“Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionayo ni wachache.” Mathayo 7:14.
Tembea katika njia nyembamba iendayo uzimani
Wale wasioitafuta njia nyembamba hawatafuti njia iendayo uzimani. Kila mmoja anataka kuwa na uzima, lakini kuna nyia iendayo uzimani, na tunapaswa kupitia katika njia hii ikiwa tunataka kupokea uzima. Uzima nini? “Angalia, nimekuwekea leo mbele yako uzima na mema, mauti na mabaya…….” Kumbukumbu la Torati 30:15,19. Uzima ni matunda ya roho kama vile utu wema, Fadhili, upendo n.k. (Wagalatia 5:22) Mauti ni matendo ya asili yangu ya dhambi, kama vile kusema uongo, kudanganya, wivu n.k.
Kuna tofauti kati ya matunda ya roho na karama za roho. Kunena kwa lugha, karama ya uponyaji, n.k, ni karama unayoweza kupokea, na Wakorintho walikua na karama hizi. (1Wakorintho 1:5-7)
Lakini hatuwezi kupokea tu matunda ya roho, lazima tuwe watiifu kwa kile ambacho roho hutwambia ikiwa tunataka kuyapokea. Tunapaswa kutembea kwenye njia nyembamba, ambapo roho hupinga dhambi katika asili yetu ya kibinadamu. Ikiwa tunataka kumfuata Yesu kwenye njia nyembamba, tunapaswa kubeba msalaba wetu kila siku na kujikana wenyewe. Hii inamaanisha tunasema “Hapana” kwa dhambi kila mara tunapojaribiwa. Ni wachache pekee ambao hupita katika njia hii.
“Si mapenzi yangu, bali mapenzi yako yafanyike”
Hakuna anayetaka kubishana na kupigana. Wanandoa huwa hawapendi mahusiano yao yawe baridi, lakini mara nyingi huwa baridi kwa namna fulani – Huwa wanabishana na kupigana. Kwa nini huwa wanabishana licha ya kwamba hawapendi iwe hivyo? Ni kwa sababau hawajaipata njia nyembamba iendayo uzimani. Kukosa uvumilivu, hasira, tuhuma, wivu n.k huwagawanyisha watu. Hicho ni “Kifo”. Kwa upande mwingine uvumilivu, wema, utayari wa kutoa na msaada, n.k. huwaunganisha watu pamoja. Huo ni uzima.
kumbadilisha, hivyo anaweza kuwa kama unavyodhani anapaswa kuwa – lakini hiyo siyo njia iendayo uzimani. Njia iendayo uzimani ni kusema “Hapana” dhidi ya dhambi katika asili yako mwenyewe ya kibinadamu, Hivyo hauiruhusu dhambi unazojaribiwa.
Ndipo roho hupata nguvu dhidi ya asili yako ya kibinadamu. Hii ndiyo maana ya kutembea katika roho hivyo hatubebi tamaa zetu za choyo. (Wagalatia 5:16) Hii itazaa matunda – unapata uzima, unapata matunda ya roho yanayotuunganisha pamoja. Hatuwezi kupewa tu matunda. Tunaweza kupokea roho mtakatifu kama zawadi, lakini kupata matunda ya roho lazima tuitii roho na kuchukia dhambi katika asili yetu ya kibinadamu yenye dhambi.
Hii ni njia ambayo wachache huipata! Watu wengi hawaipati kwa kuwa hawajioni walivyo wabaya wenyewe. Wanajishughulisha na kile wasichokipenda kwa wengine! Hii huenda pamoja na mahitaji ambayo mtu mwingine anapaswa kuyabadili, na “mauti” – uovu. Ubinafsi wetu ndio upo nyuma ya yote.
Yesu alitufundisha kuwa watumishi na kusamehe, na alisali “Siÿo mapenzi yangu , bali mapenzi yako yatimizwe!” wanandoa ambao huipata njia hii watagundua kwamba maisha yanakua yenye utukufu Zaidi na zaidi. Waumini wanaopita katika njia hii huwa pamoja kama walivyo baba na mwana. Uzima aliyokuwa nao baba – uzima wa milele hukua ndani yao, na furaha yao inakuwa Zaidi na Zaidi. (1Yohana 1:2) huu ni uzoefu wa walioipata njia nyembamba iendayo uzimani na ambao hutembea katika njia hii. Wale wasiokuwa na uzoefu huu hawatembei katika njia nyembamba.