Nini ningepaswa kufanya pindi nilipofanya kitu fulani kibaya pasipo kujua?

Nini ningepaswa kufanya pindi nilipofanya kitu fulani kibaya pasipo kujua?

Unajikuta bado unafanya vitu vibaya, licha ya kuwa hakika unataka kufanya kile ambacho ni kizuri.

19/5/20155 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Nini ningepaswa kufanya pindi nilipofanya kitu fulani kibaya pasipo kujua?

Kama mkristo, nilifanya makubaliano na Mungu kwamba sitofanya dhambi. “Basi dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake” Warumi 6:12-13. Lakini mara nyingi ninaona kwamba ninafanya vitu, na kisha baadae natambua kwamba nilichokifanya sio sahihi. Wakati huo ninakuwa nimekwisha chelewa – tendo linakuwa limekwisha kutendwa. Inamaanisha kwamba nimekwisha kutenda dhambi?

Nimekwisha yakabidhi Maisha yangu kwa Mungu na kuishi kwa ajili ya Yesu pekee. Nina mtazamo mpya akilini kwa sasa kwamba ninataka kufanya kile ambacho ni kizuri, na nimeacha kabisa tabia yangu ya zamani ya dhambi, na vitu vyote ambavyo najua ni dhambi ambavyo vinanitenganisha na Mungu.

Lakini ninajikuta bado ninajaribiwa kutenda dhambi. Kwa mfano, Ninajaribiwa kudanganya ili kuondokana na hali ngumu. Lakini hiyo “tamaa ya kutenda dhambi” ambayo ni sehemu ya asili yangu kibinadamu, sio lazima ziniongoze. Kwa msaada wa Mungu, ninaweza sasa kuona ninajaribiwa kutenda dhambi. Ndipo ninaweza kusema ‘Hapana’ kwa chochote ninachojaribiwa nacho na kuishinda dhambi.

Nimeanza pia kuona kwa kiasi gani ninafanya vitu ambavyo sikumaanisha kuvifanya, lakini ambavyo bado ni kinyume na matakwa ya Mungu. Kwa mfano, kabla sijatambua, nilikuwa na chuki na Rafiki ambaye anafanya vitu ambavyo sivipendi. Licha ya kuwa hitaji langu ni kuwa mwema kwa kila mtu, vitu hivyo vilitoka tu.

Sasa ninaelewa anachomaanisha Paulo  anaposema, “Maana sijui nilifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo,silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda” Warumi 7:15. Hata sijui kwamba ninafanya vitu hivi hadi pale ninapokuwa tayari nimekwisha vifanya. Hivyo ninatenda dhambi pasipo kujua; pasipo kupenda?

Matendo ya mwili

Kutenda dhambi, Lazima kwanza nitambue kwamba ninajaribiwa, na ndipo ninakubali jaribu. Ninapofanya kitu fulani kibaya pasipo kutambua kuwa ninajaribiwa kutenda dhambi, hicho ndicho kile Biblia inakiita “Matendo ya mwili”. (Warumi 8:13.)

Kila mtu ana tamaa mbaya za dhambi na matakwa ndani ya asili yao ya kibinadamu, na muda fulani yanatoka pasipo sisi kujua kabla kwamba yanakwenda. Hii sio sawa na kutenda dhambi. Hakukuwa na kipindi maalum ambapo nilithibitisha nilikuwa ninajaribiwa na nilihitaji kuamua ndio au la, nilikuwa naenda kusema ‘Ndio’ na kulikubali jaribu.

Inaweza kutokea, kwa mfano, kwamba ninaenda mbali na mazungumzo na ninaona baadaye kwamba nilikuwa nikimhukumu na kumkosoa rafiki yangu. Au ninatambua kwamba nilijibu bila kuwa na subira katika hali fulani. Nikaja kutambua kwamba kitu nilichokitenda hakikuwa matakwa ya Mungu; Haikuwa sahihi.

Wakati hili linatokea, bado nina nafasi ya kushinda! Lakini ninahitajika kukubali kile nilichokifanya – ikiwa ninajuvunia sana kukubali kwamba sikuwa sahihi, ndipo Mungu anaweza kufanya chochote na mimi. “Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hivyo husema, Mungu huwapinga wajikwezao, bali huwapa neema wanyenyekevu” Yakobo 4:6. Ninakubali kwamba kile nilichofanya hakikuwa mapenzi ya Mungu. Hakika ninataka kumtumikia Mungu, hivyo ninachukia kila kitu ambacho hakiko sawa na mapenzi yake, na ninachukua uamuzi thabiti kuwa macho zaidi baadae. Ninapofanya hivi, ninashinda baada ya kuwa nimefanya kitu kibaya. Hichi ndicho Biblia hukiita “kufisha matendo ya mwili” Warumi 8:23

Endelea

Ndipo ninahitaji kuendelea na kutoruhusu Shetani kunisababishia kuingia kwenye dhamiri mbaya. Kuvunjika moyo kamwe haitokuwa chaguo. Hitaji langu bado ni kufanya kile ambacho ni kizuri; hilo halijabadilika. “Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu” Warumi 7:20. Ilitokea, lakini sasa ilishapita. Sasa ninajua zaidi, na wakati ujao nitakuja kwenye hali ileile nitakuwa macho zaidi. Nitajua ni kitu gani ninajaribiwa nacho kwa urahisi zaidi na nitakuwa macho hivyo basi nitaweza kuona jaribu kwa wakati huu na kusema ‘Hapana’ kwa hilo

Paulo huendelea kuelezea: “……………….” Warumi 7:25. “Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu” Warumi 8:1. Hakuna hukumu! Akili yangu haikubaliani na “tendo la mwili” na Shetani hawezi kunihukumu.

Tuna rehema nyingi kutoka kwa Mungu. Hakika anataka tufanikiwe, na hutupa kila fursa tubadilike. (Warumi 12:2, 2 Peter 1.) Tunaweza kupata asili ya kimungu! Lakini ikiwa tunataka kushiriki katika asili ya kimungu, tunatakiwa tuwe huru kutoka kwenye asili yetu ya kibinadamu. Hivyo basi tunahitaji hali hizi ambapo tunaweza kuona asili yetu ya kibinadamu na kujifunza kujisafisha sisi wenyewe. (2 Wakorintho 7:1.) Hatuwezi kujua kipi kinahitaji kusafishwa kama hatuwezi kukiona mwanzo.

Kubadilishwa kabisa

Nilipoona kwamba nimehukumu au mwenye mashaka na wengine, licha ya kuwa sikumaanisha kufanya hivyo, ndipo ninajua kwamba kuhukumu au kuwa na mashaka ni vitu vilivyomo kwenye asili yangu ya kibinadamu ambayo ni rahisi sana kwangu kujaribiwa nayo. Sasa ninajua kipi ninahitaji kukifanyia kazi – ninatakiwa niachane na dhana ya kuwa mwenye kuhukumu na mwenye mashaka hivyo basi inaweza kubadilishwa na utu wema na rehema.

Mfano mwingine ungeweza kuwa ikiwa ninaangalia nyuma juu ya hali na kuona nilikuwa ninajifikiria binafsi, hata kipindi ambacho sikutaka kuwa mbinafsi, ndipo nilipata kuona ni kwa jinsi gani hii ilikuwa ni sehemu ya asili yangu ya kibinadamu. Sasa ninaweza kuchukua hatua na kuitumia kila nafasi ninayoiona kujifunza kutoa na kupenda, zaidi ya kujipenda mwenyewe.

Nilipokuwa nimeona kwamba nilikuwa nikiogopa, ndipo ninaona ni kwa kiasi gani zaidi ninahitaji kujifunza kuamini katika Mungu.

Orodha inaendelea. Sote tunajikuta kama binadamu ni dhaifu, lakini Mungu ni mwenye nguvu na atatusaidia. Atatupa kila kitu ambacho tunahitaji hivyo basi tunaweza kubadilishwa kabisa.

‘‘Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo. Hata vijana watazimia na kuchoka, na wanaume vijana wataanguka. Bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watapiga mbio, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.’’

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita kwenye Makala na Kate Kohl ambayo mwanzo yalichapishwa kwenye https://activechristianity.org/  na yamebadilishwa kwa ruhusa kwa matumizi kwenye tovuti hii.