Paulo alipoliandikia barua kanisa la Efeso, alianza kwa kuwaambia kwamba walikuwa wamechaguliwa na Mungu kabla ya kuumba ulimwengu! Sote tumechaguliwa na Mungu. (Waefeso 1:1-15)
Kuamini kwamba tumechaguliwa na Mungu ni sehemu muhimu katika Imani yetu; na pia Mungu aliyetuita ana nguvu ya kufanya na kumaliza kazi ambayo ameianzisha ndani yetu
Hakika Mungu hamuiti na kumchagua mtu “kwa ajali”. Mungu alituchagua kabla hajaumba ulimwengu. Alitusamehe dhambi zetu na tunaweza kukua kwake kwa kupitia neema tele aliyotupa katika hekima na uelewa.
Tumechaguliwa na Mungu kwa ajili ya tumaini jipya na bora.
Dhambi tulizorithi kutoka kwa mababu zetu zimekuwa zikitusababishia maumivu makali na mateso ulimwenguni. Lakini tukimfuata Yesu kristo, kuna tumaini jipya na bora kwa ajili yetu ambao tulizaliwa kwenye dhambi na tulikuwa watumwa wa dhambi.
Sasa kuna tumaini la kutoka dhambini na kuingia katika maisha ambapo tunashinda dhambi ambazo zilikua zimetufunga. Tunaweza kuja katika Maisha mapya kabisa ambapo tunatenda kwa njia ambazo Yesu angetenda, badala ya kufanya mapenzi yetu ambayo yanatupeleka kwenye mafarakano. Badala ya kufanya madai tunaweza kuwa wenye shukrani; badala ya kulaani tunaweza kubariki, n.k.
Hakuna wito mkuu kwetu kuliko kuitwa kutoka mbinguni na Mungu mwenyewe! Pia hakuna maisha makuu ama bora kuishi kuliko kuishi kwa ajili ya Mungu. Fikiria ni ajabu kiasi gani kwamba tunaweza kuwa sehemu ya kazi ambayo Mungu anafanya ndani ya watu wake kipindi hiki cha neema. Kila mtu anayehisi wito wa Mungu moyoni mwake anatakiwa kuufuata wito huu kwa moyo wote na uchaguzi wa kile Mungu alichotupa ndani ya kristo.
Tumechaguliwa kuwa wanafunzi wa Yesu.
Mungu haulizi kuhusu mambo yetu yaliyopita, historia ya familia zetu au tunachoweza kufanya peke yetu. Hutuita kuwa wanafunzi wa Yesu na kuwa kama yeye. Anaweza kufanya kazi ndani ya wanafunzi, wale wanaotaka kumfuata Yesu na kazi hiyo huanza pale tunapoacha maisha yetu ya zamani na kumkabidhi Mungu mioyo na maisha yetu. Kazi hii huendelea maishani mwetu tukiishi kama vile Paulo alivyoandika kwenye kitabu cha Wagalatia 2:20: “Nimesulubiwa Pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika Imani ya mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu.” Hii ni kazi kubwa ya Mungu ambayo huja tunapokuwa tumejikabidhi kwa Mungu na hatuishi kwa ajili yetu wenyewe tena.
Katika kipindi hiki cha neema ambacho tunaishi, Mungu hutupa kila kitu tunachohitaji ili kumfuata yeye. (1Petro 1:3-4) Mungu hufanya kazi na sisi na kutuadh ibu ili matunda ya roho yaweze kuwa uzima ndani yetu. (Waefeso 1:5-11; Waebrenia 12:11)
Tumechaguliwa kwa ajili ya wokovu wa kina.
Huchukua muda kabisa kuokolewa toka dhambini. Huchukua muda kupata asili mpya iliyojazwa matunda ya roho. Hivyo tunatakiwa kutumia wakati na fursa ambazo Mungu hutupa. Kila kitu ambacho Mungu hutuma katika njia yetu hutufanya kuwa huru kutoka dhambini Zaidi. Tunayaona maisha yetu wenyewe tunapokua katika hali ngumu. Maisha yetu binafsi ni dhambi ambazo huishi katika asili ya kibinadamu ambayo tumeirithi. (Petro 1:18-21) Tunapoyaona maisha yetu binafsi, tunapaswa kunyenyekea na kukubali, siyo kujitetea au kuelezea. Tunapoukubali ukweli pekee juu yetu ndipo tunapoweza kuokolewa dhidi ya dhambi hii, ambapo ni ukombozi mkuu, uhuru mkuu. (Waebrania 7:25) na hii ndiyo sababu kwamba tunaweza kuwa na furaha tele katika hali zote za maisha.
Ni tumaini kubwa na thawabu kumtumikia Mungu! Na inawezekana kwa kila aaminiye wito wake wa mbinguni na nguvu ya Mungu kuwabadiisha. Mungu anaweza kufanya kazi tukufu, lakini amini katika nguvu na msaada ambao Mungu ametupa kupitia injili. Hapa ndipo baraka za kiroho ndani ya kristo zipo kwa ajili ya wanaomtii! (Waebrania 5:9)