Je! wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii wa aina gani?

Je! wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii wa aina gani?

Mbinafsi au msaidizi?

12/7/20163 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Je! wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii wa aina gani?

4 dak

Kuna maneno mengi ya kuelezea namna watu wanavyotumia mitandao ya kijamii. Kwa mfano, ‘Mtoa habari”, “msikilizaji,” “mtafuta kibali” “muundaji,” n.k. napenda kuziweka katika makundi mawili – “mbinafsi”, na “msaidizi.”

Mbinafsi au msaidizi?

Kila siku, popote ulipo, mawazo yako, maneno yako na matendo yako yanachochewa na nafsi yako, ambayo ni kila kitu ambacho kinahusiana na “mimi” na “yangu”, au hamu ya kutumikia na kubariki wengine. Vivyo hivyo kwa jinsi unavyotumia mitandao ya kijamii.

Je! wewe ni mtuniaji wa mitandao ya kijamii wa aina gani? Je! Hisia zako hutegemea maoni mangapi inayopata katika vitu unavyochapisha? Je! Unataka uangalifu zaidi, Je! Unajihisi mtupu na kutoridhika? Chukua dakika moja kufikiria juu ya kinachokuchochea na kukusukuma.

Ikiwa matumizi yako yako ya mitandao ya kijamii yanapotawaliwa na ubinafsi wako, ambapo kila kitu ni kuhusu “Mimi”, na “Yangu”,utakuwa usiyeridhika haraka, ama mwenye kiburi, ama mwenye wasiwasi na mwenye kujishughulisha tu na mambo yako mwenyewe. Vivyo hivyo kwenye maisha ya kawaida ikiwa furaha yako inategemea namna watu wanavyozungumza kuhusu wewe au wanavyokutendea na namna unavyojilinganisha na wengine.

Unajihisi mtupu.

Kwa bahati nzuri, kuna njia ya kutokea – hauhitaji kufikiria juu yako mwenyewe!

Tafuta fursa za kubariki

Msitende neno lo lote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.” Wafilipi 2:3

Ukifanya yaliyoandikwa hapa, inaweza kubadilisha matendo yako, na hata namna ya kufikiri! Hebu fikiri ni namna gani ilivyo vyema kuwa na mstari huu katika malengo yako na kukuongoza kila siku – katika mitandao ya kijamii na katika maisha ya kila siku! Ambapo kabla ulikuwa ukijishughulisha na kuchapisha picha zako nzuri, ama kusubiri maoni au kuzungumza juu juu na marafiki – pengine hata kuwazungumzia wengine vibaya kufanya wewe uonekane mwema – sasa unatafuta fursa ya kubariki.

Mitandao ya kijamii – chombo cha ajabu

Badala ya kuwa na taswira yako binafsi na furaha yako kuamuliwa na kile unachokiona kwenye mitandao ya kijamii, mitandao ya kijamii inakuwa chombo kizuri na muhimu. Unasahau kuhusu wewe mwenyewe na taswira yako mwenyewe na badadala yake unatafuta njia ya kuwatia moyo wengine.

Badala ya kuwa na wivu watu wanapochapisha kitu kuhusu vitu vizuri walivyonunua, au likizo yao, au chochote ambacho huwa unakionea wivu sasa unaweza kufurahi na wale wafurahiao! Wakati hapo awali ulikuwa na hasira au haujali mtu anapopitia wakati mgumu, sasa unawaombea na kutafuta njia ya kuwabariki! Unatuma ujumbe wa kuwatia moyo badala ya kuwadengenya. Unawakumbuka watu kwenye siku zao za kuzaliwa. Unaandika maoni mazuri. Mambo haya madogo yanaweza kuwa na athari kubwa.

Chaguo ni lako

Sisi ni wabinafsi kwa asili, na si kawaida kubariki na kupenda na kufikiria wengine kuwa bora kuliko sisi. Ubinafsi wetu, asili yetu ya dhambi, inapaswa “kusulubiwa pamoja na Kristo” mara kwa mara, ambapo inamaana kwamba nakataa na sitaki kufanya mapenzi yangu tena. (Wagalatia 2:20). Hili ni jambo ambalo unaweza kuamua kufanya, kwa imani. Mungu yuko tayari na anasubiri kukusaidia wakati wote unapojaribiwa, na atakulipa baraka!

Je! Wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii wa aina gani? Ni chaguo lako! Chagua kuwa “msaidizi” wa kweli, na utapata njia ya kusaidia na kubariki haraka – katika mitandao ya kijamii na katika maisha ya kila siku!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye makala ya Irene Abraham awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ na imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.