Unapokua na hofu, unamfanya Mungu awe mdogo na wewe kuonekana mkuu. Kiukweli unamwita Mungu muongo. Imeandikwa na G. Gangsø
Wanafunzi wa Yesu walipewa ahadi: “Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” Mathayo 6:33.
Pia imeandikwa kwamba baba yetu wa mbinguni anajua mahitaji yetu. Anajua; yeye si mjinga. Kuwa na mashaka ni sawa na kusema kwamba Mungu ni kipofu na mjinga na kwamba hawezi fanya lolote. Lakini baba yetu wa mbinguni si kipofu wala mjinga. Yuko makini sana. Kiukweli ana hesabu ya kila nywele katika vichwa vyetu. Unaweza kuwa na uhakika: Amehesabu kila dola uliyo nayo, mpaka senti ya mwisho. Anajua fika kiasi gani unahitaji kesho, keshokutwa na kwa miaka 10 ijayo! Mungu anajua kila kitu na anajali kwa kila kitu.
Mwachie hofu yako yote: Uhusiano na mwenyezi Mungu.
Sasa kwa nini tunakuwa na hofu? Yesu anasema “Basi, mkiwa hamuwezi hata neno lililo dogo, kwa nini kijisumbua kwa ajili ya yale mengine?” Luka 12:26. Mungu anaweza fanya kila kitu lakini sisi hatuwezi kufanya hata mambo madogomadogo. Tukifikiria juu ya hili, ni mantiki kwamba tunaweza kuliheshimu fungu hili “Mwachie hofu yako yote, maana hushughulika na mambo yenu” 1Petro 5:7
Lakini kufanya hivi, lazima tuwe na mahusiano binafsi na Mungu. Ni wanafunzi wake tu ndiyo wenye uhusiano wa namna hii, wale waliozaliwa mara ya pili na wana tumaini hai. Kama haupo na Mungu na hauna tumaini hapa duniani, siyo rahisi kumwachia wasiwasi wako wote. Hapana, unakua na hofu kwa nia njema.
Kwa kuamini neno la Mungu, milima ya hofu inaweza kuondolewa na kutoswa baharini. Ni kiasi gani cha hofu kitabakia upatapo tumaini hai katika kitabu cha warumi 8:28? “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.”
Ndipo mawingu yote ya hofu yatapotea na jua la haki litachomoza na uponyaji katika mabawa yake. (Malaki 4:2) Hofu hutufanya tuzeeke kabla ya muda wetu; Hutusababishia vidonda vya tumbo na kiungulia. Hupelekea uchovu na kukosa utulivu kwa mambo yasiyo ya msingi.
Mwachie hofu yako yote: Mawazo mapya mazuri.
Ushauri unajitokeza: “Msijisumbue kwa neno lolote” Wafilipi 4:6. Mara nyingi watu huwa wana hofu karibia kwa kila kitu. Ni ugonjwa wenye kuharibu, kama nyoka anayeteleza katika mawazo yako, anayaandama maisha yako ndani ya Mungu. Mawazo yako yanazunguka gizani, na mawazo hatari ya aina hiyo yanakukujia, zaidi na zaidi. Lakini ukimpa Bwana mizigo yako na hofu yako yote, mbingu hufunguka.
Katika kitabu cha ufunuo wa yohana 4:1 imeandikwa “Baada ya hayo naliona, na tazama, mlango ukafunguka mbinguni, na sauti ile ya kwanza niliyoisikia kama sauti ya baragumu ikinena nami, ikisema, panda hata huku, nami nitakuonesha mambo ambayo hayana budi kuwako baada ya hayo.” “Tazameni Mungu yu wenu” Isaya 40:9
Unapomwona Mungu, unatambua ni kiasi gani ulivyo mdogo na usivyo na matatizo yako yasiyofaa. Kabla hujamwachia wasiwasi wako, hofu ilitafuna nguvu na motisha yako, lakini sasa nguvu imekuja na nia ya kusimama na kutumika. Unajikuta hauongozwi na kupigwa na mawazo yako mwenyewe. Matatizo ya kuwa na hofu yamepelekwa mbali na maisha yako, hivyo unaweza wasaidia wengine kuwa huru na kuleta faraja katika nafsi zinazoteseka. Ndipo nuru yako itaangaza katika giza, na utakua mwangavu kama jua wakati wa mchana. (Isaya 58:10)
Jambo la kutia moyo limeandikwa katika kifungu hicho hicho “…. walishe wenye njaa, wajali wenye mahitaji na wanaoteseka” Hili ni pigo lenye nguvu dhidi ya hofu. Mungu huona vitu hivi na atakulipa”
Mwachie hofu yako yote: Mungu anaweza kufanya yasiyowezekana
Hivyo tujizoeshe kuwa katika hofu ya Mungu – tufanye mazoezi ya kumwachia hofu yetu yote. Hivi, bila shaka, moja kati ya “michezo ya kiroho” inayotumika sana unayoweza ifanyia kazi.
Kama Mungu ni mwingi wa rehema ambapo huzitupa dhambi zetu zote katika kina cha bahari, tunatakiwa tuitumie nafasi hii nzuri. Mwachie hofu yako yote! (1Petro 5:7) Mungu anaweza fanya mambo ambayo kwetu hayawezekani. (Mathayo 19:26)