kutoka katika ugomvi kuwa mwenye shukrani hadi kufurika kwa shukrani.

kutoka katika ugomvi kuwa mwenye shukrani hadi kufurika kwa shukrani.

Ninavyoweza kububujikwa na shukrani.

6/7/20173 dk

Na Ukristo wa Utendaji

kutoka katika ugomvi kuwa mwenye shukrani hadi kufurika kwa shukrani.

4 dak

Imeandikwa katika 1wathesalonike 5:18, “Shukruni kwa kila jambo, maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika kristo Yesu.”

Ukisoma hii, ni rahisi kufikiri kwamba ninapaswa kuwa mwenye shukrani, na kuzingatia kile kilicho chanya na chema, hivyo naweza kuwa mwenye shukrani hata kama si rahisi na mambo hayaendi namna ninavyotaka. Hivyo naamua kupigana vita ya ndani kuwa mwenye shukrani kila wakati. Nadhani hivi ndivyo vijana wengi wa kikristo huanza kupigana dhidi ya kutokuwa na shukrani.

Lakini nilipoyatazama vizuri maisha yangu, nilianza kuona fadhila za Mungu zisizo na kikomo kwangu. Kwa kweli alikuwa na mawazo juu yangu kwabla hajauumba ulimwengu! Alinichgua mimi kati ya wengine wengi kuwa ndugu wa Yesu, kujifunza mambo mengi hapa katika maisha ili nifae kwa kazi ambayo ameiandaa kwa ajipli yangu katika ufalme wake wa milele.

Nilipoona hili, sikuwa na haja ya kupambana tena kuwa mwenye shukranu. Ndipo shukrani kuu ilibubujika moyoni mwangu kwa muumba wangu, kwa upendo wake mkuu kwangu. Moyo wangu ulijaa shukrani nilipofikiria jinsi alivyoongoza hatua zangu katika mdomo wangu – nilipopaswa kufanya maamuzi muhimu ya maisha yangu – ili niwe salama katika mapenzi yake kwenye maisha yangu.

Nilijawa shukrani pia kwa sababu Mungu aliniongoza kukutana na watu wengine waaminifu pia wanaotaka kufanya mapenzi ya Mungu katika maisha yao. Ninashuhudia ushirika wa kweli pamoja na wale wanaotaka kuwa huru kutoka kwenye nguvu ya dhambi, na wale wanaotaka kweli kuishi maisha kama ambayo Yesu aliyaishi. Na nimejazwa na shukrani za milele kwa Bwana na mwalimu wangu, Yesu, ambaye alinipenda sana mpaka akawa tayari kutoa maisha yake mwenyewe ili mimi nikolewe.

Nimefikiria sana ni kwa kiasi gani nilizaliwa na ubinafsi. Fikra zangu na asili yangu ziiljazwa nao. Nilichojali zaidi kilikuwa kuhusu mimi mwenyewe na kwamba wengine wangenizungumzia vizuri na kunisifu kwa mambo niliyofanya. Kwa sababu hii, mara nyingi nilikatishwa tamaa na namna watu walivyokuwa wakinitendea, nililalamika na sikuwa na furaha na watu na hali nilizokutana nazo katika maisha yangu.

Lakini nilipoacha kufikiria juu yangu mwenyewe, na nikaanza kufikiria kuhusu nini ningetoa na kutenda ili kufanya mambo mema kwa wengine, Mimi mwenyewe nilikuwa mwenye furaha. Ilitokea kama tu ilivyoandikwa katika Mithali 11:25., “Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa, anyweshaye atanyweshwa mwenyewe.”

Nilipozingatia kuwakarimu wengine, nilianza kuona watu wengi zaidi ambao walitaka kunikarimu mimi, na moyo wangu ulijawa na shukrani hata zaidi kwa jinsi nilivyoukwa na wema. Fikra hizi za shukrani zilivyoanza kuujaza moyo wangu, moyo wangu uliishia kububujikwa na shukrani pekee. “Kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.” Luka 6:45. Naweza kusema kwamba sasa nina shukrani za kweli na si kupigana vita kubakia kuwa mwenye shukrani.

Ni vyema sana kuwa na pamoja na watu wenye shukrani. Wana furaha daima, wametosheka daima, wanaeneza upendo daima, kamwe hawawezi kutoridhika, kamwe hawalalamiki kuhusu cho chote!

Kwa rehema ya Mungu, nimepokea msaada wa kushinda ubinafsi wangu mwenyewe. (Waebrania 4:16) na nimekuja kwenye maisha yenye shukrani, ambayo kwa kweli ni maisha ya kupendeza.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye makala ya Torger Log awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.