Kwa watu wanaotaka kufanya utofauti

Kwa watu wanaotaka kufanya utofauti

Kuna vita tunahitajika kupigana, vita dhidi ya dhambi – ambayo ni mzizi wa mateso yote.

10/3/20144 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Kwa watu wanaotaka kufanya utofauti

Ulimwengu umejawa mateso; magonjwa, vifo, njaa, vita, udhalilishaji. Unahisi kwamba unataka kufanya utofauti katika ulimwengu lakini uko peke yako kati ya mamiliomi ya watu wengine. Lakini ulijua kwamba biblia inasema kwamba tunaweza kweli kusaidia kusitisha mateso ulimwenguni?

Nguvu ya kuchagua

Hapo mwanzo Mungu alimuumba Adamu na Eva. Aliwapa mapenzi huru. Aliwapa nguvu ya kuchagua.

Mwanadamu wa kwanza alichagua kutenda dhambi – walichagua kumsikiliza nyoka badala ya kutii amri nzuri kutoka kwa Mungu wao mpendwa. Walidhani walikuwa wanajua kuliko Mungu.

Mateso yote ni matokeo ya moja kwa moja ya dhambi hiyo. Mambo yote katika dunia na katika ufalme wa mbingu hufuata sheria. Mungu ni Mungu wa haki, na sheria zake haziwezi kubadilika. Moja ya sheria hizi ni, kwa mfano “kiburi hutangulia uangamivu” kama ilivyoandikwa katika Mithali 16:18. Kiburi ni pale unapodhani wewe ni mwema ama unajua Zaidi. Adamu na Eva walipochagua kutotii amri za Mungu na kula tunda walilokatazwa, matokeo yalikuwa mwanzo wa dhambi na uangamivu.

Jambo tunaloweza kufanya

Shetani anapokuwa na nguvu katika dunia hii, kutakuwa na dhambi na uharibifu. Kwa sababu ya chaguo la Adam na Eva, ilikuja kuwa asili kwa watu wote kutaka kufanya mapenzi yao badala ya kumtii Mungu.

Mungu kamwe hakutaka ulimwengu uwe katika hali hii ya kutisha, siyo kipindi hicho wala leo. Anataka kuwa na roho yetu. Hutuita kwake, na tunapojibu, anaweza kututumia kufanya kazi yake kamili ya kuharibu dhambi katika maisha yetu, na kwa njia hii huimaliza kazi ya mwovu.

Unapomkabidhi Mungu maisha yako, ma kufanya maamzi thabiti kufanya mapenzi yake badala ya mapenzi yako mwenyewe, “vita” huanza – vita vya kumaliza nguvu ya dhambi na uharibifu maishani mwako. Vita dhidi ya asili yako ya kibinadamu mwenyewe, ambayo siku zote huwa inataka kufanya mapenzi yake mwenyewe badala ya mapenzi ya Mungu. Unapopigana vita hivi, unatimiza wajibu wako wa  kumaliza kazi ya mwovu – ambaye huua na kuharibu. Kwa kupigana vita hivi, unatimiza wajibu wako wa kushinda mzizi wa mateso katika ulimwengu huu!

Matokeo ya vita hivi

Matokeo ya vita hivi ni kwamba maisha yako yanakuwa baraka. Unapokuwa mwaminifu kwenye maamzi yako kufanya mapenzi ya Mungu unaweza kuwambia wengine, “Nifuate, kama ninavyomfuata Kristo.” Unashinda dhambi na unajawa na furaha, badala ya kutenda dhambi na kushuhudia uharibufu, Zaidi na zaidi tena. Unatengeneza amani ulipo katikati ya mateso. Uaminifu wako mwenyewe kwa Mungu pia huleta baraka kwa Watoto wako na vizazi vijavyo.

Utakuwa pamoja kwenye kufuta machozi pamoja na Mungu na Yesu katika maelfu ya miaka yenye amani, katika milenia. Imeandikwa katika ufunuo kwamba wote wanaoshinda dhambi na nguvu ya dhambi katika maisha yao wenyewe walipokuwa duniani, watanyakuliwa. Baada ya unyakuo itakuja milenia ya maelfu ya miaka ya amani, wakati ambapo shetani atakuwa amefungwa, wakati ambapo utatumia kile unachojifunza leo kusafisha uharibifu uliosababishwa na dhambi katika dunia hii!

Unakuwa mwenye furaha. Ni dhambi inayotufanya tusiwe na furaha. Kutii sheria na amri ambazo Mungu ameandika mioyoni mwetu huleta amani na furaha.

Utaishi na kutawala pamoja na Yesu milele yote! “Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi.” Ufunuo wa Yohana 3:21.

Changuo ni lako

Mungu bado ana nguvu mbinguni na duniani. Mungu bado ni pendo. Na bado una uhuru wa kuchagua. Kila siku, unaweza kuchagua kupigana dhidi ya shetani na nguvu ya dhambi, na maisha yako yanaweza kuwa silaha kwa Mungu!

“Nazishuhudia mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako baraka uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao wako.” Kumbukumbu la torati 30:19.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala ya Irene Laing awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ imachukuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii.