Ni amani gani ambayo yesu hupatia?

Ni amani gani ambayo yesu hupatia?

Lengo la mwisho katika maisha haya ni kupumzika na amani katika hali zote, katika kila aina ya shida. Je! Tunapataje amani ya aina hii?

8/8/20194 dk

Na Ukristo wa Utendaji

Ni amani gani ambayo yesu hupatia?

7 dak

“Amani nawaachieni; Amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. Yohana 14:27. Yesu aliwapa maneno haya wanafunzi wake katika ujumbe wa kuwaaga, na kuwafariji. Hakuwapa amani ambayo ulimwengu hutoa, kwa hili tunatakiwa tufurahi sana.

Amani mara nyingi huwa imefungamana na kitu fulani. Amani ambayo ulimwengu hutoa huwa ni ya kipindi kifupi tu na inaweza potea ghafla kwa maana huwa inategemea watu wengine na vitu vya kidunia.

Aina hii ya amani huwapo tu wakati ambapo kila kitu kinaenda sawa, wakati ambapo watu wanazungumza vizuri kukuhusu na unapokea sifa na heshima, wakati ambapo afya yako na vitu vingine vinaenda sawa katika maeneo mengi. Watu wengi wameshuhudia kwamba amani hii inaweza potea muda wowote; lakini bado watu wengi wanaitafuta amani hii. Muda fulani kila kitu kinaweza onekana kuwa kizuri na chenye kupendeza na wakati unaofuata hali inaweza kuwa tofauti.

Amani ambayo Yesu hutoa.

Bwana aliyajua haya yote, ndiyo maana akaja na zawadi nzuri kwa ajili yetu; Alikuja na amani ya Mungu, amani katika hali zote! Hii ni amani ya aina tofauti kabisa, iliyotulia wala isiyobadilika ambayo haifungamani na watu wala ulimwengu huu. Imefungamana thabiti mbinguni.

Kwa asili sisi ni watoto wa “ghasia”, wasumbufu. (Hesabu 24:17) Hatuifahamu njia ya amani. Warumi 3:17) Hivyo tutaipataje amani hii? Siyo kitu ambacho tunakipata tu moja kwa moja. Amani huwa inakua sehemu ya maisha yetu zaidi tunapozitii amri za Mungu, maneno yake. “Mtu akinipenda atashika neno langu; na baba yangu atampenda nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.” Hakutakua na chochote zaidi ya amani ukiwa na baba na mwana moyoni mwako na akilini mwako. (Ufunuo wa Yohana 3:20)

“Laiti ungesikiliza ammri zangu! Ndipo amani yako ingalikua kama  mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari”. Isaya 48:18.

“Wana amani nyingi waipendao sheria yako, wala hawana lakuwakwaza.” Zaburi 119:165.

Amani hii imejazwa na imani na tulizo na uhakika na  nguvu. Paulo alikua nayo. Aliteseka sana, aliteswa, alichukiwa, alidhalilishwa,alitukanwa, alitendewa vibaya n.k. Alipitia magumu mengi sana, lakini alikuwa jasiri ambapo aliandika katika kitabu cha Warumi katika sura ya 8:38-39 “kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwepo wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe chochote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika kristo Yesu Bwana wetu”.

Alijua hayo mateso yalikokua yanaelekea. Tunaokolewa haswa kupitia mateso, siyo bila mateso. Katika nyakati ngumu tunapata kujitambua na kumjua Mungu, udhaifu wetu na nguvu ya Mungu! Mtu mmoja angefikiria kama nisingekua na magumu mengi ningekuwa na amani, lakini haiwezi kuwa kwa namna hiyo. Lengo la mwisho ni kuwa na pumziko na amani katika hali zote, katika hali zote ngumu. Hivi ndivyo mwalimu na mitume waliishi. Kila atakae kuishi maisha ya kumuogopa Mungu atakuwa na uzoefu huo.

“Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni  mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.” Yohana 16:33. Hii ni ya ajabu! Kuushinda ulimwengu na kila kilichomo! Ni ushindi wa namna gani! Hii njia ni yetu pia. (1Yohana 5:4)

Kuingia katika amani ya Mungu

 

Kuna mengi ambayo hutuleta kwenye machafuko katika asili yetu ya kibinadamu, kama vile kiburi, “kwa kujua zaidi”, kutokua na uvumilivu, hasira, Kutokua na rehema, n.k. huwa tunahisi kuwa na mambo haya tunapopitia nyakati ngumu. Huwa tunakosa utulivu, na matokeo yake tunakosa amani na Mungu katika hali zetu. Lakini kupitia katika neema ya Mungu nguvu yake, kupigana vita vizuri vya imani tunapata ushindi dhidi ya mambo haya, kutakua na amani kati yetu na ndani yetu. Fikiria ni vizuri kiasi gani hali hii inapotokea katika maisha yetu,, sio tu karibu nasi bali ndani yetu pia.

“Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.” Warumi 12:21. tukifanya hivi, matokeo yake yatakuwa amani, lakini tukifanya kinyume kama ambavyo wengi tumejionea matokeo yake yatakuwa machafuko, siyo tu karibu nasi lakini pia ndani yetu. Lakini wale ambao huushinda uovu kwa wema, taratibu watajifunza njia ya amani vyema. Hii ni nzuri kiasi gani! Itakua ndiyo amani tunayoihitaji!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii imejikita katika makala ya Svein Kronstad amabyo awali ilichapishwa katika https://activechristianity.org/ na imepewa ruhusa kutumika katika tovuti hii.