Kuwa na wasiwasi ni kupoteza wakati!

Kuwa na wasiwasi ni kupoteza wakati!

“Je! Kuna yeyote kati yenu kwa kuwa na wasiwasi anaweza kuongeza saa moja katika maisha yake?” Mathayo 6:27

29/1/20183 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Kuwa na wasiwasi ni kupoteza wakati!

4 dak

Katika mahubiri ya mlimani, Yesu anafundisha wazi kabisa jinsi ilivyo vibaya na ujinga kuwa na wasiwasi.

Anaanza ujumbe wake kuhusu kuwa na wasiwasi kwa maneno haya: “kwa sababu hiyo nawaambieni, msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?” Mathayo   6:25.

Watu huwa na wasiwasi, sio tu juu ya bidhaa za mali lakini pia kuhusu kile ambacho wengine wanaweza kufikiria juu yao, na juu ya vile siku zijazo zitakuwa. Utafiti uliofanywa juu ya tabia ya watu ya kuwa na wasiwasi unaonyesha kuwa ni asilimia 10 tu ya vitu ambavyo watu wanahangaikia, huwa vinatokea. Hebu fikiria ni kupoteza muda kiasi gani!

Kutunza maisha ya ndani

Wasiwasi ni ujanja mkubwa wa shetani kutudanganya na kujaza mawazo yetu, na mara nyingi husababisha shaka na kutokuamini. Mawazo ya wasiwasi ni kama chatu, nyoka mkubwa anayeua wanyama kwa kujifunga katika miili yao na kuwasaga. Mawazo ya wasiwasi huharibu maisha yetu ya ndani na Mungu. Yesu anasema, “je! Uzima sio zaidi ya chakula?” Anazungumza juu ya maisha yetu ya ndani na Mungu. Lazima tuchukue tahadhari kubwa katika maisha haya na tuyalishe kwa maneno ya imani, ili yasife. Lakini ni rahisi kufikiria, “Napaswa kuwa na hiki, na lazima niwe na kile pia!” kwa kufikiria hivi, tunajali sana mwili wetu wa nje.

  Lakini kile anachokisema Yesu hapa ni: “Tunza uhusiano wako na Mungu, na usiruhusu huduma yako igeuke kuwa wasiwasi juu ya vitu vya kimwili.” Tunapozingatia mambo muhimu, juu ya maisha ambayo Baba anataka kutupa, tutawekwa huru kutoka wasiwasi wote, kwa sababu Baba huangalia maisha yetu ya ndani, Haiwezekani kuwa na maisha ya ndani na Mungu wakati tunapokuwa na wasiwasi kila wakati juu ya mambo ya nje.

wasiwasi ni kutoamini

 Katika mahubiri ya Mlimani, wakati wa kufundisha kuhusu wasiwasi, Yesu anazungumza juu ya majani ya kondeni, kati ya mambo mengine (Mathayo 6:28-30) Ikiwa tunafikiria zaidi juu ya picha hii, hatuwezi kufikiria kwamba majani ya kondeni yangewahi kusema, “sidhani kama nilifanya vizuri katika eneo hili. Sina asili ya kulia. Ningepaswa kuwekwa mahali pengine!” Hapana, majani ya kondeni hayana wasiwasi juu ya eneo lake. Lakini watu wanaweza kuwa na wasiwasi juu ya mambo haya-kwa mfano, kwamba hawana nafasi maishani ambayo wanafikiri wanastahili.

Yesu huwaambia wale wenye wasiwasi: “Enyi wenye imani haba!” Na Yesu anasema kutokukamini ni dhambi. (Yohana 16:9) tunapaswa kuona wasiwasi kwa njia ile ile. Ni kutokuoamini, na kwa hiyo ni dhambi.

Dawa bora ya wasiwasi ni kujijaza na maneno ya imani na kuamini tu katika maneno mengi yenye kuimarisha imani, hebu fikiria Waebrania 13:5-6 au Warumi 8:31-32, kwa mfano. Mungu hatatuacha kamwe, atakuwa nasi kila wakati, kwa sababu yuko upande wetu. Ahadi hizi ni kwa wanafunzi wa kweli wa Yesu, ambao wamechagua kutopoteza wakati kwa kuwa na wasiwasi. Makala hii inategemea makala ya Svein Gilbu iliyochapishwa hapo awali kwenye https://activechristianity.org/ na imebadilishwa na ruhusa ya matumizi kwenye tovuti hii.

Chapisho hili linapatikana katika

 Makala hii imetafsiriwa kutoka kinorwei, na ilionekana kwanza katika jarida la BCC la “Skjulte skatter” (“Hazina zilizofichwa”) mnamo juni 2004.Imebadilishwa kutumika katika tovuti hii.