Nawezaje kuwa mkristo wa kweli?

Nawezaje kuwa mkristo wa kweli?

Kuna tofauti kubwa kati ya watu wanaojiita wenyewe wakristo. Ni wangapi twaweza sema ni kweli wanamtukuza Mungu katika maisha wanayoishi?

23/10/20123 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Nawezaje kuwa mkristo wa kweli?

5 dak

Unapaswa kufanya nini ili uwe mkristo?

Unapaswa kufanya nini ili uwe mkristo? Sio vigumu unavyofikiria.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya watu wajiitao wakristo. Hebu tufikirie juu ya mamilioni ya wakristo – ni wangapi tunaweza sema kwa kweli wanamtukuza Mungu katika maisha yao?

Si vigumu kuwa mkristo, na haipaswi kuwa vigumu. Lakini tunaweza sema kwamba “wakristo wote” wataurithi ufalme wa mbingu? Unapaswa kufanya nini ili kuwa mkristo? Kwanza unapaswa kuwa mkristo wa kweli na uamue kuwa hivyo. Watu wengi walikua kama “Wakristo”, Lakini kamwe hawayaachi maisha yao ya zamani; kila mara huwa na dhamira mbaya ndani yao. Ukristo kwa wengine ni kwa ajili ya kujionyesha mbele ya watu. Lakini vipi kuhusu wewe? Je unataka kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu?

Mwaliko kutoka kwa Mungu upo wazi kwa kila mtu, lakini maamuzi ni yako. Usisubiri kufanya maamuzi. Huenda usipate nafasi kama hii tena.

Fikiria kuhusu maisha yako.

Unahitaji kuanza kutambua kile unachokifanya. “Alipotambua alichokua anafanya, alifikiria…. ‘Nitaondoka nirudi kwa baba yangu”. Luka 15:17-18. Unapoishi maisha ya kawaida yanayoitwa maisha ya kikristo kama mtenda dhambi, unajidanganya mwenyewe. Fikiri juu ya hili, Hutakiwi kabisa kuishi kama hivi! Hutakiwi kujifanya mkristo ilhali ndani yako unajua kwamba dhambi inakuongoza. Labda umefungwa na tamaa ya pesa, au una mawazo machafu? Labda unajua kwamba wewe ni mvivu, au ukristo wako ni kwa ajili ya kupata heshima kutoka kwa watu?

Umezoea kuishi maisha ambayo kiukweli yanapingana na moyo wako. Fikiri kuhusu maisha yako. Kama vile mwana mpotevu, utasemea, “ Kwa nini nisiishi hivi?” Kwa nini nisiwe mwenye furaha, Ujihisi kuhukumiwa na dhamiri yako, Kuwa mbali na Mungu? Angefurahi sana kukupokea. Unaweza kuishi kwa uaminifu mbele ya Mungu, na roho mtakatifu kama mshauri wako.

Kubali ukweli kuhusu wewe mwenyewe

Kubali ukweli kwamba unatenda dhambi. “Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote”. 1Yohana 1:9. Yesu na Paulo wote wanatuambia tuache kutenda dhambi kwa kudhamiria. (Yohana 8:11; 1Wakorintho 15:34) yeyote aliye ndani yake hatendi dhambi. Wakristo wengi hawajali kuacha kutenda dhambi. Ukristo wao ni njia tu ya kuwapa dhamiri nzuri. Wengine wana ugumu zaidi kiasi kwamba hutumia ukristo kama njia ya kujipatia vitu katika ulimwengu huu. Huwa wanafikiria kila aina ya miradi na mbinu kwa ajili ya kuomba pesa huku wakijifanya kuwa wakristo wazuri, lakini kiukweli wameridhika na maisha yao ya dhambi na hivyo hufanikiwa na mipango yao ya ujanjaujanja.

Ikiwa utakubali kwamba wewe kama mkristo bado unatenda dhambi na haujafika katika maisha ya ushindi dhidi ya dhambi, na una huzuni kubwa kuhusu hali hii, hivyo kuna tumaini kwa ajili yako. Kama kweli una hamu ya ushindi, hivyo upo tayari kumkabidhi  Mungu maisha yako yote . Kama umechoka kutenda dhambi, kuja kwa Yesu, ambaye anaweza kukusaidia. (Mathayo 11:28)

Uaminifu kamili

Unapaswa kuwa mwaminifu kabisa kwako na kwa Mungu. Labda wewe ni mwerevu na uliyejaaliwa na unaweza kuwafanya watu waamini kwamba wewe kweli ni mkiristo mzuri. Lakini huwezi kumdanganya Mungu. Ni dhambi ndiyo husababisha kututenganisha na Mungu. Mungu ana nguvu ya kukusaidia, kama una nia ya kuacha kutenda dhambi na kumkabidhi maisha yako yote. Yesu alikuja katika ulimwengu huu ili kutuokoa sisi toka katika dhambi zetu.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita katika makala ya Elias Aslaksen ambayo awali ilichapishwa katika https://activechristianity.org/  na imepewa ruhusa kuchapishwa katika tovuti hii.