Je, upendo wako kwa Yesu ni wa kweli?

Je, upendo wako kwa Yesu ni wa kweli?

Kulingana na kile Yesu mwenyewe alisema, kuna njia moja ya kujua kwa hakika kwamba uhusiano wetu na Yeye ni halisi.

31/1/20254 dk

Written by Sharon van Rietschoten

Je, upendo wako kwa Yesu ni wa kweli?

Je, unampenda Yesu na unaamini kwamba wewe ni mmoja wa marafiki zake wa kweli? Huu ndio uhusiano ambao tunapaswa kuwa nao na Yesu ikiwa tunataka kuishi naye milele.

Lakini kuna tofauti gani kati ya kumwamini tu, na kuwa na uhusiano wa kweli na Yeye? Uhusiano ambao Yeye anaishi katika mioyo yetu, ambapo tunakuwa kama Yeye zaidi na zaidi kila siku?

"Mkinipenda, mtazishika amri zangu"

Yesu anasema katika Yohana 14: "Mkinipenda, mtazishika amri zangu... Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye. Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.." Yohana 14:15,21,23.

"Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake. Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda." 1 Yohana 2:5-6.

Yesu ametuwezesha kuzishika amri hizi na kuwa  kama Yeye zaidi na zaidi kila siku! Na ametupa Roho Mtakatifu kama msaidizi. Tunaweza kushika amri zake zote kwa kusema Hapana kwa mapenzi yetu wenyewe na kamwe hatukubali dhambi kwa hiari. Yeye atatupa nguvu zote na msaada kwa hili, ikiwa tutajitoa kikamilifu kwake.

Kufanya mapenzi ya Baba

"Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.!" Mathayo 7:21-23 .

 

Ni muhimu sana kutii amri zake; basi Yesu yupo kwa ajili yetu tunapoomba msaada. Ikiwa tunafanya mapenzi yetu wenyewe, na kuvunja amri zake, basi ukweli ni kwamba tunajipenda wenyewe, na hatumpendi Yesu. "Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake..." 1 Yohana 2:4.

 Kwa kusoma juu ya Yesu na jinsi alivyoishi wakati wake duniani, tunaweza kuona amri Zake ni zipi, tunahitaji kufanya nini ili kumfuata. Amri za Mungu kwa ajili yetu katika wakati wetu ni wazi katika neno lake. Angalia kwa mfano Mathayo 22:37-40 ambapo Yesu anasema: "Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii." Soma pia Mathayo 5:28 na 1 Yohana 2:15.

Biblia pia inasema kwamba sheria za Mungu zitaandikwa mioyoni mwetu badala ya kwenye magome ya mawe kama ilivyokuwa kabla ya Yesu kuja duniani. Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika nia zao nitaziandika; ndipo anenapo. Waebrania 10:16. Tumepewa Roho Mtakatifu kama Msaidizi katika wakati wetu, kutufundisha mapenzi ya Mungu na kutukumbusha maneno Yake. (Yohana 14:26.)

Ahadi kwa wale wanaotii amri zake

Kama vile kulivyo na maonyo ya wazi kwa wale wanaomwomba Yesu msaada lakini hawatii amri zake, pia kuna ahadi kubwa kwa wale wanaompenda kweli (wale wanaoshika amri zake)! lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao."1 Wakorintho 2:9.

Tunapoanza kushika amri Zake na kuyaishi maneno Yake, tunazidi kuwa kama Yesu zaidi na zaidi kila siku. Kisha tutakuwa na furaha na shukrani zaidi kwa amri zake; huleta pumziko la kweli na furaha ambayo ulimwengu hauwezi kutupa kamwe.

"Kuyafanya mapenzi yako, Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu; Naam, sheria yako imo moyoni mwangu." Zaburi 40:8. Ikiwa tuna hili, basi amri zake hazitakuwa ngumu kwetu hata kidogo. "Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito." 1 Yohana 5:3.

Lazima tujifunze kushika amri zote za Yesu ikiwa tunataka kuwa pamoja naye milele; kama tunataka kuwa na furaha na huru katikati ya yote yanayokuja wakati wa maisha yetu duniani.

Tunajua katika mioyo yetu jinsi tunavyo nazo. Ikiwa hatujafanya vizuri, basi tunaweza kufanya uamuzi mpya wa kubadilisha njia tunayoishi na kumpenda Yesu badala yake; Kama vile alivyotupenda sisi kwanza.

"Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele." 1 Yohana 2:16-17.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii ni msingi wa makala ya Sharon van Rietschoten awali kuchapishwa kwenye https://activechristianity.org/ na ilichukuliwa na kupewa  ruhusa ya matumizi kwenye tovuti hii.