Samweli: Jinsi ya kusikia sauti ya Mungu

Samweli: Jinsi ya kusikia sauti ya Mungu

Samweli alikuwa maalumu toka utoto. Hadithi yake inatuonesha ni jinsi gani ilivyo muhimu kusikiliza sauti ya Mungu na kuitii, kwa namna yo yote.

30/1/20244 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Samweli: Jinsi ya kusikia sauti ya Mungu

6 dak

Kuhani mkuu Eli alikuwa mzee wakati Samweli, kama kijana mdogo, alipoenda kuishi na kumtumikia katika hekalu. Vijana wa Eli walipaswa kurithi ukuhani Eli alipofariki, lakini hawakuvutiwa kumtumikia Mungu. Walikuwa waovu na hawakuonesha heshima yeyote kwenye sheria za Mungu, na Eli hakuwa na nguvu wala nia ya kuwasukuma kuacha dhambi zao. (1 Samweli 2:12-17) Matokeo yake, Mungu hakuzungumza na Eli kama ilivyokuwa kwa wengine, kama Musa.

Wakati Samweli mdogo anaenda kuishi hekaluni, Mungu alimtazama kwa karibu. Mama wa Samweli aliahidi kumleta Samweli hekaluni ili amtumikie Mungu kuanzia utoto wake. Mungu alikumbuka hili na alikuwa akisubiri wakati sahihi wa kuzungumza na Samweli kwa njia ambayo hakuifanya kwa Eli na vijana wake.

Mungu aliona moyo safi ndani ya Samweli

Nini kilifanya kijana mdogo huyu kuwa maalumu kiasi kwamba Mungu atake kuzungumza nae? Imeandikwa kwamba Bwana hakuongea mara kwa mara kwa mara na wanadamu siku hizo, na hapakuwa na maono mengi. (1 Samweli 3:1) Mungu alikuwa amemuonya Eli kwamba familia yake ingevunjwa, anasema, “Nami nitajiinulia kuhani mwaminifu, atakayefanya sawasawa mambo yote niliyo nayo katika moyo wangu, na katika nia yang. Nitamjengea nyumba iliyo imara; naye atakwenda mbele ya masihi wangu milele.” 1 Sanweli 2:35. Alikuwa anatafuta mtu mwenye moyo safi na aliona hili kwa Samweli.

Mungu alipomwita usiku mmoja, Samweli alidhani kwamba alikuwa Eli. Alizoea kuwa mwenye nindhamu, hivyo aliamka mara moja. Hii ilitokea mara tatu, na hatimae Eli alitambua kwamba Mungu alikuwa anajaribu kuzungumza na kijana mdogo. Hivyo alimwambia Samweli kwamba akisikia tena sauti , anapaswa ajibu, “Nena Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia.” (1 Samweli 3)

Nimekuwa nikiwaza mara nyingi kuhusu Samweli na majibu yake rahisi. Nilifikiri juu ya jinsi gani ilivyo muhimu kuwa macho zaidi na kusikiliza Mungu anapajaribu kuzungumza na mimi. Wakati wa Samweli Mungu alizungumza na manabii na makuhani, na ndipo wao walienda kuzungumza na watu. Lakini sasa Mungu huzungumza nasi moja kwa moja kupitia roho wake mtakatifu.

Sheria na hekima za Mungu zinapatikana katika biblia. Kwa mfano imeandikwa katika kitabu ya Yohana 14:21 kwamba “Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.” Hivyo kama nitalijua neno la Mungu na kulitii, nitapokea roho mtakatifu. Kisha kama nitaendelea kuwa mwaminifu, nitajifunza kusikia suti yake moyoni mwangu zaidi na zaidi na inaweza kuniongoza katika maisha yangu ya kila siku.

Uhusiano na Mungu wa moyo -kwa -moyo

Mungu alipozungumza na Samweli kwa mara ya kwanza, alikuwa na kazi muhimu kwa Samweli kuifanya- jaribio la kuthibitisha imani yake. Imeandikwa kwamba Samweli aliogopa kumwambia Eli alichosema Mungu. (1 Samweli 3:15.) Lakini Eli alitaka kusikia, hivyo Samweli alimwambia: Mungu alikua tayari kutimiza ahadi zake dhidi ya Eli na vijana wake, na alimuweka Samweli katika eneo la Eli kama nabii kwa ajili ya watu wake.

Samweli alikuwa na moyo safi, lakini Mungu alihitaji kumjaribu katika hali hii. Ni sawa pia kwetu. Mungu hututumia kazi ambazo huthibitisha imani yetu. Zinaweka kuonekana kuwa ngumu – labda Mungu anataka anataka sisi tumwambie mtu ukwel, kama Samweli, hata kama tunajua kwamba mtu mwingine hapendi kusikia. Lakini kama nataka kuthibitisha kwamba nampenda Mungu kuliko chochote, ndipo ninahitaji kutii mara moja Mungu anapozungumza na mimi moyoni mwangu. Ninapotii haraka ndipo matokeo yanapokuwa mazuri.

Maeneo katika biblia ambapo nabii Samweli ametajwa yanatuonesha kwamba aliweka moyo wake safi katika maisha yake yote, na matokeo yake alisikia sauti ya Mungu. Alipowaombea watu, Mungu alisikia.

Nii dhambi ambayo hututenganisha na mungu. Imeandikwa katika kitabu cha Yakobo 4:6 kwamba, “Mungu huwapinga wajikwezao, bali huwapa neema wanyenyekevu.” Kama hatutaki kunyenyekea katika mapenzi ya Mungu, kumtii yeye na kuharibu nguvu ya dhambi, tutashuhudia kwamba tunawekwa mbali na neema ya Mungu, kama tu ilivyokuwa kwa Eli. Lakini ikiwa tutweka mioyo yetu safi, tunaweza pia kuwa na uhusiano wa moyo kwa moyo na Mungu, ambapo anaweza kuzungumza na sisi, kama alivyofanya kwa Samweli. Ndipo pia tutakuwa wafanyazi wenzake, kama alivyokuwa nabii Samweli katika wakti wake!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye makala ya Heather Crawford awali ilichapishwa kwenye https://activechristianity.org/ imechukuliwa na kupewa ruhusa kutumika kwenye tovuti hii