Yesu yuko wazi kabisa anaposema kwamba lazima tuzaliwe mara ya pili ikiwa tunataka kuona ufalme wa Mungu. Tunaweza kusoma hili katika Yohana 3: 3-6: "Yesu akajibu akamwambia, Amini, amini nakuambia, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Nikodemo akamwambia, Awezaje mtu kuzaliwa, akiwa mzee? Aweza kuingia tumboni mwa mamaye mara ya pili akazaliwa? Yesu akajibu, Amini amini, nakuambia, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa na mwili ni mwili; na kulichozaliwa na roho ni roho."
Yesu hazungumzii juu ya kuzaliwa mara ya pili kimwili. Anazungumzia juu ya akili mpya - mabadiliko kamili ya kiroho.
Kwa nini ninahitaji kuzaliwa mara ya pili?
"ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na nia, tukawa kwa tabia yetu Watoto wa hasira kama na hao wengine." Waefeso 2:3 . Kabla ya kuzaliwa mara ya pili, ninaongozwa na tamaa zangu za dhambi, vitu ambavyo "mimi" ninataka. Na kwa kawaida hii ndiyo inayodhibiti mawazo na maamuzi yangu yote. Lakini tamaa hizi za dhambi hazielekei kwenye maisha ya Kristo, ambayo nimeitiwa. (1 Petro 2:21.) Kujitoa kwa tamaa za dhambi kama vile kiburi, uvivu, tamaa, wivu, ubinafsi, na aina nyingine nyingi za uovu, husababisha dhambi.
Yesu anaeleza jinsi tulivyo kabla ya kuzaliwa mara ya pili: "Kwa kuwa wasema, mimi ni Tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi." Ufunuo wa Yohana 3:17.
Ninapoona na kukubali kwamba hivi ndivyo nilivyo kweli, basi niko tayari kuzaliwa mara ya pili. Hakuna kitu ambacho ninacho kama mtu wa asili kinachoweza kumtumikia Mungu. Ninapoona na kukubali kwamba siwezi kutenda mema, basi Mungu anaweza kuchukua nafasi. Ninahitaji kuacha kila kitu, mapenzi yangu mwenyewe, mipango yangu mwenyewe na mawazo n.k. kuzaliwa kwa Roho - ni kuzaliwa upya kwa akili na moyo wangu. Kisha siongozwi tena na tamaa zangu za dhambi, lakini ninaongozwa na kile Roho anachoniambia. (Warumi 6:11.)
"Nimesulubiwa pamoja na Kristo; lakini ni hai; wala si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu; na uhai nilio nao sasa katika mwili, ninao katika Imani ya mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu." Wagalatia 2:20.
Kwa kweli, bado nina asili yangu ya kibinadamu ya dhambi ambayo inataka kufanya mapenzi yake mwenyewe, lakini sasa tamaa hizi haziniathiri tena. Badala yake, ninasikiliza kile Roho anasema. Mawazo yangu ya zamani lazima yabaki "kusulubiwa na Kristo" na maisha mapya ambayo nimezaliwa nayo ni "maisha ya Kristo". Watu wanapaswa kuona maisha ya Yesu ndani yetu. (2 Wakorintho 4:11.) Ni kwa sababu nimezaliwa na Roho na Roho anaishi ndani yangu, kwamba nina uwezo wa kupinga na kusema Hapana katika majaribu, kubaki "kusulubiwa" kwa tamaa za asili yangu ya dhambi ya kibinadamu na kuishi kwa ajili ya Kristo. (Waroma 15:13))
Soma zaidi: Ninatoaje Maisha yangu kwa Yesu?
Tamaa Mpya
Wakolosai 3 inatoa maelezo mazuri sana ya Mkristo aliyezaliwa mara ya pili, kuanzia na: "Basi mkiwa mmefufuliwa Pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maana mlikufa, na uhai wenu umefichwa Pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa Pamoja naye katika utukufu." Wakolosai 3:1-4.
Najua kwamba nimezaliwa mara ya pili ikiwa najua moyoni mwangu kwamba hamu yangu sio ya kitu chochote cha dunia hii, lakini hamu yangu ni kumtumikia Mungu pekee na kumruhusu awe na udhibiti katika maisha yangu. Tamaa ya kuishi milele badala ya kitu chochote katika ulimwengu huu. Tamaa kama Yesu aliyokuwa nayo: "Si mapenzi yangu bali yako yafanyike." Luka 22:42.
Ni pale ninapokuwa tayari kuacha kiburi changu mwenyewe, ukaidi na uwezo wa kibinadamu, na kufuata uongozi wa Roho, basi mapenzi ya Mungu yanaweza kufanywa. Kisha ninaona kwamba kwa nguvu ya Roho, kila kitu kinawezekana. Ninaweza kuhamisha milima katika maisha yangu. Kisha ninaweza kushinda dhambi, ambayo nilikuwa nikidhani haiwezekani. Ninakuwa mtu aliyebadilika; Kiumbe kipya. Ninamruhusu Mungu aniunde kuwa mtu ambaye anataka niwe.
Kuona Ufalme wa Mungu
Katika Waefeso 1: 17-19 Paulo aliomba kwamba macho ya Waefeso yafunguliwe: "Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye; macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjuw tumaini la mwito wake jinsi ilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake watakifu jinsi ulivyo; na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadri ya utendaji wa nguvu za uweza wake."
Kama macho yangu yamefunguliwa, naweza kuuona ufalme wa Mungu. Kisha naona zaidi ya mambo ya dunia hii; Ninaona kile ambacho kina thamani ya kweli. Kwa ufalme wa Mungu huja kila kitu ambacho ni kizuri kweli, katika ulimwengu huu na milele. Kutafuta ufalme wa Mungu ni jambo bora zaidi ambalo mtu anaweza kufanya.