Katika uliwemwengu tunaoishi na katika mazingira tunayokulia, daima watu hujaribu kufanya mambo fulani yaonekane kuwa makubwa katika macho yetu na mambo mengine hujaribu kufanya yaonekane kama si chochote! Lakini yesu alituambia kwamba kinachoonekana kikubwa katika macho ya mwanadamu ni chukizo machoni pa Mungu. Luka 16:15. Chukizo ni kitu kibaya sana na chenye kuudhi ambacho hukufanya utamani kukitupilia mbali! Ni huzuni kubwa kung’ang’ania na kujishughulisha na vitu ambavyo ni chukizo kwa Mungu!
Mfano watu watamwangalia mtu mwenye elimu nzuri ulimwenguni mara kwa mara bila kujali namna anavyoishi. Anaweza ishi katika dhambi na kuwa mgumu na asiyependa watoto wake na asiye mwaminifu kwa mke wake N.k, lakini kama ana kazi nzuri na yenye malipo mazuri, ah! Huyo ni mtu mzuri machoni mw a wengi! Na pia kuna watu wasio na elimu nzuri, pengine wana kazi ya kawaida kama waudumu wa migahawa ama wafanya usafi, lakini ni wakweli na waaminifu – lakini kwa kuwa wana kazi ya “hali ya chini” wengi huwaona kuwa wa chini na kuwadharau!
Kama wakristo, tuna wito mkuu na mtakatifu sana, na ambao hautegemei hata kidogo katika elimu au historia ama rangi! Lakini kwa sababu ni machache sana yamesemwa kuhusu wito wetu mkuu, twaweza danganywa kirahisi na mawazo (roho) za ulimwengu huu. Umewahi sikia kamwe kwamba una wito mkuu na mtakatifu na wito wa kuwa kama yesu?
“Basi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi”. (Warumi 8:28-29)
Kuonesha jinsi wito wetu ulivyo mkuu, hebu tutumie mfano wa mtu mmoja ambaye amepata mafunzo ya udaktari. Siyo kama tu ni daktari wa kawaida lakini ni mtaalamu wa kwenye utafiti wa saratani. Hufanya utafiti mwingi na kugundua dawa mpya na namna ya kutibu watu wenye saratani kali. Na ana mafanikio ya kiwango cha juu! Hivyo, majarida ya kitabibu huandika kumhusu na anaonekana katika kurasa za mbele za magazeti na majarida. Watu hudhani kuwa hiki ni kitu kikubwa sana, na anaheshimika sana.
Sasa, daktari bingwa huyu anapokea mgonjwa. Anaugua saratani mwili mzima na zaidi ya hapo mgonjwa huyu ni mbinafsi sana, kujifikiria tu mwenyewe. Mke wake na watoto wake wanateseka sana juu ya tabia yake ya ubinafsi, na ana hasira kwa yale aliyotendewa na ndugu yake miaka iliyopita; na kazini ana wivu sana kwa sababu mtu mwingine amepandishwa cheo ilhali hakupandishwa… haya yote yanamfanya asiwe na furaha! Daktari bingwa wetu anamtibu mgonjwa huyu asiye na furaha na anapona kabisa saratani!! Saratani yake ilikua mbaya sana, ambapo kila mtu anazungumzia uponaji wake. Na daktari wetu anakua maarufu zaidi na zaidi!
Ni kweli mgonjwa anafuraha sana na anaondoka hospitali na tabasamu kubwa. Lakini anafika nyumbani, asili yake ya ubinadamu yenye dhambi inarudi tena na uchungu wake, wivu, ubinafsi na kukosa furaha vinaamka tena (Kwa kuwa ndiyo asili yake). Japo mwili umepona, maisha ni yenye huzuni kwake yeye na wanaomzunguka. Ni kweli daktari bingwa wetu aliweza kuuponya mwili lakini hakuweza kumponya dhidi ya uchungu wake, wivu, ubinafsi n.k. Hakuweza kumponya kutoka ugonjwa wa kutisha ambao ni dhambi ambayo huwafanya watu waumwe ndani yao….. Na majarida ya kitabibu kamwe hayawezi kuandika kuhusu ugonja huu wa kutisha! Na cha kushangaza zaidi: Japo watu wengi wanateseka sana na huu ugonjwa wa kutisha karibu hakuna mtu ambaye huzungumzia kuhusu hili.
Lakini unadhani kuna watu duniani wanaweza kukusaidia upate kupona ugonjwa huu wa kutisha? Kuponywa wivu, uchungu, ubinafsi, n.k? Ndiyo shukrani kwa Mungu, wapo!! Wapo ambao wameukubali wito mkuu na mtakatifu kutoka kwa Yesu na wameruhusu kufundishwa naye. Yesu alikuwa wa kwanza kushinda wivu, uchungu n.k Kamwe hakuzipa nafasi dhambi zote hizi zilizopo katika asili ya mwanadamu. (Waebrania 4:15). Na sasa yupo tayari kutusaidia kutoka katika dhambi sawa na hizo. (Waebrania 2:17-18) Na anaweza kutuokoa daima ili tusifungwe tena na dhambi hizi! (Waebrania 7:25): ”Basi mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kwelikweli” (Yohana 8:36).
Na cha kufurahisha zaidi: Tukiwekwa huru toka hizi dhambi, tunaweza saidia wengine pia kuwa huru kutoka dhambi hizi! Hivi ndivyo wito wetu mkuu na mtakatifu ulivyo! Na maneno sawa ambayo yesu alizungumza kwetu, na kwa jinsi alivyotuweka huru kutokana nayo, kwa mfano uchungu, na wivu, tunaweza kuwasaidia wengine pia kuwa huru! Ndiyo maana imeandikwa “jitunze nafsi yako na mafundisho yako. Dumu katika mambo hayo; maana kwa kufanya hivyo utajiokoa nafsi yako na wale wakusikiao pia”. (1Timotheo 4:6)
Na sasa unaweza kujiuliza mwenyewe: ni kipi bora zaidi? Kumponya mtu kimwili (kwa nje) ama kumponya mtu nafsi yake (ndani)? Hilo la mwisho ni wito mkuu ambao tunao! Yesu anakualika katika wito huu bila kujali historia ya maisha yako ilivyo! Ufuate wito huu!