Kuna tofauti gani kati ya jaribu na dhambi?

Kuna tofauti gani kati ya jaribu na dhambi?

Naweza kuhisi kama nakuwa mchafu nijaribiwapo. Lakini je, nimitenda dhambi?

6/3/20173 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Kuna tofauti gani kati ya jaribu na dhambi?

3 dak

Imeandikwa na UkristoHai.

Kuna tofauti gani kati ya jaribu na dhambi?

Katika Maisha yangu ya kikristo, naweza kujihisi mchafu ninapojaribiwa, na kwamba nimetenda dhambi katika fikira zangu. Lakini kujaribiwa siyo dhambi, lakini ninapojaribiwa, Imani yangu imejaribiwa, na kwa msaada wa injili (kwa kile kilichoandikwa katika biblia), nitaweza kuendelea kusimama katika majaribu bila kutenda dhambi kamwe.

Dhambi ni mwili – dhambi ndani ya asili yangu ya kibinadamu.

Dhambi ilikuja duniani wakati ambapo watu wa kwanza, Adamu na Hawa, walipomdharau Mungu. Uzao wote wa Adam na Hawa ulirithi asili ya dhambi – wote walizaliwa na tamaa ya kufanya mapenzi yao kuliko kufanya mapenzi ya Mungu. Biblia hutumia maneno mengi kuelezea tamaa hizi za kutenda dhambi: Dhambi ndani ya mwili, dhambi katika asili yetu ya kibinadamu, mwili wa dhambi, sheria ya dhambi, tamaa na hamu, tamaa ya dhambi n.k. Katika Warumi 7:18 Paulo anaandika “Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai nenno jema.” Hapa anaelezea namna tulivyozaliwa na tamaa hizi za kutenda dhambi. Soma pia dhambi ni nini?

Jaribu na dhambi – siyo sawa!

Yakobo anaandika wazi kuhusu jaribu na dhambi katika kitabu cha Yakobo 1:13-15: “Mtu ajaribiwapo, asiseme, ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hawezi kumjaribu mtu” Mstari wa 13. “Lakini kila mmoja hujaribiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kudanganywa.” Mstari wa 14. “Halafu ile tamaa ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi,” Mstari wa 15.

Kutokana na hili tunaweza ona ikiwa tukijaribiwa, siyo sawa na kutenda dhambi; dhambi ni pale unapozikubali tamaa za dhambi zinazoishi ndani ya asili yako ya dhambi. Hivyo kutenda dhambi ni kitu ninachochagua kutenda, na dhambi haiwezi kutokea kama sikubaliani nayo. Soma pia: Inamanisha nini kupata ushindi dhidi ya dhambi?

Hakuna anayepaswa kutenda dhambi!

Anachotufundisha Yakobo hapa, ni kwamba kujaribiwa ni mtihani wa imani yangu, na wale wanaoendelea kusimama imara wakati wa majaribu bila kutenda dhambi watapata taji ya uzima. (Yakobo 1:12) Petro aliandika kwamba tunahitajika kufurahia tunapopita katika mitihani na majaribu, kwa sababu Imani yetu inapimwa hapo, na matokeo yake ni ukombozi wa nafsi zetu. Injili ni kwamba hata kama nimejaribiwa, sipaswi kutenda dhambi – naweza kufuata nyayo za Yesu na kushinda jaribu. Matokeo ya dhambi ni mauti, lakini waishindao dhambi, watapokea uzima wa milele!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org na imechukuliwa na kupewa ruhusa kuchapishwa kwenye tovuti hii.