Namna unavyoweza kuwa mwinjilisti mwenye ufanisi zaidi.

Namna unavyoweza kuwa mwinjilisti mwenye ufanisi zaidi.

Njia muhimu ya kuwa mwinjilisti mwema.

7/10/20155 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Namna unavyoweza kuwa mwinjilisti mwenye ufanisi zaidi.

“Basi, enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la baba, na mwana na roho mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi. Mathayo 28:19.

Maelekezo haya ambayo yesu aliwapa wanafunzi wake mara nyingi huitwa “Amri kuu” na ni kusudi na malengo ambayo Yesu alikua nayo kwa wanafunzi wake. Katika pendo lake na lisilo na ukomo na hekima, anahitaji wengi iwezekanavyo kuja katika maisha yenye furaha na amani pamoja na Mungu. (2Petro 3:9)

Kwa bahati mbaya shetani hujaribu sana kuwafanya watu wafuate njia nyingine. Na wakati mwingine licha ya juhudi zako zote unapotaka kuwaleta watu kwa kristo yeye huwasukumia mbali zaidi.

Pigania wokovu wako mwenyewe.

Paulo aliandika wazi kabisa kwamba namna ya kuwasaidia wengine ni kujitazama mwenyewe. “Jitunze nafsi yako na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia. 1Timotheo 4:16

Labda hii haionekani kuwa sahihi, lakini ni hekima. Paulo alijua kwamba hakuna mtu angeweza kudanganywa na yule anayejiita “mkristo” anayejaribu kuhubiri maisha ambayo yeye mwenyewe alikua hayaishi. Hivyo njia ya kufanyanya watu kua wanafunzi ni kuishi maisha ya kiuanafunzi mwenyewe.

Amri kuu yote inaweza timizwa kwa kufuata mawaidha rahisi ya Paulo. Hakuandika kwamba ujitunze nafsi yako na mafundisho halafu baada ya hapo unaweza kwenda kuwasaidia wanaokusikiliza. Hapana, ni kwa kujitunza mwenyewe ndipo utaweza kuwaleta wengine kwa kristo.

Kwa maneno mengine, Paulo anasema ikiwa unataka kuwasaidia watu waokolewe, lazima uwe makini na kile ambacho Mungu anakuamuru ufanye katika maisha yako. Yeye atafanya sehemu iliyobaki. Atakuonesha wakati wa kuzungumza na watu na nini cha kusema na namna gani utakavyosema.

Maisha ya kuvutia.

Kama ulisoma mapema katika kitabu cha 1Thimotheo 4, unaweza ona mambo machache ambayo Paulo alimaanisha kwa kusema “Jitunze nafsi yako na mafundisho yako”.

“Mtu yeyote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwa waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi. Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha. Usiache kuitumikia karama ile iliyomo ndani yako uliyopewa kwaa unabii na kwa kuwekewa mikono na wazee. Uyatafakari hayo; ukae katika hayo; ili kuendelea kwako kuwe dhahiri kwa watu wote”. 1Timotheo 4:12-15.

Kuwa mfano katika upendo. Katika usafi. Katika imani. Katika tabia. Soma mafundisho yaliyoandikwa katika biblia. Kuwa makini na mawaidha unayopata.  Kwa kifupi fanya mapenzi ya Mungu katika maisha yako. Kufanya mapenzi ya Mungu ni kuwa huru kutoka katika dhambi na kuishi maisha ambayo ni matakatifu, yaliyo safi na yasiyokuwa na lawama.

Na ndipo utakua kama Paulo aliyeandika, “Na neno langu na kufundisha kwangu hakukuwa kwa manenoya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na nguvu za Mungu” 1Wakorintho 2:4 . Ukienenda katika njia hii Mungu atakupa nguvu uzungumzapo. Ndipo maneno yako hayataonekana yenye kushawishi tu. Maneno yako yatakuwa yenye kuridhisha, yenye nguvu, na hekima ya maisha ya imani. “Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea chumvi, mpate kujua jinsi mpasavyo kumjibu kila mtu” Wakolosai 4:6.

Ikiwa utaishi maisha kama haya, utakua “Biblia” katika miguu miwili ambapo watu wanaokuzunguka wanaweza “kusoma”. Lakini kama hawawezi kukuona ukiwa huru toka katika dhambi, ukiwa mwenye furaha tele, mwenye amani, mnyenyekevu, mwenye fadhili, mvumilivu na mwenye kubariki, hivyo kwa nini wahitaji kuwa wakristo?

Mungu hufanya kazi ndani yetu.

Imeandikwa kwamba “Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu kwa kulitimiza kusudi lake jema”. Wafilipi 2:13. Na kwa kuwa tunafahamu kuwa kusudi jema la Mungu ni kwamba watu wengi iwezekanavyo wanaokolewa, hivyo tunajua kwamba Mungu atatenda kazi ndani yetu ili kusudi lake liweze kutimia.

Ukiwa mwenye kuheshimu kwa asilimia mia kila kitu ambacho Mungu amekiweka moyoni mwako ukifanye, na unaishi maisha yenye usafi, yasiyo na lawama na matakatifu, hivyo ataweza kukutumia wewe ili aweze kuwaokoa wale wanaokuzunguka na kuwaleta kwa Kristo.

Maandiko pia yanasema “Hakuna awezaye kuja kwangu, asipovutwa na baba aliyenipeleka”. Yohana 6:44. Hakuna hata mmoja ambaye amebadilishwa na mtu mwingine kuwa katika kristo. Ni Mungu mwenyewe ndiye huwavuta watu kwake. Lakini unaweza kufanya kazi na Mungu na akakutumia kama chombo ambacho anaweza kukitumia kuwaleta watu kwake.

Mungu anataka watu waokolewe. Na kama unataka kile Mungu anataka, atakutumia kusaidia kutimiza lengo hili. Hata kama inaonekana kama kutoleta maana, njia ya kufanya hili ni kujitazama mwenyewe na kuuliza “Mungu, unataka nifanye nini katika maisha yangu? dhambi zipi naweza zisafisha katika maisha yangu? ni majivuno yapi na unafiki ambao natakiwa kuushinda? Je, nawezaje kuuonesha maisha ya kristo ndani yangu?”

Na wakati ambapo huu mwanga mweupe halisi unang’aa kutoka kwako, wakati mambo unayosema na kufanya yanafanana na yale ambayo kristo mwenyewe alikua akisema na kufanya, wakati ambapo kuna amani kuu, furaha, na usafi ndani yako hivyo wengine wataona toka kwako. Na ndipo Mungu ataweza kukutumia wewe.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii ilichapishwa katika https://activechristianity.org/ na imepewa ruhusa kutumika katika tovuti hii.