhusa ya matumizi kwenye wavuti hii.