Kituo cha mvuto wa kiroho

Kituo cha mvuto wa kiroho

Mawazo yako yanavutiwa na nini siku nzima?

17/6/20162 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Kituo cha mvuto wa kiroho

3 dak

Kituo chako cha mvuto

Kila meli ina sehemu maalumu ambayo huitwa Kituo cha mvuto. Hata kama meli “itayumba na kujiviringisha”, sehemu hii hubaki kuwa tulivu. Ikiwa unataka kutopatwa na ugonjwa wa baharini, sogea karibu na eneo hili iwezekanavyo. Japo hutembea pamoja na meli majini, sehemu hii haihusiani na muondoko wa meli.

Hili ni sawa pia katika maisha ya kiroho. Ukitaka kuzuia kuyumbishwa na taabu na mihangaiko katika mwili wako na akili yako, tafuta “kituo”, ambapo utapata pumziko la Mungu. Kituo hiki ni Yesu Kristo. Katika hali ya maisha, tunafanana na meli ambazo husukumwa mbele na nyuma na mawimbi. Wakati tunaponyanyuliwa juu wimbi jingine linaandaliwa kuturudisha chini. Lakini kituo cha mvuto kinabaki kimetulia na hakika, japo sehemu zingine za meli zinayumbishwa na mawimbi mazito.

Mtu anayependa pesa kituo chake chamvuto kipo katika pesa zake. Kila kitu ambacho hufanya husababishwa na tamaa ya pesa, na hata pesa zaidi. Lakini kwa kuwa hali yake ya kiuchumi hubadilika mara kwa mara lazima atakua anaendana na haya mabadiliko ya kupanda na kushuka. Vivyo hivyo maisha ya watu wengi yamechukuliwa na mtindo. Mtindo ukibadilika, nao hubadilika. Hupenda kila ambacho ni maridadi, na wanachukia vitu ambavyo havina mtindo, vya wazi au rahisi. Mienendo yote hii ya kupata vitu vizuri kwa ajili yako mwenyewe inamanisha kituo chako cha mvuto kipo katika vitu vya nje.

“Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwepo moyo wako” Mathayo 6:21.

Wanaoamini na kujiruhusu wenyewe kuwa huru kutoka katika vitu hivi vinavyowazuia kupokea hekima kama kituo chao cha mvuto, na watajifunga katika hekima – watajifunga katika Kristo. Katika kituo cha mvuto cha hekima hakuna hofu kabisa. Pametulia na pana amani na utulivu. Lakini tunapojisogeza mbali zaidi na hekima hofu zaidi na kutotulia vinakuwepo, kukatishwa tamaa, kero na mambo mengine mengi yasiyopendeza uliyo nayo. Kwenye kituo cha hekima mambo yote haya hayapo.

Ni kituo kitukufu kiasi gani: Hekima na nguvu ya Mungu! Wamebarikiwa wale wajao katika utulivu unaopatikana katika “sheria hii ya kituo” ambapo kila mmoja ana chemchemi ndani yake. Watapewa kila kitu.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita katika makala ya Johan Oscar Smith awali ilichapishwa katika https://activechristianity.org/ imechukuliwa na kupewa ruhusa kuchapishwa katika tovuti hii.