Je! ninapata wapi maisha yatakayo nipeleka katika uzima wa milele?

Je! ninapata wapi maisha yatakayo nipeleka katika uzima wa milele?

Je, una tumaini la maisha ya milele? Unaweza kuishi maisha ambayo yatakupeleka katika uzima wa milele katika muda wako hapa duniani?

8/11/20183 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Je! ninapata wapi maisha yatakayo nipeleka katika uzima wa milele?

4 dak

Maisha yanayoelekeza kwenye uzima wa milele

 

Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na baba, bali vyatokana na dunia. Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.” 1Yohana 2:15-17.

Hapo tumeipata. Maisha pekee yanayoweza kutupeleka katika uzima wa milele ni maisha ambapo tunafanya mapenzi ya Mungu.

 Mtume anamaanisha nini anaposema “tamaa ya mwili ambayo watu huona na kuhitaji, na kila kitu katika ulimwengu huu ambavyo watu hujivunia, hakuna chochote kati ya hivi kinachotoka kwa baba; vyote vinatoka katika ulimwengu?”  inamaanisha kwamba si baba, muumba wetu ambaye anasababisha tamaa hizi. Ni miungu ya hii dunia anayesababisha haya. Ndiye ambaye Yesu alimzungumzia kwamba “Mwizi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele” Yohana 10:10. Mmoja hukuibia na mwingine hukupatia. Mwizi huiba furaha katika maisha yako, “huua” nia yako ya kuishi na kuharibu maisha yako ya baadaye.

Tamaa na hamu haziwezi kuridhishwa

 

Ni muhimu kuelewa hili. Hatuwezi kusaidia kuwa na tamaa na hamu katika mwili wetu, katika asili yetu ya dhambi. Lakini lazima tuelewe kwamba haya yapo kama matokeo ya anguko la mwanadamu. (Mwanzo sura ya 3) Mungu alituumba na akili, na alimaanisha tuzitumie kufurahia kila kitu alichokiumba – katika usafi wote. Kwa mfano Paulo aliandika kuhusu chakula: “………. ambavyo Mungu aliviumba vipokewe kwa shukrani na walio na imani wenye kuijua hiyo kweli.” 1 Timotheo 4:3.

Wakati mwingine kukidhi mahitaji ya kiasili kama vile chakula vinaweza kupokelewa kwa kutoa shukrani – yaani kwa kushukuru. Lakini tamaa ya dhambi haiwezi kuridhishwa kwa shukrani. Huwa haitosheki, huwa haina kikomo, kama moto ambao hutaka zaidi na zaidi. Hamu na tamaa za dhambi haziwezi kutupa chochote; yenyewe huchukua. Huchukua kila kitu, na inakuacha bila furaha yoyote au kitu cha kuridhisha.

Yuda anaandika kuhusu matokeo ya kuishi kutokana na tamaa na hamu za kimwili: “Watu hawa ni wenye kunung’unika wenye kulalamika, waendao kwa tamaa zao…...” Yuda 16”. Unaweza fikiria kwamba wanaweza kuwa wenye shukrani na wenye furaha. Lakini matunda ya tamaa zao ni manung’uniko, na kulaumu, kukata tamaa na uchungu. Maisha haya hayawezi kukupeleka katika uzima wa milele.

Matokeo ya shukrani

 

Habari njema ni kwamba tamaa zinaweza kusulubiwa na imani. Kumbuka – weka kiunga cha makala inayoelezea dhana ya ‘kusulubiwa kwa imani’ kwa sababu “Na hao walio wa kristo Yesu amewasulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake.”  Wagalatia 5:24. matokeo ya mwisho ya hili ni shukrani. Tumepokea kitu na tunaweza kusema ahsante.

“Na huo ni ushuhuda, ya kwamba Mungu alitupa uzima wa milele; na uzima huu umo katika mwanawe.” 1Yohana 5:11. ni maisha pekee ambayo tunaweza kuwa na ushirika na Mungu, na kumheshimu, ndiyo yatakayotupeleka katika uzima wa milele.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita katika makala ya Øyvind Johnsen mwanzoni ilichapishwa katika https://activechristianity.org/  na imechukuliwa  na kupewa ruhusa kuchapishwa katika tovuti hii.