Biblia inasema nini kuhusu uzinzi?

Biblia inasema nini kuhusu uzinzi?

Ni nini "uzinzi" kulingana na Neno la Mungu na matokeo ya uzinzi ni yapi?

16/2/20153 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Biblia inasema nini kuhusu uzinzi?

6 dak

Uzinzi ni pale ambapo mtu aliyeoa au kuolewa anakuwa na  uhusiano wa kimapenzi na mtu ambaye si mume ama mke wake. Biblia inalaani wazi hili kama tunaposoma katika Kutoka 20:14: "Usizini." Ukifanya hivyo, unavunja ahadi uliyotoa mbele ya Mungu kuwa mwaminifu kwa mwenzi wako wa ndoa.

Imeandikwa kwamba Mungu "kila kitu amekifanya kizuri kwa wakati wake," (Mhubiri 3:11) na wakati ambao ameruhusu kujamiiana ni kwa mwanamume na mwanamke ndani ya ndoa.

Kuwa na uhusiano huu wa kimapenzi kabla ya ndoa au na mtu mwingine baada ya ndoa ni kutotii moja kwa moja mapenzi ya Mungu, kama inavyosema katika Waebrania 13: 4: "Ndo ana iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu." Hata kama mwenzi wako angekubali uzini, hii haiifanyi kukubalika machoni pa Mungu.

Kaa mbali na usherati

Paulo anaonya wazi dhidi ya tabia zote kama hizo katika 1 Wakorintho 6:18: "Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo ." Tunapaswa kutumia mwili wetu kumheshimu yeye aliyeutoa, kama inavyosema katika 1 Wakorintho 6: 19-20: "Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu?, wala ninyi si mali yenu wenyewe. Maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi mtukuzeni Mungu katika miili yenu.

Na katika 1 Wathesalonike 4: 3-5 inasema: "Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama mataifa wasiomjua Mungu."

Yesu anasema kwamba ni uzinzi hata kama kwa kutamani moyoni na akilini mwako: "Mmesikia kwamba imenenwa, usizini; lakini mimi nawaambia, kila mtu atazamae mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake." Mathayo 5:27-28 .

Yesu pia anazungumzia jinsi tunvyopaswa kuchukulia uzito ili kuepuka dhambi kama hiyo: "Jicho lako la kuume likikukosesha, ling’oe ulitupe  mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum. Na mkono wako wa kuume ukikukosesha, ukate ukate uutupe mbali nawe; kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehanum." Mathayo 5:29-30.

Yesu anajua jinsi ya kutusaidia

Tunapojaribiwa kwa mawazo machafu, tunaweza kukumbuka kwamba Yesu alifanya iwezekane kwetu kushinda. Tunasoma katika Waebrania 4:15-16: "Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye aliyejaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji."

Katika kiti cha enzi cha neema, kupitia Yesu, tutapokea msaada tunaohitaji. Yesu anaelewa jinsi tulivyo dhaifu, na anajua hasa jinsi ya kutusaidia, kama inavyosema katika Waebrania 2:18 : "Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa."

Hakuna furaha ya kweli kwa Mkristo nje ya mapenzi ya Mungu. "Mafanikio" ya uzinzi ni mafupi sana lakini huzuni baadaye ni kwa muda mrefu sana. Heri kila mtu ambaye, kama Yesu, anachagua kufanya mapenzi ya Mungu, na hakubali majaribu, hata kama inamaanisha vita na mateso kwa muda. Kisha tutakuwa baraka na mfano tulipo. Na tunapokuwa waaminifu hapa duniani, tutakuwa na furaha, sasa na milele.

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii inategemea maka ya Steve Lenk iliyochapishwa awali kwenye https://activechristianity.org/ na imebadilishwa kwa ruhusa ya matumizi kwenye wavuti hii.