Mistari 14 ya Biblia inayothibitisha kwamba Mungu anataka tushinde dhambi

Mistari 14 ya Biblia inayothibitisha kwamba Mungu anataka tushinde dhambi

Hapa kuna mistari michache kuhusu ahadi tukufu ya Mungu kwetu: tunaweza kushinda dhambi!

26/5/20173 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Mistari 14 ya Biblia inayothibitisha kwamba Mungu anataka tushinde dhambi

6 dak

Kushinda dhambi: Kusudi la Mungu  kwetu!

Biblia inaahidi wazi wanafunzi wote waaminifu wa Yesu kwamba watashinda dhambi. Mungu anataka tuachane kabisa na dhambi. Ingawa injili ni wazi sana, mara nyingi haieleweki au hata kupuuzwa. Chini ni baadhi ya mistari ya wazi ambayo inathibitisha zaidi bila shaka mapenzi ya Mungu kwetu ni nini - na hiyo ni kwamba dhambi haitakuwa na nguvu yoyote juu yetu tena!

Mathayo 5:48:

"Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Warumi 6:12-14:

"Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake; wala msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki. Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.."

Warumi 8:12-13:

" Basi, kama ni hivyo, ndugu, tu wadeni, si wa mwili tuishi kwa kufuata mambo ya mwili, kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.."

1 Wakorintho 15:34:

"Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.."

2 Wakorintho 2:14:

"Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu."

Wakolosai 3:5:

"Basi, vifisheni viungo vyenu vilivyo katika nchi, uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya, na kutamani, ndiyo ibada ya sanamu."

Waebrania 2:17-18:

"Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake. Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa"

Waebrania 4:15-16:

"Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.."

1 Petro 2:21-22:

"Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake. Yeye hakutenda dhambi, wala hila haikuonekana kinywani mwake.."

1 Petro 4:1-2:

"Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi.  Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani.."

2 Petro 1:10:

"Kwa hiyo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara kuitwa kwenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe."

1 Yohana 3:3:

"Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu."

1 Yohana 3:6-7:

"Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua. Watoto wadogo, mtu na asiwadanganye; atendaye haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki;"

Ufunuo 3:21:

"Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.."

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii ilichapishwa awali kwenye https://activechristianity.org/ na imebadilishwa na ruhusa ya matumizi kwenye tovuti hii.