Kutoka katika shida ndogo hadi utukufu wa milele

Kutoka katika shida ndogo hadi utukufu wa milele

Hakuna Mtu Anayependa Kuwa na Majaribu na Matatizo, Lakini Kwa Nini Tunayahitaji ili kuja katika Utukufu wa Mungu?

3/1/20253 dk

Written by Aksel J. Smith

Kutoka katika shida ndogo hadi utukufu wa milele

Utukufu wa milele sio hali yetu ya asili

" Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso." Waebrania 2:10.

Ni baraja na faraja kujua kwamba Kristo amekuwa na huruma juu yetu, na kwamba sasa anatupeleka kwenye utukufu wa milele kwa mkono wenye nguvu.

Kwa asili, hatuna utukufu ndani yetu wenyewe, kwa hivyo kuja kwenye maisha ya utukufu, sasa na milele, tunahitaji kuwa kama Kristo zaidi na zaidi. Ikiwa tunataka kupokea maisha Yake na asili Yake, Yeye anahitaji kutuongoza kupitia kila aina ya hali. (2 Petro 1:4; 1 Petro 1:6-9.) Anatubadilisha na kututakasa kupitia mateso, na kwa kupitia haya yote tunajifunza kujua njia yake njema na mapenzi yake kwetu, kama tunavyosoma katika Zaburi 119:67, " Kabla sijateswa mimi nalipotea, Lakini sasa nimelitii neno lako."

Ikiwa tunajua kwamba tuko chini ya mwongozo wake mwema na wenye nguvu juu ya njia ya utukufu katika kila kitu kinachokutana nasi, matokeo yatakuwa kwamba shida zetu zitakuwa kwa muda mfupi na zitatuletea utukufu mkubwa zaidi kuliko shida hizi ndogo. " Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana." 2 Wakorintho 4:17 .

Kristo atakapokuja kumpeleka bi arus wake katika utukufu, litakuwa kundi la watu ambao tayari wamepitia maisha yake ya utukufu katikati ya giza na uovu wa ulimwengu. Katika majaribu mengi ya maisha waliumbwa na kubadilishwa kupitia mateso kwa njia ile ile kama Yesu Mwenyewe.

Kila mmoja wa watu hawa atakuwa na uzoefu mwingi wa ajabu kutoka katika safari yao kupitia maisha - na watashukuru kwa majaribu tofauti ambayo Mungu aliwapitisha katika njia yao ya utukufu wa milele.

Wale ambao walikuwa na kiburi na wakaidi watakuwa na hadithi za nyakati ambapo walivunjwa na kuwa wanyenyekevu na wema. Watatoa sifa na shukrani kwa Mungu kwa milele yote kutokana na shukrani kwa matokeo haya makubwa na yenye baraka. Fikiria kama wangekuwa na hali rahisi tu na wangebaki wakaidi na kujivuna maisha yao yote!

Tunaweza kuja katika utukufu wa milele wa Mungu kama mashujaa hawa!

Yusufu alitupwa shimoni na kufungwa gerezani akielekea kuwa mtawala. Daudi alikuwa uhamishoni, aliteswa na watu wenye wivu  akielekea katika ufalme wake. Zaburi zake za kinabii na zilizobarikiwa zilizaliwa wakati wa mateso, shida, vita, na upinzani.

Tunahitaji kuwa na hekima ya Mungu ili aweze kututumia, na tunaweza tu kuipokea kupitia mateso na uaminifu katika majaribu ya maisha.

Yesu pia alijaribiwa kama sisi kwa sababu alikuwa na asili ile ile ya kibinadamu ambayo tunayo. Aliteseka  alipojaribiwa na kujifunza utii kwa mambo aliyoteseka (Waebrania 5: 8); na kwa njia hii alikua katika hekima. Alifanywa mkamilifu kupitia mateso, kama tunavyosoma katika Waebrania 2:10. Hakuna mtu aliye mtiifu na mwaminifu kama Yeye. Alivumilia majaribu yote ya maisha bila kutenda dhambi. Kwa kweli yeye ni mkuu anayestahili kati ya ndugu na dada zake. (Waebrania 2:10,14-18; Waebrania 4:15Waebrania 5:7-9.)

Hebu tutegemee furaha inayotusubiri, kama Yesu alivyofanya, na kumsifu Mungu kwa kila kitu tunachopitia njiani kuelekea katika utukufu!

Chapisho hili linapatikana katika

Makala hii inategemea makala ya Aksel J. Smith ambayo ilionekana kwanza chini ya kichwa "Katika njia ya utukufu" katika chapisho la BCC ya "Skjulte Skatter" (Hazina zilizofichwa) mnamo Juni 1953. Imetafsiriwa kutoka  Kinorway na imebadilishwa na ruhusa ya matumizi kwenye tovuti hii.