Tunawezaje kujihesabu kama wafu kwa dhambi?

Tunawezaje kujihesabu kama wafu kwa dhambi?

wote tunajaribiwa kutenda dhambi, lakini kama tunataka kushinda dhambi, tunahitaji kuchukua hatua!

16/11/20174 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Tunawezaje kujihesabu kama wafu kwa dhambi?

“Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake” Warumi 6:12

“Kufa katika dhambi” humaanisha kutokukubaliana na matakwa ya dhambi kwenye miili yetu

“Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kama wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu” Warumi 6:11. Katika tafsiri nyingine imeandikwa kwamba tunatakiwa “kufikiri” juu yako mwenyewe kama mfu, ingawa dhambi inahofiwa.

Wote tuna tamaa mbaya na matakwa ambayo yamefichwa katika miili yetu. Tunapojaribiwa, dhambi hizi “amka”, lakini hatupaswi kuziruhusu zitawale. Mapema pindi tunapokuwa na ufahamu juu ya tamaa mbaya au matakwa, lazima tujione kama wafu katika dhambi. Hii ni namna tunaweza kushinda dhambi katika maisha yetu. Wote tunajaribiwa pale tunapozama kutokana na matakwa yetu, ambayo hujaribu kututia mtegoni kufanya dhambi (Yakobo 1:14) Lakini kujaribiwa sio kutenda dhambi.

Kama Petro anavyosema, ”…. ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbal; Ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo.” 1 Petro 1:6-7

“Lakini mimi nawaambia, kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake” Mathayo 5:28. Kumbuka kwamba imeandikwa: “kumtamani”. Kwenye tafsiri nyingine imeandikwa “kufanya dhambi ya ngono naye”. Sheria inasema: Usitamani mke wa Jirani yako. (Kutoka 20:17.) Lakini ikiwa mwanaume atamuangalia mwanamke na kutaka kufanya dhambi ya ngono naye- kwa maneno mengine, amekubaliana na tamaa kwenye mwili wake badala yakujiona mwenyewe kuwa mfu katika dhambi, kufa kwenye tamaa hizi-kisha atakuwa tayari amekwisha kufanya dhambi kwenye moyo wake

Lakini mtume Paulo alisema kwamba aliitumikia sheria ya Mungu kwa akili yake. (Warumi 7:25.) Hiyo inamaanisha kwamba alitaka kuitii sheria ya Mungu.


Mfu kwa dhambi humaanisha kiukamilifu kusema Hapana kwa dhambi

Yakobo anauliza, “Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu? Mwatamani, wala hamna kitu; mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!” Yakobo 4:1-2

Ni tamaa mbaya za watu na tamaa za ubinafsi ambazo husababisha mapigano na mivutano katika makusanyiko ya kikristo kwa sababu watu hawajioni wao wenyewe kama wafu kwa dhambi-wafu kwa tamaa mbaya na tamaa za ubinafsi- na, kama matokeo, ni kama wameikubali dhambi. Lakini hakika hatujasema “Hapana” kwa dhambi mara tu tunapokuwa tumeitambua, na tunafanya hivi kwa kusema ‘Hapana’ kwa tamaa mbaya na matakwa ya kutenda dhambi hii.

Sheria ilikuwa ikifanya kazi baada ya dhambi kuwa imefanywa na ikaonekana kwa wengine. “Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili.” Warumi 8:3

Kazi ya Mungu katika Kristo iliingia ndani zaidi ya sheria ilivyoweza (tangu sheria iliweza tu kuchukua nafasi juu ya dhambi baada ya kuwa imeonekana); kazi hii ilichukua nafasi ndani ya mwili wa Yesu (kabla dhambi kuwa imefanywa na kuonekana). Hapo tamaa mbaya na tamaa za ubinafsi (mbayo pia inaitwa ‘dhambi ndani ya mwili’) ilihukumiwa na kulaaniwa. Ndiyo maana Yesu alisema “Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini mimi nawaambia, kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake”

Wale ambao ni wafu kwa dhambi huishinda dhambi

Yesu alikuja kuharibu kazi za shetani. Alifanya hivi kwa kuto-kuikubali dhambi,akishinda dhambi wakati wote alipojaribiwa, kupitia nguvu ya Roho ambayo iliishi ndani yake. Kwa namna hii dhambi ndani ya mwili wake ilikufa, lakini kwa malipo alifanywa hai na Roho.

Ingawa mafunzo yetu katika utauwa, kama tunavyopigana vita vizuri vya Imani dhidi ya tamaa mbaya na tamaa za ubinafsi kwenye miili yetu, tunaye Yesu Kristo kama Kuhani mkuu, kwa sababu alijaribiwa na ndio maana alikuja kutusaidia.

Wale tu wanaotaka kuacha kutenda dhambi hupitia vita hivi vya ndani dhidi ya dhambi na ushindi huu-na watakuwa pia zaidi na zaidi kama Yeye

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita katika Makala na Johan Oscar Smith ambayo mwanzo ilionekana ikiwa na kichwa “Pinga tamaa mbaya ndani ya mwili” katika jarida la BCC “Skjulte Skatter” (Hazina iliyofichwa) Aprili 1928. Imetafsiriwa kutoka kwenye Kinorwei na imebadilishwa kwa ruhusa kwa matumizi kwenye tovuti hii.