Adui ni nani na kwa nini nipigane nae?

Adui ni nani na kwa nini nipigane nae?

Tunapaswa kushinda nini? Kwa nini ni kibaya sana?

28/2/20175 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Adui ni nani na kwa nini nipigane nae?

“Ushiriki taabu pamoja na nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu. Hakuna apigaye vita ajitiaye katika shughuli za dunia, ili ampendeze yeye aliyemwandikia awe askari.” 2Timotheo 2:3-4.

Biblia yote imeandika kuhusu maadui, na vita na kuhusu kuchukua mapambano. Tunapaswa kukumbuka kwamba tunapigana katika vita vya kiroho. Tunapigana dhidi ya “…. falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Waefeso 6:12. Katika ulimwengu vitu huwa vya giza, visivyo haki zaidi na zaidi na vyenye dhambi nyingi, lakini tumeitwa kupigana kwa uelekeo mwingine. Tunapigania usafi, haki, kwa ajili ya mapenzi ya Mungu katika dunia yenye kila aina ya ufisadi na watu wenye dhambi. (Warumi 12:2; Wafilipi 2:15.) Ni maisha ya kutenda ambayo kila mkristo anapaswa kuyaishi. Ni jukumu letu kuonesha kwamba mapenzi ya Mungu ni kamili. Tunapaswa kuongoza vita vita dhidi ya shetani na jeshi lake ovu, linalotaka kutawala ulimwengu wote. Tunapaswa kuwazuia kutawala kabisa na kufanya iwe vigunu kwao kutimiza lengo lao. Tunapaswa kuwa mwanga na chumvi katika ulimwengu huu. (Mathayo 5:13-16)

Je, mtu mmoja anawezaje kuleta mabadiliko?

Vita ya kiroho katika Maisha yako binafsi.

Unaweza kuleta tofauti kwa kuwa mwaminifu katika maisha yako mwenyewe. Kama unampenda Yesu kuliko kitu chochote, na unataka kumfurahisha, utafanya kila kitu kumpendeza. Na adui ni kitu chochote kinachotaka kuingia kati yako na Yesu.

Dhambi ni kitu chochote ambacho huenda kinyume na neno la Mungu na mapenzi ya Mungu na huvunja uhusiano kati yetu na Mungu. Tunajaribiwa kutenda dhambi kwa tamaa ya dhambi katika asili yetu ya kibinadamu, na shetani hutumia majaribu haya kujaribu kutuweka katika dhambi. Hufanya dhambi zionekane kuwa nzuri, kama kitu ambacho kitatufanya tujihisi vizuri, lakini ukweli kuhusu dhambi ni kwamba huvunja uhusiano wetu na Mungu na kuondoa baraka zote ambazo huja pamoja na uhusiano huo. Badala yake huleta mateso, upofu, maumivu, na maovu mengine mengi katika maisha yetu.

 Imeandikwa katika Yohana 10:10 kwamba “Mwivi haji ila aibe na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.” Mwizi ambaye Yesu anamzungumzia hapa ni shetani. Lakin tena Yesu anasema amekuja kuleta uzima tele! Uzima tele ni ule tunaoupata tunapopigana na adui huyu. Tunapoona majaribu yetu wenyewe kama vita dhidi ya nguvu za giza ambazo zinataka kuitawala dunia hii, hivyo tunatambua kwa nini biblia inazungumza kwa nguvu kuhusu ushindi, kushinda, na kuwa mwanajeshi. Ushindi mmoja dhidi ya dhambi katika maisha yetu wenyewe ni ushindi dhidi ya mwovu ulimwenguni. Vita ni Zaidi ya maisha yetu binafsi.

Hatujipiganii wenyewe. Tunapigania kuujenga mwili wa Kristo. (Warumi 12:5). Kila anayepigana katika vita hivi vya kiroho ni sehemu ya mwili wa Kristo. Tunapigana kwa ajili ya kila mmoja wetu, kujiimarisha na kujenga kila mmoja wetu. Tukijikita katika kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo yetu na kuendelea kufanya kilichoandikwa katika biblia, tunajiokoa wenyewe kutoka dhambini na wale wanaotusikia. (1Timotheo 4:16) ndipo Mungu anaweza kututumia kwa kutenda mema, kuwa mfano kwa kila mmoja tunaekutana naye. (Warumi 6:12) tunaweza kuwa harufu nzuri ya maisha yanayoelekeza katika uzima, harufu nzuri ya Kristo kati ya wale waliookolewa. (2Wakorintho 6:12)

Uzima wa milele

Tukienenda Zaidi katika njia hii tunazidi kuwa hai zaidi na zaidi rohoni mwetu, na hii ni roho ya milele ndiyo inayotupeleka katika uzima wa milele. Tunapokubali majaribu na ule uhusiano wa milele na baba na mwana unapotea. (Waefeso 2:1) kukubali dhambi ni upotevu wa milele; siyo kipindi kifupi cha kutenda dhambi ambacho unaweza kukilipa haraka. Huwezi kuishi kwa wakati huo tena. Huwezi kupata nafasi tena ya kupata nafasi ya kimungu ambayo ungepokea kwa kipindi hicho. Na tukiendelea kukubali dhambi, kuishi dhambini, hutupeleka mautini. (Yakobo 1:14-15) Hiki siyo kifo cha kimwili. Wote tutakufa kimwili, lakini wale waliowekwa hai katika roho zao huenda kuwa Pamoja na mwokozi. Waliovunja uhusiano wao na Mungu na kutenda dhambi watatumia kipindi kilichobaki kuwa na nia ya kuwa na uhusiano na Mungu na wema wake, lakini hawatakuwa na uwezo wa kuupata. Hiki ni kifo cha kiroho, matokeo ya dhambi. (Warumi 6:20-23.) Hiki ni kitu kibaya zaidi kinachoweza kukutokea! Hii ndiyo maana dhambi ni adui mkubwa kiasi hicho.

Lakini leo hapa, tunapoishi duniani, tunaweza kuchagua kupigana dhidi ya dhambi. Kumpiga shetani kila wakati tunapojaribiwa. Tuna nafasi kubwa hapa, hivyo tusimwache Mungu kwa sababu tumedanganywa na shetani na dhambi. Badala yake tunaweza kuwa na kilio cha aina moja mioyoni mwetu kama alichokuwa nacho Yesu: “Nimekuja nifanye mapenzi yako, Mungu.” (Waebrania 10:7) Hivyo tufanye mapenzi yake, na tunapata uzima wa milele zaidi na zaidi ndani yetu. Hakuna shaka kwamba kila jaribu litakuwa ushindi Mungu akiwa upande wetu. Ana nguvu zote mbinguni na duniani, na anaweza kutupa kila kitu tunachohitaji ili kumshinda adui. Na baraka tunazopata kwa kumpigania kwa uaminifu ni zaidi ya tunavyoweza kufikiria.

Makala hii ilichapishwa awali katika https://activechristianity.org/ na imechukuliwa na kupewa ruhusa kutmika katika tovuti hii.

Shiriki