Mbona Mungu hatanisikiliza?

Mbona Mungu hatanisikiliza?

Umewahi kuhisi wakati mwingine kwamba Mungu huwa hakusikilizi? Kwa nini Mungu hataki kujibu maombi yako?

1/11/20133 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Mbona Mungu hatanisikiliza?

5 dak

“Kwa nini Mungu huwa hajibu maombi yangu?”

Umewahi kuhisi kwamba Mungu huwa hajibu maombi yako? Umewahi kuwa na siku ambapo mambo yanaendo ovyo na unajikuta unamlilia Mungu, lakini hakuna kinachobadilika? Kwa nini Mungu huwa hajibu maombi yako?

“Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Warumi 8:28.

Ikiwa unaamini kwamba vitu vyote hufanya kazi pamoja kwa wema, hudhani kwamba Mungu anajibu maombi yako kirahisi kwa tofauti na ulivyofikiria?

Huwezi kuyakimbia majaribu yako

Vuta picha unahudumia mteja msumbufu kazini. Labda mpaka analalama dhidi yako na kwa ndani unajihisi mwenye hasira Zaidi.

Anapoondoka unaomba kwamba mteja huyo asirudi tena kwa kuwa huwezi kuvumilia kelele zake tena. Au unaona kwamba kupatwa na hasira siyo namna ambayo ulipaswa kuwa kama mkiristo. Unaomba. “Ooh, tafadhali usiruhusu tena mteja huyu arudi, kwa kweli sitaki kukasirika tena.” Lakini siku inayofuata mteja yule anakuja tena kulalama Zaidi! Unadhani kwamba Mungu hakusikia ombi lako?

“Wapenzi msione kuwa ni ajabu ule msiba ulio kati yenu, unaowapata kama moto ili kuwajaribu, kana kwamba ni kitu kigeni kiwapatacho. Lakini kama mnavyoshiriki mateso ya kristo, furahini; ili na katika ufunuo wa utukufu wake mfurahi kwa shangwe. 1 Petro 4:12-13.

Kwa nini unaombea majaribu na mitihani iondoke? Huwezi kuishi maisha yako yote bila kukutana na mtu anayekufanya uwe na hasira. Watu kama hao wapo kila mahali! Mungu huruhusu kupatana na watu hawa ili uwe na fursa ya kuishinda hasira yako na kuwa mwenye kupenda zaidi na mwenye uvumilivu.

Kamili na timilifu, haihitaji chochote

“Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali; mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi. Saburi na iwe na kazi timilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa na neno.

Je! Hili siyo suluhisho bora? Kuwa mkamilifu na mtimilifu, na kuwa na kila kitu unachohitaji?

Kwa kweli ndiyo! Lakini Mungu ametunga sheria, na kama tutazifuata, tutafika huko. Mungu hawezi kufanya hasira yako ipotee kwa siku moja. Anataka kuona kama unataka kufanya mapenzi yake na kumheshimu. “Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.” Mathayo 6:10.

Badala ya kuuliza mbona Mungu hakusikilizi, labda unapaswa kujiuliza kwa nini haumsikilizi Mungu! Ikiwa kweli unataka kufanya mapenzi ya Mungu, atajibu maombi yako kwa Subira na kwa majaribu sahihi ambayo yatakufundisha kuwa mwenye Subira. Kama unahisi kwamba Mungu hasikii maombi yako, jiulize mwenyewe kama ulisema “Mapenzi yako yatimizwe” kwenye kila hali.

Usimwombe Mungu akuondolee majaribu na mitihani; mwombe akutie nguvu ya kutumia majaribu hayo kuwa kama Yesu! Ndipo atakuwa Zaidi ya kutaka kujibu maombi yako! Ndipo hautakua na siku nyingine ya kukosa matumaini tena!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.