“Lakini zikimbie tamaa za ujanani.” 2Timotheo 2:22. “….. mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.” 2 Petro 1:4.
Hatuwezi kugusa kitu ambacho ni kichafu bila kuwa sisi wenyewe . Kwa hiyo imeandikwa, “Msiguse kitu kilicho kichafu!” 2 Wakorintho 6:17. Biblia imeandika mengi kuhusu ukweli kwamba tunapaswa kujitakasa wenyewe kutoka kwenye kila kitu ambacho hufanya miili yetu na roho zetu kuwa chafu, na tufanye bidii kuwa watakatifu kwa kuwa tuna hofu ya Mungu. (2 Wakorintho 7:1)
Unajijaza na nini?
Tumejiweka wazi kwa kila aina ya uchafu kila siku, na haiwezekani kujiweka safi bila kuuchukia. Watu wengi hudadisi mambo ya wengine, hupenda kujua nini kinachoendelea. Haiwezekani kwa watu kama hawa kujiweka safi; kwa hiyo hawawezi kuja katika asili ya uungu, wala kuwa watakatifu kama ilivyoandikwa kwenye 2 Wakorintho 7:1. Kikubwa wanachoweza kufanya ni kujiongoza wenyewe.
Tunasoma kwenye Ufunuo wa Yohana 2:24 kwamba baadhi ya watu wengine hujisifu kwa kujua kwa undani mambo ya shetani, kama wanavyosema. Lakini yesu anasema kwamba anajua mawazo ya kila mmoja, na atamlipa kila mmoja kwa kile alichofanya. (Ufunuo 2:23)
Tunahitaji kufanya bidii kujiweka safi kutoka kwenye majaribu yanayokuja nje ya uwezo wetu. Kwa hiyo kwa nini tuchague kutazama kitu au kusoma kitu ambacho kitaamsha tamaa kwenye asili yetu ya dhambi? “Bali mvaeni Bwana Yesu kristo, wala msiuangalie mwili, na hata kuwasha tamaa zake.” Warumi 13:14.
Ikimbie dhambi: kimbia kwa ajili ya maisha yako!
“Maana kwa kule kufa kwake, aliifia dhambi mara moja tu; lakini kwa kule kuishi kwake, amwishia Mungu.Vivyo hivyo nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.” Warumi 6:10-11
Hili ni jambo la muhimu kufanya katika fikra zetu. Ikiwa tunataka kuja katika asili ya kimungu, kuwa watakatifu, hivyo tunapaswa kuwa waaminifu katika fikra zetu. Tukiendelea kufikiria kuhusu mambo ambayo yanatujaribu, hatuyakimbii! Hatuyachukii. Lakini kama tunayachukia, hutupelekea kupata asili ya kimungu katika eneo hili! Hatuwezi kuishi maisha haya bila kusimama mbele ya uso wa Mungu na kuishi katika roho.
“BWANA wa majeshi asema hivi, waulizeni sasa makuhani katika Habari za sheria, mkisema. Mtu akichukua nyama takatifu katika upindo wa nguo yake, naye akagusa kwa upindo wake mkate au ugali au divai au mafuta au chakula chochote, je! Kitu hicho kitakuwa kitakatifu? Makuhani wakajibu, wakasema, La. Ndipo Hagai akasema, kama mtu aliyetiwa najisi kwa kugusa maiti, akigusa kimoja wapo cha vitu hivi, je! Kitakuwa najisi? Makuhani wakajibu, wakasema, kitakuwa najisi.” Hagai 2:11-14.
Hapa tunaona namna gani onyo linavyofaa kuhusu kuikimbia shambi! Mungu anapokuwa karibu na tunakuwa tumebarikiwa kwenye ibada za maombi au kupitia kusoma neno la Mungu, hivyo ni muhimu kwamba tusiruhusu macho yetu na fikra zetu zielekee katika kila mwelekeo. Hatuwezi kuutunza “utakatifu” mioyoni mwetu na kwenye fikra zetu kama hatukikimbii kila kitu kilicho najisi; kama hatulichukulii kwa uzito, tutakuwa najisi kutokana na kile tunachotazama na kusikiliza. Israeli ilikua kama hivyo. Kila kitu walichofanya, na kwa kila kitu walichotoa sadaka, kilikua najisi.
Hata watu wenye hofu kuu ya Mungu, kama akina Yohana aliyewaandikia, walihitaji maonyo kama haya. (1Yohana 2:13-17)