Je, Mungu ni sehemu ya uhalisia wangu?

Je, Mungu ni sehemu ya uhalisia wangu?

Mungu ana mpango na kusudi kwa maisha yangu. Ninaliona hili?

6/10/20253 dk

Written by Isak Ditlefsen

Je, Mungu ni sehemu ya uhalisia wangu?

Watu wengi wanatafuta kitu Fulani maishani - inaweza kuwa , kazi muhimu, hadhi, pesa  nyingi, ili watu wawapende, ili mambo yawe "mazuri zaidi" katika maisha yao nk, na kwa kawaida Mungu hajajumuishwa katika hili. Lakini maisha yakoje hasa?

Je, ninaelewa kweli kwamba haya ni maisha?

Ukweli ni kwamba niko hapa, katika hali yangu ya kawaida ya kila siku, na familia niliyonayo, kazi niliyonayo, afya niliyonayo, uchumi wangu, nchi ninayoishi. Siku zinakuja na siku zinakwenda. Je, ninaelewa kweli kuwa haya ni maisha yangu? Siku hizi za kawaida ambazo zinanijia?

Labda ninahisi kuwa hali yangu ni ngumu. Lakini Mungu amezipanga, anajua mipaka yangu vizuri, anajua mimi ni nani, na upendo wake kwangu ni mkubwa sana. Alikuwa na mpango wa maisha yangu tayari kabla ya msingi wa dunia kuumbwa, mpango wa kina ili niweze kumkaribia Yeye. Ili niweze kumtafuta na kupata msaada. Ili niweze kutambua kwamba ninahitaji msaada, kwamba haiwezekani kuendelea kufuata starehe  na hadhi ya ulimwengu huu, na wakati huo huo kujaribu kumtumikia.

Yesu alikuja katika ulimwengu huu kufanya mapenzi ya Mungu. Sasa tunapaswa kufanya sawa na wafuasi wake. (Waebrania 10: 7.)

Na ikiwa tutatambua ni uwezekano gani tunao tunapomfuata Yesu, basi tusingefikiria hata kujaribu kuepuka hali ambazo tumewekwa. Ikiwa tungeweza tu kufungua macho yetu ili kuona nguvu za mbinguni ambazo zinafanya kazi ulimwenguni kote kutoa msaada mkubwa kwa wale ambao mioyo yao imejitolea kikamilifu kwa Bwana (2 Mambo ya Nyakati 16: 9), na pia thawabu zinazongojea wale ambao ni waaminifu!

Soma zaidi: Je, unajua mipango ya Mungu kwako ni nini? na Waliochaguliwa na Mungu: Tumechaguliwa kwa ajili ya nini? 

Changamoto za kila siku huwa na maana

Hivyo ndivyo ukweli ulivyo! Kama wanafunzi wa Yesu tumeitwa kufanya mapenzi ya Mungu na kushinda dhambi. (1 Petro 2:21-24.) Kushinda dhambi iliyokuja ulimwenguni wakati wa anguko, dhambi ambayo inatujaribu kukasirika tunapohisi makwazo, kuwadharau wengine ambao sio werevu kama sisi. Au ambayo hutudanganya kwa ndoto za starehe na ukuu bila kuona shida halisi: kiburi na kutoridhika na dhambi zingine zote zinazoishi ndani yetu na ambazo hutufanya tusiwe na furaha na hali zetu za kawaida za kila siku.

Mungu ametupa kila kitu tunachohitaji - alimtuma Yesu kuonyesha jinsi ya kushinda dhambi hizi. Ametuma Roho Mtakatifu kutuongoza na kutusaidia katika hali zetu zote za kila siku. Ametupa Neno lake kama mwongozo wa maisha yetu. Tunapaswa tu kuliamini na kulitumia.

Imani inamaanisha hatua. Ni kuwa mtiifu kwa Neno la Mungu na mapenzi Yake, katika majaribu yote yanayojitokeza kila siku, kutii kusema Hapana ninapojaribiwa. Na kuamini kwamba mimi, licha ya kila kitu nilichofanya, sihitaji tena kukubali dhambi inayoishi ndani yangu! Wakati mambo ni magumu, mtu anapofikiria nilipaswa kufanya kazi bora, ninapojaribiwa, basi sitakosa furaha tena na sitalalamika! Ninahitaji kuachiliwa kutoka kwenye dhambi, ndipo nitapata furaha ya kweli.

Wakati haya yanakuwa matakwa yangu makubwa, basi Mungu yupo kunisaidia - Ameahidi hili. " Kwa maana macho ya Bwana hukimbia-kimbia duniani mwote, ili ajionyeshe mwenye nguvu kwa ajili ya hao, waliokamilika moyo kuelekea kwake. Kwa hayo umetenda upumbavu; kwani tangu sasa utakuwa na vita.." 2 Mambo ya Nyakati 16:9.

Soma zaidi juu ya jinsi ya kupigana na dhambi na kushinda katika hali zetu za kila siku: Kupambana na dhambi: Sio lazima iwe ngumu na Tunapaswa kupigana vipi dhidi ya dhambi?

Makala hii inatokana na Makala ya Isak Ditlefsen iliyochapishwa hapo awali katika https://activechristianity.org/ na imebadilishwa kwa ruhusa ya matumizi kwenye tovuti hii.

Shiriki